Binadamu wa kwanza kuzaliwa na kuua

 
Dah..... Kudadadeki.... Sijui walipata wapi madem..... Au waliwatafuna dada zao? Nauliza tu [emoji15]
 
Kwa wale ambao walikuwa hawafahamu huyo ndo kaini binadamu wa kwanza kuzaliwa na kuua
Aliwekewa Alama na Mungu ili watu wa NODI wasimdhuri.Haya kumbe Adam na Hawa si watu wa kwanza kuumbwa bali walikwepo wengine tayari kule nchi ya NODI.
 
Adamu na Hawa waliumbiwa Uarabuni kule Iraq na bustani ya Eden ipo Iraq.Kwa maana hiyo wanadamu wote chimbuko Lao ni Waarabu.Sasa ni lini na kwa sababu gani yakatokea mabadiliko (evolution )tukapata Waafrika,Wachina,Wazungu na indigenous (wenyeji) yaani Waarabu.Na kwa nini hiyo evulution sasa imesimama na mataifa mengine mapya hayazaliwi tena.
 

Hiyo biblia inavyosema watu wameanzia Iraq ni uongo tu...hamna la kweli hapo!
 
Kwahiyo mwanamke mmoja alikuwa anazaa watoto wawili wawili asubuhi na jioni?

Huko madrassa ndio mnafunzwa haya au ni makanisani? [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Aisee jamaniii nimecheka hapo tumefunikwa ujingaa
 
Hiyo biblia inavyosema watu wameanzia Iraq ni uongo tu...hamna la kweli hapo!
kwanini iwe uongo wakati hata hao wa mwanzo kama babake abraham,wanaonekana mwanzo iraq?,hata mji wa babeli si uko iraq,ule mtumbwi nuhu alitumia kukimbia mafuriko ya mto frat ulioko iraq nao ulipelekwa na maji mpaka juu ya vilele vya mlima mmoja kule uturuki,jamii nzima kwa mjibu wa bible inaonekana kuanzia iraq,hata lugha aliyoongea abraham na hata yesu asili yake ni iraq pia
 
mbaya zaidi mungu wake alimwahidi kuwa atakaemuua KAINI ,atapewa adhabu mara saba,


lameki babake na Noah,ndiye aliemuua kaini,na adhabu mpaka leo hajapewa

Huyo baba Noah atakomaje...??
na kwa vile una uhakika kuwa hajapewa adhabu basi naomba siku akipewa tu unijulishe mwenzio
........ mbona atakiona... au hakusoma maandiko?
Au ndo shetani kaamua kumkosanisha na Mungu?
 
Mbona akili imekuganda ivo mkuu sasa hao kina kaini na habili una hata undugu nao wala si wafrika wenzio leo unalalama watu wanawafata wazungu na kuwaamini mbona ww unafata imani zao? au unadhani chimbuko la hao finction characters ni afrika?

Umeacha vingapi vya asili yako? Ningekuona wa maana kama ungeleza mila za kwenu huko, Wazungu sio kwamba wanasikilizwa ivo science ni Majaribio na ushahidi na pia science ni dynamic sio static kama dini na sio porojo na imigination kama dini hizo mnazozipigia debe
 
Mkuu chimbuko la mwanadamu sio mwarabu bali ni mwafrika kama utakuwa umechunguza mwafrika ndio bold na binadamu imara sio kingozi,mwili mpaka akili wengine ni kama wametokea ktk jamii ya kiafrika ,Mabadiliko ya rangi ni mazingira ya eneo alipo kama atapaishi kwa muda mrefu sana changes lazma zitokee kwa vizazi vyake yani evolution sasa je kwanini sasa hawatokei watu wa race zingine?

Ndugu Evolution process ni too slow yani inaweza take up ata miaka 1000 mpaka buku mbili ili kunotice changes mwanadamu anaishi let say karne hawezi notes evolution ambayo ina take up thousand yrs kutokea.

Zamani sana watu walikuwa giant na minywele mingi leo watu ni dwarf hiii ni mfano na watu kuwa na maumbile madogo imeletwa na technology binadamy hashughulishe kivile mwili wake mbadala wake ka design machines zinazo msaidia
 
yn hii ni hadithi mpya kabisa kuwahi kuickia tangu nilipoliona jua, kweli hizi ni safari saba za Sindibadi Baharia

Kuishi kwingi ni kuona na kuskia mengi. Ukiendelea kuishi utaweza kuskia na kuona mengi tu mazuri mazuri.

Hiyo ndio raha ya kuishi coz maiti hapati hivi vitu.
 
Mkuu naomba tuelimishane.

Mwanzo 4:25 inasema Adamu akamjua mkewe tena na kujaliwa maana, na kabla ya hapo tunaona Kaini alishaenda nchi nyingine iliyopo mbele ya hedeni na kumjua mkewe na kuanzisha kizazi chake.
 
Mimi nilidhani hii sadaka, ni kwa ajili ya kuwapa binadamu wengine wenye shida wakati huo, kama hiyo nyama alikua anampa Mungu ale huu ni uongo kweupe.
 
Haha mtoa post anakimbia hili swali naona hata hapo juu kuna mkuu ameuliza amelipotezea
Mtopa mada Tafadhali tunaomba majibu ya hilo swali !!!!
 
Wataalamu wa historia(Archaeologist mbona hawasemi kabisa dunia iliumbwa mwaka gani na mabaki ya watu na wanyama wa kale (fossils)ya Adam na Hawa, Kaini na Habili pamoja na mifugo yao inapatikana wapi na hayo mabaki yana umri gani.

Na wakati Mungu anaumba dunia yeye mwenyewe Mungu alikuwa yupo kwenye kitu gani na materials ya kuumbia dunia alikuwa anatoa wapi.Ni dhahiri kuwa taarifa za maandiko matakatifu yanatoka kwenye biblia na quran kwa njia ya simulizi (oral traditions).

Moja ya disadvantage ya oral traditions ni kupotoshwa kwa taarifa. Kwa hiyo utata wa maandiko matakatifu ya biblia na quran umegubikwa na giza la wanahistoria kutofanyia uchunguzi mabaki ya Adam na Hawa pamoja na watoto wao Kaini na Habili na mifugo yao.

Kutokana na sababu hizo inakuwa vigumu kuthibitisha uwepo wa watu hawa na mabadiliko yao (evulution )
 
Mkuu hebu elezea vizuri haka ka story kana utamu flani hivi
 
Sura 11za kitabu cha mwanzo sio matukio ya kihistoria Bali simulizi la kikuhani lenye lengo la kueleza asili ya binadam na dhambi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…