Binadamu tuna mapungufu/madhaifu yetu, lakini huyu jamaa sikuona mapungufu yake

Binadamu tuna mapungufu/madhaifu yetu, lakini huyu jamaa sikuona mapungufu yake

A JUSTMAN

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
439
Reaction score
555
martin-luther-king-freedom.jpg

“And I say to you, I have also decided to stick to love. For I know that love is ultimately the only answer to mankind's problems. And I'm going to talk about it everywhere I go. I know it isn't popular to talk about it in some circles today. I'm not talking about emotional bosh when I talk about love, I'm talking about a strong, demanding love. And I have seen too much hate. I've seen too much hate on the faces of sheriffs in the South. I've seen hate on the faces of too many Klansmen and too many White Citizens Councilors in the South to want to hate myself, because every time I see it, I know that it does something to their faces and their personalities and I say to myself that hate is too great a burden to bear. decided to love.”

Namtafakari sana huyu ndugu Martin Luther King JR. maisha yake namna alivyoishi na watu wa rika zote na kujitoa katika kupigania haki za watu weusi huko Marekani(USA).

Dr. Martin Luther King JR. alikuwa ni mchungaji/pastor na mwanaharakati kiongozi wa Civil right movement na wachambuzi wa mambo mbalimbali wanasema huyu ni mtu mwenye uwezo mkubwa sana akiwa anahutubia watu na kujenga hoja, kushawishi watu wanaomsikiliza na hakika katika karne ya 21 hajatokea mwingine zaidi yake duniani.

Falsafa yake ya passive na non violent resistance, misimamo yake thabiti ya kile anachokiamini na hasa upendo wake kwa wengine vilimfanya awe kipenzi cha wengi.
Hotuba zake nyingi zipo mtandaoni tafuta hii inayoitwa
- BEYOND VIETNAM,
- THE OTHER AMERICA,
- THE CASUALTIES OF THE VIETNAM WAR,
- I've been to the mountaintop nk,nk,nk.

Nyingine hii alipanga kuitoa lakini aliuawa kabla ya kuhutubu,
- Why America May Go to Hell.

Ninapomtafakari huyu mwanaharakati akiwa kama binadamu mimi binafsi sioni madhaifu yake, yani kama tulivyo binadamu wengi tuna mapungufu kama chuki dhidi ya wenzetu, sifa, tamaa, hasira, wivu, kulipa visasi, wagumu kusamehe, wabinafsi na tunapenda sana ukuu au madaraka/mamlaka na mengine mengi sana.

Sasa Martin Luther King JR. naona tu zile hulka zake nzuri daima inawezekana humu wapo wanaomfahamu vizuri huyu mtu zaidi nimjuavyo kwa mapungufu yake kama kweli yapo waeleze hapa ili tuyafahamu .
 
Uzi huu upo lockup kwani shida nini JamiiForums nimeandika jana hadi leo ni zaidi ya masaa 24 lakini tu "awaiting moderation!" kunani?
 
Wananikera hata mm hawa wanavyokawiza kupublish agrriiiiiii inauzi
 
Mwa 1965 director wa FBI J Edgar Hoover ali mtrack Martin Luther King jr kwa kufunga vifaa chumbani kwake na kwenye simu yake aligundua mambo mengi tu yasiyo faa ya Dr King. King alikuwa na mapungufu mengi sana na uchafu mwingi tu lakini. Alipigania alicho kiamini na alipigania haki za weusi, hakuna binadamu mkamilifu na yeye alikiwa ni binadamu hakika hakuwa mkamilifu.
 
