sembo
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 4,350
- 3,451
Hapa anamzungumzia Vincent Bossou, yule Beki kiboko ya Drogba.. Namnukuu..
"Korea Kusini ni moja ya nchi ambazo wachezaji wanalipwa vizuri na kwa ujumla wachezaji wakubwa huondoka Ulaya kwenda nchi za Asia kama China, Korea, Japan, Qatar, Saudi Arabia kufuata maslahi mazuri.
Mchezaji anapotoka nchi kama hiyo kuja nchi masikini za Afrika, lazima kuna namna na Yanga SC wanatakiwa kabla ya kutoa fedha kumsajili Bossou wawe wamejiridhisha hakuna tatizo.
Lakini kama utakuwa usajili wa presha na shinikizo la kuwahi dirisha la usajili, haitakuwa ajabu Yanga SC wakasajili mchezaji ambaye Desemba watavunja Mkataba kwa kumlipa na kumruhusu aondoke."
Bossou mwenyewe ndo huyu hapa, akiwa kazini.
View attachment 274126
View attachment 274127
Bin Zubeiry Anaendelea.. Hapa anamzungumzia wakala Gibby Kalule, aliyemleta Bossou.
"Si unangalia mtu ana misuli, wasifu mzuri- unampa fomu na Mkataba mnono. Huyo wakala ambaye amewaletea Yanga SC Bossou ndiye aliyewaletea Sherman na ndiye ambaye aliwaletea Azam FC mchezaji anaitwa Leonel Saint-Preux.
Leonel alifukuzwa Azam FC ndani ya miezi miwili kutokana na utovu wa nidhamu na kiburi.-
Aliwachukua wachezaji wengine wa Azam FC, Kipre Tchetche, Kipre Balou na Didier Kavumbangu akaenda nao kulala nje ya kambi timu ikiwa Kigali, Rwanda kwenye Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Waliporudi asubuhi na kuulizwa, yeye aliwajibu kifedhuli viongozi wa Azam FC na timu iliporejea Dar es Salaam akatupiwa virago. Azam FC sasa hawataki kumsikia Giby Kalule wakikumbuka balaa la Leonel" ... mwisho wa kunukuu.
NOTE: Cha kufurahisha huyu beki katili leo ametimiza miaka 29 na miezi 6 net.. Hivyo ni bado kinda kabisa.
SOURCE: NI AINA GANI YA USAJILI HUU INAFANYA YANGA SC? | BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE