Bima za afya ni hatari sana kwenye vituo binafsi vya afya

Kifupi hizo situation za kufikirika haziko kwenye fani ya udaktari duniani kote
Hospitali ni huduma sio biashara.Haina cha mambo ya target kama mtu unauza njugu
Watu kuumwa huwezi weka target kuwa mwezi huu wataumwa mia na kuja hospitali
Hospitali ni huduma sio biashara?? kuwa serious kidogo tafadhari
 
Nilichanganyikiwa, maana walimpa prescription ya dawa za kifafa za kutumia mwaka mzima, bahata nzuri ndio alikuwa ametumia wiki tu.

.., utasingiziwa magonjwa ya gharama gharama ili wafikisi mifuko ya bima, na hapa mlengwa mkubwa ni NHIF..
Hiyo Bima inayoweza kutoa prescription ya dawa ya mwaka mzima kwa mara moja ni bima ya aina gani?
Kama mlengwa ni NHIF basi hapa umepotosha maana wao prescription wanaruhusu za siku 30 tu maximum.
 
Hiyo ya kwako ni special case watu mamilioni wanatibiwa na bima ya afya kila siku kwa miaka hospital za private kubwa na ndogo hawajapata hilo tatizo la kubambikwa magonjwa

Nina kisa cha namna hiyohiyo nitakuja nacho

Siku hizi kama Huna uelewa na mambo ya kitabibu na vyema utafute Dokta wako unayemuamini. Ûkienda hospital umshirikishe kîla kitû hata kama siô daktari ya hospital uliyoenda
 
Hiyo ya kwako ni special case watu mamilioni wanatibiwa na bima ya afya kila siku kwa miaka hospital za private kubwa na ndogo hawajapata hilo tatizo la kubambikwa magonjwa
Ni tatizo kubwa Tanzania. Hata ukienda kwa malipo cash usipokuwa mwangalifu unabambikiwa ugonjwa ili wapate fedha. Siyo hospital zote lkn zipo baadhi au baadhi ya ma-dr. Na wengine ni vilaza.
 
Aseee!! Umenipa mwanga
,
 
Una bima mkuu?
Ushawahi ugua?

Baada ya vipimo hivo ulienda kupima Tena hospital nyingine?

Binafisi niliwahi enda nina dalili za maralia
Nikamweleza vyote

Cha ajabu nikaandikiwa nipime Hadi mavi nikakubali.

Naenda maabara akachukia damu na akanipa chupa mbili za kinyesi na mkojo.

Nilipo enda kupokea majibu Kwa Dr naawambiwa na uric acid,amonia yaani vipimo vyote vya damu!

Mbaya zaidi walinipa na Ngoma japo majibu hakunipa!

Tunakuja kwenye dawa Sasa hapo ndo nilichoka nimepewa madawa mengi Naya gharama kubwa Hadi nikachoka kabisa.

Nikaona hapa nipite government hospital nikapime upya maana nilkuwa nimeogopa foleni ya pale.

Nilikuwa maralia Sina,minyoo Sina na magonjwa mengine nilipewa dawa gharama yake si zaidi ya 7000 tu

Kule imepigwa 117,000/=

Bima ni Assemble

Zile dawa nikampa mshikaji tu ana kaduka ka madawa kuwa utauza hizi dawa.

Kama Bado yajakukuta ipo siku utakutana nayo kulazwa Huwa nikugusa tu na ukikubali utakaa hata siku3 mle
Hiyo ya kwako ni special case watu mamilioni wanatibiwa na bima ya afya kila siku kwa miaka hospital za private kubwa na ndogo hawajapata hilo tatizo la kubambikwa magonjw
 
Mkuu hii ushawahi nikuta Mimi mwenyew nimeajibu hapo juu

Hii ni ya mtoto wangu Ambae alikuwa na mwaka mmoja na tu miezi kadhaa

Mtoto alikuwa anachemka na kuharisha sana.

Mama tulimwambia akasema msimpeleke hospital ni meno tu hayo Yana msumbua akatuambia dawa simple tutengeneze awe anaoga na kunywa mle mle anayooga tukaona huu ni uzamani

Tukambeba Hadi private hospital
Wife akatoa maelezo kama ilivyo na Mimi nikisikiliza.
Dr akamwangalia

Akasema ameishiwa maji Tena mngechelewa ingekuwa mbaya zaidi akapewa kitanda.

Sasa nikawa na wasi wasi mtoto kaharisha Jana na leo tu na anyonya vzr tu kaishiwa maji lini

Bahati nzuri Kuna Dada yangu ni Dr pia kaka ni nurse nikawaambia nikawaambia na mama alivyotuambia wakasema wote kama anatoa meno mrudusheni tu nyumbani ni kawaida wakatuandikia tu dawa ambazo haikuzidi hata 5000.

Nikachamaa nikamwambia Dr leteni form nisaini kuhusu julazwa hapa hapana tumeona tuende hospital kubwa zaidi yenye huduma ya vip tukalazwe huku.

Tukawa tumeondoka pale. Tukatengeneza dawa tuliyofundishwa na mama dogo hakuongezwa maji hata tone. Nabaada ya muda mwili ukapoa ukarudi kawaida akabaki kuharisha Tena mara chache.
 
Kifupi hizo situation za kufikirika haziko kwenye fani ya udaktari duniani kote
Hospitali ni huduma sio biashara.Haina cha mambo ya target kama mtu unauza njugu
Watu kuumwa huwezi weka target kuwa mwezi huu wataumwa mia na kuja hospitali
Bado hujui jinsi gani hizi hospital binafsi zinavojiendesha. Zipo kifaida zaidi na hasa kwenye watumiaji wa bima ya Afya maana ndo wengi sana kuliko wagonjwa wa Cash.

Kwa upande wa wagonjwa wa Cash wao ni rahisi kuruka viunzi kwani ukimbambikia lundo la dawa anaenda kununua kwingine famasi za nje ya hospital. Sasa hawa wa bima inakua ni ngumu kwao.

Na hii strategy wanaitumia kwa ajili ya kibiashara kupata faida maana ya management wanakaa na madaktari kabisa na kuwambia hizo mbinu za kuongeza mapato bila kutoa huduma stahiki.
Nimekua kwenye hii field ya afya najua watu wanavyoumizwa na hospital bila wagonjwa wa bima ni Ngumu sana kutoboa. Usipinge kila kitu
 
Kubambikiwa magonjwa sina uhakika. Ila nachojua unaweza kupewa madawa ambayo hayana ulazima. Mfano mm binafsi niliwahi pewa panadol na aspirin za kutuliza maumivu. Nilikuja shtuka nipo home. Nikajiuliza hizi ni common zinajulikana vipi kwa madawa ambayo sijui?
 
Kwamba kisa maaadili hayaruhusi ndio guarantee kwamba wanfuata hayo maadili?! Pengine wameweka monthly quotas za kumeet? How am i to know?!
How are you to know?
Kwamba hujui!!
Kutokana na kutojua wawezaje kukataa kwamba ulichoandika ni uongo?
Yaani ikiwa hujui jambo, basi lolote unalofikiria wewe ndo linakiwa sahihi?
Halafu wasema unajielewa!!!
 
Hiyo Bima inayoweza kutoa prescription ya dawa ya mwaka mzima kwa mara moja ni bima ya aina gani?
Kama mlengwa ni NHIF basi hapa umepotosha maana wao prescription wanaruhusu za siku 30 tu maximum.
Hazikutolewa mara moja za mwaka mzima, bali scheme ya dawa iliyokuwa imeandaliwa ni ya mwaka mzima, (means ni medication inayokamilika kwa mwaka mmoja) kwamba kila zinapoisha zinaenda kuchukuliwa.., na kwa Vipimo tu na dawa ambazo alishapewa za mwezi nadhani, billed amount ilikuwa zaidi ya milioni 1. Sasa can’t imagine mwisho wa huo mwaka ilikuwa inakuja ngapi kama ingeendelea..
 
It happened tupo advance, jamaa eti kaumia wakati tunacheza Moira. Tukasema, si bima zipo, Wacha tumpeleke hospital, walichofanya kule ni kumchua tu na kumpa dawa nyingine kwamba atakua anachua. Kuja kusoma form ya bima, inasema jamaa amefungwa POP, madawa mengi kweli 😂

It happens kwenye hz hospital za private..na ndio maana siku hz nyingi zinaenda bima sana kuliko wa cash, maana kukata kwenye bima ni rahisi sana
Unaenda hospital unarud na mfuko wa madswaa kama vle unaenda kuanzisha famasi 😂
 
How are you to know?
Kwamba hujui!!
Kutokana na kutojua wawezaje kukataa kwamba ulichoandika ni uongo?
Yaani ikiwa hujui jambo, basi lolote unalofikiria wewe ndo linakiwa sahihi?
Halafu wasema unajielewa!!!
Suala la wewe kurule out vitu ambavyo nimeviona na kuviexperience kwamba sio maadili ndiocho nina kipinga, kitu kimefanyika 1,2,3 ambavyo sababu pekee ninayoiona yenye logic na inaayomake sense ni kuongeza mauzo tu.., kama unasababu nyingine itoe
 
Madokta wanaofanya hivyo wanapaswa kufutiwa leseni zao
 
Labda hio hosp huyo dokta awe ana hisa zake hpo, au awe analipwa kwa commission za kias atachokiingiza.. vinginevo ni ngumu maana pesa itaingia kweny account ya hosp tena baada ya miez hta miwili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…