Bima ya afya kwa wote isigeuzwe 'tozo' ya kuonana na daktari

Bima ya afya kwa wote isigeuzwe 'tozo' ya kuonana na daktari

G-Mdadisi

Senior Member
Joined
Feb 15, 2018
Posts
165
Reaction score
100
Moja ya maamuzi muhimu ambayo yatafanywa na Serikali na kimsingi yanachochea tabasamu zaidi kwa mamilioni ya watanzania ni hili la BIMA KWA WOTE ama 'Bima kwa kila Mtanzania.'

Nimefarijika sana kuona hata waziri mwenye dhamana ya Wizara ya Afya Nchini, Dkt. Gwajima kuthibitisha kwamba zaidi 85% ya watanzania wapo nje ya mfumo wa bima ya Afya. Hii ni hatari kwa taifa.

Kumbuka hawa watanzania 85% wanaozungumziwa hapa wote ni wale wazazi/ndugu zetu vijijini ambao hatma ya afya zao wakiugua wanategemea wauze kilo ya mahindi, Mpunga, uwele, dagaa au kulima vibarua. Ndipo wapate shilingi elfu 1 wakanunue Panadol dukani angalau ili wapoze maumivu ya kichwa baada ya siku ndefu ya kuunguzwa na jua kali.

Hizo 15% zilizobaki ni mchanganyiko wa wale wenye vibarua vidogo ambavyo taasisi zao zinawalipia bima kule NHIF au kwingineko pamoja na wale watanzania daraja la kwanza ambao akiumwa na kichwa bima yake inamruhusu kwenda Hospital yoyote aipendayo bila kikwazo.

Wakati ambapo serikali inaelekea kukamilisha mpango huu marhaba kwa watanzania, ni lazima kwanza ijibu swali la iwapo mpango huu utafanikiwa, 'je, ni katika hospitali, vituo vya vyote (public/private) ambapo watanzania wataruhusiwa kwenda wakati wowote kupata huduma waitakayo kwa kutumia hizi bima? Au ni bima za kumsaidia mwananchi kuepukana na ulipaji wa TOZO za kuonana na daktari kifuatacho ni "Nenda pharmacy kanunue dawa hizi hatuna"

Moja ya kilio kilichopo kwa sasa hasa kwa wale wenye bima za kawaida wanakutana na wakati mgumu wanapohitaji huduma kwani vituo na hospitali nyingi zimegubikwa na ubaguzi wa aina ya bima ambazo zinapokelewa na kupelekea mhusika kutumia kiwango kikubwa cha pesa kuipata huduma hiyo jambo ambalo linakatisha tamaa wengine kujiunga na bima za afya kwa kuamini si msaada kwao tena.

BIMA YA AFYA kwa wote ni wazo jema sana, wema na ubaya wake utabaki mikononi mwa serikali juu ya namna itaamua kulitekeleza.

Bima hizi zikitumika kama tiketi za kupunguza gharama za kumuona daktari huku Dawa na huduma nyingine muhimu zikakosekana, bado ni tatizo.

Wasalaaam
#GMdadisi
 
Sisiyemu ni kwa kurukia rukia mambo hawajambo, juzi namsikia waziri mchakato wa bima ulikwama tangu 2010 sasa waliokua wanatumia bima walitoa wapi.

Serikali kama serikali wameshindwa kuwekeza kwenye afya, matokeo yake inafikia hatua hadi bohari ya dawa inaidai serikali pesa mingu. Chukulia hizo tozo wanazokusanya wangesema Percent fulani serikali inakuchangia bima ya bei hii wewe unatakiwa kulipa bei hii tungekua tumevuka hatua.


Ili swala la bima sijui kama tutaweza kama tu swala la vitambulisho vya taifa limekua hadithi ndefu.
 
Serikali ina pesa ila haina vipaumbele, kuna mambo ya kufanyika mara moja yakaisha kwa usimamizi thabiti tu lakini inapenda sana kufanya mambo nusu nusu!

Kuna jambo la billion 100 ambalo zikiwekwa na kusimamiwa litakamilika kwa wakati ila utashangaa serikali imekimbilia swala la billion 600 ambazo hizo pesa hazipo! Wataunga unga 100b kila baada ya miezi 6 mpaka mradi uishe ni miaka 4 imeisha!

Sometimes kuwa mtanzania ni kama kero yani!
 
Back
Top Bottom