Binadamu anaweza kupata CoronaViris kutoka kwa Wanyama?

Binadamu anaweza kupata CoronaViris kutoka kwa Wanyama?

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
Virusi vya #Corona ni familia kubwa ya virusi ambayo ni vya kawaida kwa wanyama. Wakati mwingine, watu huambukizwa virusi hivi ambavyo baadaye vinaweza kuenea kwa watu wengine

Kwa mfano, Ugonjwa wa #SARS (Severe Acute Respiratory Syndrome) uliosababishwa na Virusi vya familia ya Corona (SARS-CoV) mwaka 2003 ulioanzia China, virusi vyake vinahusishwa kutoka kwa Paka

Aidha, MERS (Middle East Respiratory Syndrome) uliogundulika mara ya kwanza mwaka 2012 huko Saudi Arabia ulisababishwa na virusi jamii ya Corona (MERS-CoV) vinavyosambazwa na Ngamia

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), hadi sasa haijathibitika mnyama gani ni chanzo cha ugonjwa wa COVID19, japo baadhia ya taarifa zinadai ni Popo

Ili kujilinda, mfano unapotembelea soko ya wanyama hai, jaribu kukwepa kugusana na wanyama hao lakini pia kwepa kugusa sehemu walipo wanyama hao

Weka vizuri nyamba mbichi, maziwa na vitu vingine vitokokanavyo na Wanyama ili kuepuka kuambukizwa virusi hivyo kwenye chakula kibichi. Usile vitu kama nyama au maziwa mabichi au yasiyoiva vizuri

Maambukizi.jpg
 
Upvote 0
mbona wamasai hawaumwi hata hii corona hutasikia mmsai kaambukizwa
umewahi kusikia mmsai anaumwa Maralia?
 
Ushauri;tuache kula wanyama na wadudu wa hovyo

Sent from my TECNO K8 using Tapatalk
 
Habari wakuu
Kuwa sasa dunia ipo kwenye mashaka ya janga kubwa la maambukizi ya corona
Kama mjuavyo kwa sasa maambukizi makubwa yapo kwa binaadamu lakini je kuna uwezakano maambukizi kuhama na kwenda kwa wanyama hususani hawa wafugwao?

Tusaidiane mawazo ya kitaalam na tafiti na sio maombi

Karibuni
IMG_20200422_115449.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom