Binadamu tuna mapungufu/madhaifu yetu, lakini huyu jamaa sikuona mapungufu yake

Tuna mtukufu sana wa karne ya 21 yupo Tz anaitwa sizonje yy hadi ana malaika wanaoshuka akiomba kuja kuzima hata social networks[emoji81] [emoji81] [emoji81]
 
Elezea basi alivyokuwa mzinifu, alizini na nani weka na reliable source tafadhari.
La uzinifu mkuu halina ubishi na linajulikana wazi. Hata mke wake Coretta katika baadhi ya interview alishakiri kuwa kuna kipindi hata aliwaza talaka.

Mleta mada naona ana mapenzi mahaba kiasi cha kukufuru. HAKUNA BINADAMU ALIYE MKAMILIFU NA ASIYE NA MAPUNGUFU. Mleta mada angeeleweka zaidi kama angejikita katika uadilifu katika harakati na falsafa zake.

Tunapozungumza juu ya viongozi hawa tutambue kuwa nao walikuwa binadamu na tujaribu kutenganisha harakati zao na ubinadamu wao. Mohammed Ali amekufa shujaa pamoja na ukweli kwamba yeye alikuwa ni womanizer wa waziwazi akisafiri na wanawake tofauti tofauti katika mapambano yake mbalimbali. Mema aliyotenda na alichokuwa akikipigania vinafunika mapungufu ya kibinadamu unless kama tunatafuta malaika!

Namheshimu sana Mwl. Nyerere (wahafidhina wa Kiarabu hasa Faiza na Mohammed Said mtanisamehe) si kwa sababu hakuwa na kasoro za kibinadamu bali ni kutokana na ukweli kwamba harakati zake na falsafa zake alizoziamini aliziishi. Aliamini kabisa kabisa katika uhuru wa mtu mweusi pamoja na ujamaa wake; na alichukia rushwa na ufisadi kwa maneno na vitendo. Siyo hii mianasiasa iliyomfuatia inasema hichi halafu inatenda hichi.
 
Tayari mmeshakimbilia Google na Wikipedia kukopi na ku-paste. Aaaargh!!!
 
The man did not have a dream,,,,The dream had him.
 
Umenitoa nje ya mada kidogo. Yesu alikua na mapungufu gani? Yameelezwa/andikwa katika kitabu gani ama chapisho gani?
 
Jamaa alikuwa kichwa hiv kwa Africa unaweza kumfananisha na nani
Dr. James Emman Kwegir Aggrey huyu aliishi (October 18, 1875 – July 30, 1927)
ni mghana lakini ni FORGOTTEN HEROE.
Tofauti ya huyu na King ni kwenye influence King alifanikiwa sana kwa kuwa na ushawishi mkubwa, huyu hakuwa na ushawishi mkubwa.

Hapa nimemnukuu anasema hivi...
“YOU CAN PLAY SOME MUSIC
ON THE BLACK KEYS OF AN ORGAN;
YOU CAN PLAY SOME MUSIC ON THE WHITE KEYS;
BUT TO MAKE THE BEST MUSIC,
YOU NEED BOTH THE BLACK AND WHITE KEYS”.
 
Ambatanisha hiyo interview ya Coretta tumsikie.
 
Kati ya watu 5 unaowaheshimu sana duniani umemtaja mmoja ni King, wengine ni nani hao wataje tuwafahamu.
 
*UJUMBE MZITO WA PAPA FRANCIS*

*Hakuna familia isiyo na mapungufu. Hatuna wazazi wasio na mapungufu, sisi pia si wakamilifu, hatuoi au kuolewa na mtu asiye na mapungufu, kadhalika watoto wetu nao si wakamilifu. Tunayo manung'uniko au malalamiko kila mmoja dhidi ya mwenzake. Tumevunjana moyo na kukatishana tamaa. Kwa hiyo, hakuna ndoa iliyokamilika wala familia iliyoboreka bila kuwa na mazoea au utamaduni wa kusameheana.*

*Msamaha ni nguzo au msingi wa utulivu wa akili na uhai wa roho zetu. Kama hakuna msamaha, familia inakuwa uwanja wa migogoro na mlipuko wa ugomvi. Panapokosekana msamaha, familia inaugua. Msamaha unahuisha moyo, kwa kusafisha fikra na kuufanya moyo kuwa huru. Binadamu asiyesamehe hana amani moyoni na wala hana urafiki au muunganiko na Mungu.*

*Maumivu ni sumu inayodhuru na kuua. Hebu kiponye kidonda hicho cha moyo endapo kuna dalili za kujiumiza. Mtu asiyesamehe anajisababishia mwenyewe ugonjwa wa mwili, kiakili na kiroho. Ndiyo maana familia inapaswa kuwa sehemu ya uhai na si kifo; eneo la uponyaji na sio mahali pa magonjwa; jukwaa la msamaha na si la uovu. Msamaha huleta furaha pale uchungu ulipoleta maumivu; huleta uponyaji hata pale ambapo maumivu yalisababisha magonjwa.*

Ujumbe huu wa Baba Mtakatifu umfikie kila mmoja wetu leo katika familia yake. Leo basi tuutafakari ujumbe huo muhimu.

*TUMSIFU YESU KRISTO*
 
Kuna movie J Edger Hoover, inahusu maisha ya mkurugenzi wa upelelezi wa Marekani wa miaka ya 60, 70, katika moja ya jambo alilofanya ni kufuatilia/kunasa kwa siri maongezi ya simu au mambo anayofanya MLK ofisini. Ndipo vitendo hivyo viliponaswa pia.
Je una uhakika ulichokiona kwenye hiyo movie ni halisi?
 


Aliiba Jina ambalo siyo lake na kulifanya lake, Martin Luther ni Mwanamapinduzi hasa aliyeibadilisha Dunia ya leo kama tuijuavyo, Martin Luther original ndiyo chanzo cha Makanisa yote Duniani kuanzia British Anglican church, Danish Church, Swedish Church, US Baptist Church, kwa kifupi Kanisa lolote lile la Kizungu lisilo sehemu ya Kanisa Katoliki leo lilianzishwa na Martin Luther original, hivyo huyu wa Martin Luther King wa USA ameiba tu jina na kuligeuza lake na amefanikiwa kiasi kwamba kuna binadamu wengi wanafikiri Martini Luther Mwanamapinduzi ndiyo huyu mchumia tumbo wa USA, kumbe siyo!
 


Usichanganye Martin Luther King (USA) na Martin Luther Mwanamapinduzi, ni watu wawili tofauti kabisa!
 


Niambie kaibadilisha vipi Dunia Martin Luther King? Sema labda kaibadilisha USA lkn siyo Dunia!
 
Alipingana na sheria za kanisa katoliki.


Hata wewe unachanganya Martin Luther King mchumia tumbo wa USA na Martin Luther original Mwanamapinduzi, ni watu wawili tofauti mmoja ni wa USA King alikufa miaka ya 60' mwingine ni Mjerumani aliyeishi karne ya 16 huko, kuwa mwangalifu hapo, ni watu wawili tofauti kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…