A
Anonymous
Guest
Naombeni mtusaidie kupaza sauti au kutafuta ukweli kuhusu bima ya afya inayotolewa na NSSF kuna ukiritimba unaifanywa na baadhi ya wamiliki wa hospitali wakishirikiana na wakuu wa makampuni binafsi kwa kuwataka wafanyakazi wote wa kampuni kutibiwa hospitali moja bila kujali unaishi wapi?
Mfano mimi naishi Gongo la Mboto lakini inanibidi nikatibiwe Tegeta, inavyoonekana ni dili la mmiliki wa hiyo hospitali na viongozi wa kampuni maana hata fomu wanatujazia wao viongozi.
Lakini ukienda NSSF kuwauliza wao wanasema utaratibu ni kuchagua hispitali moja katika orodha ya hospital watakazo kuontesha ambao kiukweli zimetapakaa Dar es Salaam yote, lakini kampuni haitaki inataka wote twende hospitali moja ambayo ipo Tegeta na wengine tupo mbali na huko Tegeta.
Tunaomba mtupazie sauti maana kila sehemu nchi hii kuna maadili ya unyonyaji na uonevu nipo tayari hata kutaja hiyo kampuni lkn jina langu lihifadhiwe.
Ingawa pia wapo wafanyakazi ambao walijiunga tangu zamani na NHIF wao wanatibiwa hospitali tofauti tofauti, lakini sisi ambao tulichelewa tulilazimika wote kusajiliwa kutibiwa Tegeta bila kujali unaishi wapi, na kama hutaki basi hupewi usajili wa bima ya afya ya NSSF, mimi nimejisajili na ninaishi gongo la Mboto hata huko Tegeta nilikua sipajui lakini kuna siku nilizidiwa nikaenda huko yaani ni mateso kwelikweli na wakati hapa gongo la Mboto kuna hospitali inaitwa KITONGA na inapokea kadi za NSSF kwa nini tukatibiwe Tegeta?