Macbook pro
JF-Expert Member
- Jul 15, 2020
- 722
- 1,030
Na kama huyu Mtumishi aliyekopa pesa hizi akaacha kazi kwa hiari yake kwa sababu zake binafsi, bima inahusikaje au Bank litaenda kumtafuta huyu aliyeacha kazi alipe mkopo wake ama mzamini atawajibika ama Bima italipa kiasi cha pesa kilichobakia ?Kwa mfano muombaji ni mtumishi wa umma, analipa kwa makato ya mshahara kila mwezi, sasa akafariki kabla mkopo haujaisha. Basi familia yake na mali zake hazitakaa zikasumbuliwa. Naamini ata ikitokea amefukuzwa kazi pia.
Ila ata wanaokopa kwa mali zisizoamishika mfano nyumba, ikitokea nyumba imeungua au ghorofa kama la Kariakoo limevunjika, hautasumbuliwa.
Kwa kifupi kama zilivyobima nyingine, inafaida zaidi kwao kuliko kwako.
Habari zenu wakuu!
Ninatumaini mko pouwa asee, ninashida moja juu ya ufahamu wangu juu ya Bima ya Mkopo ambao mtu akichukua mkopo Bank. Hii Bima ya mkopo imekaaje au sheria inasemaje kuhusu hilo ? Ni katika mazingira gani hiyo Bima inafanya kazi na mwombaji wa mkopo ananufaikaje na hii Bima?
Mabenki au Taasis zinazotoa mikopo zinanugaikaje ? Mwenye ufahamu tafadhari naomba anisadie niko gizani nahitaji kufahamu hili
Ahsante sana mkuu, hizi nondo nikienda kwenye tovuti ya Shirika la Bima la Taifa nitazikuta?
Kwenye red, bima ya mkopo inamlinda mtoa mkopo dhidi ya kupoteza fedha zake ikitokea mkopeshwaji amefariki au amepata janga lolote linaloweza kupelekea ashindwe kulipa deni.
Kwa mfano, umekopeshwa na taasisi fulani ya kifedha na mkopo umekatiwa bima Shirika la Bima la Taifa (NIC), ikitokea umefariki, kwa kuzingatia Kipengele Na. 6.0 cha Sera ya Bima (Credit Life Assuarance Policy), mkopeshaji atapeleka madai ya kulipwa kiasi cha fedha ambacho ulikua bado hujalipa pale umauti ulipokukuta.