Watoaji Bora kwa bima za afya ni jubilee, strategies na Assemble Insurance (mwanzoni walikua wakiitwa AAR+) Kama ushawah kuona mahospitalini. Mfumo wa bima za afya huenda sambamba na KIWANGO CHA PREMIUM/ADA PAMOJA NA BENEFITS/FAIDA AU TUSEME HUDUMA ATAKAZOPATA. Hio inamaanisha sio kila coverage utakayochukua au kukatia itakusaidia kwenye hospital yoyote. Cha kwanza kabisa kabla hujaenda kwenye hizo kampuni kwa ushauri wangu kama kweli unataka utibiwe hizo hospital basi usiwe na premium chini ya million 1.2+ otherwise kampuni zote utaona ni wahini.kwann nasema hivyo;
Gharama ya vipimo na kumuona dactari kwenye hospital kubwa ni tofauti na hospital zingine. Unaweza kushangaa benefits zako zinaisha kabla hujapata hata dawa na matibabu(nimeeleza kifupi). So lazima ujipange mkuu.
Kuhusu kampuni jubilee+strategies imesambaa zaidi nchini na wana huduma nzuri ila Assemble Insurance Wana huduma Bora zaidi na licha ya kutosambaa nchi nzima Wana option ya wew kuomba hospital yoyote na popote ikupatie huduma as long as mtawasiliana nao na huduma Yao ni 24hrs. Unapokata pia NHIF au tuseme tu kampuni zote msingi kwanza kabisa angalia benefits then fanya maamuzi.
Hata hizo jubilee, strategies na Assemble Wana vifurushi vya bei rahisi kabisa mpk 300k+ lakini vinaminya benefits ambapo ukienda mfano Aghakhan utaishia kupata vipimo tu.
Yangu ni hayo machache