Binadamu wote ni huru ni sawa ukikutana na ubaguzi usikae kimya, tumia njia hizi kuripoti ubaguzi huo

Binadamu wote ni huru ni sawa ukikutana na ubaguzi usikae kimya, tumia njia hizi kuripoti ubaguzi huo

Joined
Sep 17, 2024
Posts
21
Reaction score
16
Ibara ya 12(1 )ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Binadamu wote huzaliwa huru, na wote ni sawa, pinga ubaguzi.

Ubaguzi kwa msingi wa haki za binadamu ni tendo la kutendea mtu au kundi la watu kwa njia isiyo ya haki kwa misingi ya tofauti zao, kama vile rangi, jinsia, dini, kabila, hali ya kijamii, au mtazamo wa kisiasa.

Ubaguzi unaweza kuwa wa wazi (dhahiri) au wa kificho (usioonekana moja kwa moja) na unaweza kujitokeza katika maeneo mbalimbali kama vile sehemu za ajira, elimu, afya, na haki za kiraia.

Je, unaweza kuripoti wapi ukiwa umebaguliwa?

Mtu anayebaguliwa anaweza kuripoti katika sehemu zifuatazo, kulingana na aina ya ubaguzi anaokumbana nao:

1. Polisi
Kama ubaguzi unahusisha vitendo vya uhalifu, vitisho, au vurugu, unapaswa kuripoti polisi mara moja.

2. Kupitia sisi Tume ya Haki za Binadamu na utawala Bora

3. Mashirika ya Kijamii na Kisheria
Kuna mashirika yanayotoa msaada wa kisheria kwa waathiriwa wa ubaguzi, kama vile Legal Aid na NGOs zinazopambana na ubaguzi.

4. Vyombo vya Usimamizi wa Kazi
Ikiwa ubaguzi unatokea kazini, unaweza kuripoti kwa mamlaka za kazi, kama vile wizara ya kazi au vyama vya wafanyakazi.

5. Vyombo vya Haki za Kijinsia na Makundi Maalum
Ikiwa ni ubaguzi wa kijinsia, unapaswa kuwasiliana na mashirika yanayotetea haki za wanawake na makundi maalum.
 
Ibara ya 12(1 )ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Binadamu wote huzaliwa huru, na wote ni sawa, pinga ubaguzi.
Binadamu wote huzaliwa huru kwa muktadha gani?

Watu wanaozaliwa bila kuchagua wazaliwe au wasizaliwe utasema vipi huzaliwa huru wakati wamejikuta tu wamezaliwa bila kupanga wala kukubali kuzaliwa?
 
Back
Top Bottom