WEWE MLETA MADA BADIRIHSA HEADING,HAKUNA MWANADAM MKAMILIFU DUNIANI,NI MUNGU PEKEE ,NADHANI UMEHEUKA NA MICHOCHETO YA KIHISIA,
DUNIA HII AWEPO MKAMILIFU?HATA IBRAHIM MWENYWE ALIKUWA SI MKAMILIFU HEBU JIULIZE,

THINK TWICE KABLA HUJATOA THREADY,UNAWEZA UKAABIKA
Ndiyo maana nikaeleza mapema hii ni maoni yangu sasa wewe uoneshe mapungufu ya King ili tuyajue ni rahisi tu.
 
Mwa 1965 director wa FBI J Edgar Hoover ali mtrack Martin Luther King jr kwa kufunga vifaa chumbani kwake na kwenye simu yake aligundua mambo mengi tu yasiyo faa ya Dr King. King alikuwa na mapungufu mengi sana na uchafu mwingi tu lakini. Alipigania alicho kiamini na alipigania haki za weusi, hakuna binadamu mkamilifu na yeye alikiwa ni binadamu hakika hakuwa mkamilifu.
Waligundua yapi hayo eleza tufahamu
 
waligundua nini?
 
Martin Luther King ni mmoja ya watu ninao waheshimu sana duniani. nawaheshimu sana. wapo watu kadhaa wasiozid 5 ninaowaheshimu sana. sana duniani. and this man is one of them. ukisikiliza speeches zake yu will discover he was an orator, he was the speaker and the speech himself aliongea toka moyoni kwa kile alichoamini. ukisikiliza i have a dream, au i have been to the mountain top, utanielewa. mimi nina audios zake zote. the man alikuwa akihubiri upendo na alifanya upendo.

kibinadamu alikuwa na mapungufu yake lakini yasingeweza kuficha mazuri yake. hakuwa mtakatifu lakini alihusika kwa kiasi kikubwa kuibadilisha dunia ya leo. ni mmoja kati ya watu wenye akili sana na mwanamapinduzi.
 
Ufinyu Wa akili ya mleta mada maana hajui hicho kichwaa kinauzito kiasi gani
 
Mkuu mleta uzi,
Kuhusu mapungufu nakubaliana na wengi kwamba LAZIMA AWE NAYO.
Namkubali pia maana alikuwa ANAYAISHI yale ALIYOYAAMINI.
Hotuba zake ninazozipenda ukiacha izo ulitaja ni pamoja na:

WHAT IS YOUR LIFE BRUEPRINT,

LOVE YOUR ENEMY,

THE DRUM MAJOR INSTICT na

IF I HAD SNEEZED (Bila shaka ni sehemu ya I HAVE BEEN TO THE MOUNTAIN TOP)
 
Martin Luther King ni mmoja ya watu ninao waheshimu sana duniani. nawaheshimu sana. wapo watu kadhaa wasiozid 5 ninaowaheshimu sana. sana duniani. and this man is one of them. ukisikiliza speeches zake yu will discover he was an orator, he was the speaker and the speech himself aliongea toka moyoni kwa kile alichoamini. ukisikiliza i have a dream, au i have been to the mountain top, utanielewa. mimi nina audios zake zote. the man alikuwa akihubiri upendo na alifanya upendo.

kibinadamu alikuwa na mapungufu yake lakini yasingeweza kuficha mazuri yake. hakuwa mtakatifu lakini alihusika kwa kiasi kikubwa kuibadilisha dunia ya leo. ni mmoja kati ya watu wenye akili sana na mwanamapinduzi.
Hii nayo umeiskia? Beyond Vietnam au Why I'm opposed to the war in Vietnam kama hujaiskiliza embu itafute humu ndani anawajibu watu waliokuwa wanamwambia asizungumzie chochote/asipinge vita ile ilokuwa inaendelea ya Vietnam kwani kupinga vita nchi yako inapokuwa vitani ni sawa na uhaini. Ni hatari tupu mkuu. Hapa mie nilikubali kuwa kweli binadamu wapo ambao wana uwezo usio wa kawaida hakika.

Anasema "They ask me... why are you opposing the war Dr. King?...
 
Back
Top Bottom