Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 15,460
- 24,233
"Ndugu zako wanakupenda, kuwa kwako na Bima ya Maisha inaonyesha Unawajali Pia"
Umuhimu:
Maisha yamekuwa magumu na ya gharama sana, hata kitu kama kifo / mazishi /Misiba yamekuwa mzigo kwa familia na jamii na sababu ni jambo la ghafla unaweza ukakuta kifo chako kinawasumbua na kuwatia hasara na gharama watu wako wa karibu wanapokusitiri kwa kuanza kuchangishana na kutoana upepo.
Suluhisho:
Kumekuwa na hii biashara mpya ya Bima ya Maisha ambayo wanapewa vikundi, ni jambo jema sana. Huduma hizi zinatolewa na baadhi ya kampuni za Bima kwa kupitia mabenki tofauti. Jambo hili ni jema sana ambalo nashauri ndugu, familia katika vikundi vyao vya watu kuanzia kumi na kuendelea wajichange na kupata huduma hii sababu ni pesa ndogo na wanachopata kama mmoja wao akifariki au ndugu zake wa karibu wanaweza kupata hadi milioni kumi kwa gharama ya kuchangia chini ya elfu kumi kwa mwezi.
Tatizo:
Uelewa wa wengi je wanachokinunua au kukipata wanakifahamu, sababu kwa sasa mkienda kama kikundi moja ya kigezo ni kwamba mtu awe chini ya miaka 75, jambo ambalo ni sawa kwa mtoa huduma sababu risk ya wewe kufa baada ya miaka 75 ni kubwa.., ila tatizo lililopo kama mtu amekata BIMA hii tangia ana miaka 15 na anarenew kila mwaka akifikisha miaka 75 ukimkatalia hio itakuwa ni sahihi kulingana na aina ya Bima aliyochukua lakini je anaelewa kwamba aina aliyochukua ni ya term (muda mfupi) na sio Permanent (ya Maisha mpaka mtu akiacha kutoa Pesa au Akifa)
Aina za Bima ya Maisha:
Kuna aina mbili; Term na Permanent; Term ni kila baada ya muda fulani mnakaa na kurenew kwa terms mtakazokubaliana (nadhani nyingi wanazotoa hapa kwenye hivi vikundi ni Term) na kuna ile Permanent ambayo utalipwa kama mlivyokubaliana na mtaendelea na mkataba huo mpaka siku ukifa au ukiacha kulipia malipo mliyokubalina (kama mlikubaliana ulipe kila mwaka, mwezi n.k.)
Hitimisho:
Bima hii ni muhimu sana, hususan kama unajali watu wako wa karibu na hautaki wapate matatizo au kuingia kwenye gharama siku ukiondoka..., ila ni vyema watoa huduma wakawaelewesha watu kwamba huenda hii unayochukua ni term yaani ya muda. Yaani BIMA kwamba hautakufa kwa mwaka huu ila usipokufa mpaka unafikisha miaka 75 huenda wapendwa wako hawatakuwa covered kama ulivyodhani na itabidi wachangishane ili wapike ubwabwa siku wanakusindikiza.....