Binafsi nimeguswa na funga ya wakristo kipindi hiki cha kwaresma,Funga yenu haina kelele Wala majisifu

Hata China Watanzania wanauza Supu ya Makongoro na Ushanga mitaani. Wamasai wanausa dawa (sokonoi+) Misri na zambia.
 
Mbona mkialikwa futari huwa mnawahi kuliko waislam waliofunga?
Umaarufu wa uislam umefanya hata wakristo wenyewe mnasema huu ni mwezi wa Ramdhan yani hata nyie hamjui kama kuna kwaresma yenu inaendelea

Alafu mkristo tangu lini akafunga? Nilikua na rafiki yangu mkristo alikuja nyumbani kutusalimia akapewa sambusa za nyama akafumua sambusa akatoa nyama za ndani akala maganda ya nje kumuuliza akasema kafunga kula nyama ya ng'ombe ila misomi mingine anagonga sasa kuna funga hapo?

Mkristo hana uwezo wa kuvumilia njaa hata dakika 3 funga atawezea wapi
 
Hizi picha umeziangalia vizuri?!
Hawa watawa wa kanisa katoliki pia unaweza kuwaita wapumbavu?!
Na huyu askofu mkubwa na bilionea goe dev pia waweza kusema halijui neno lililomo kwenye biblia?
 

Attachments

  • 03... (1).jpeg
    1 MB · Views: 1
Kristo anataka ukifunga ufanye kwa siri
Mbona yeye kristo alipofunga hakufanya kwa siri hadi leo 2025 Mimi muislamu niliyezaliwa ndani ya uislamu na wazazi waislamu ninajua kuwa Yesu alifunga siku 40 usiku na mchana?!
Ingekuwa kufunga kunafanywa kwa sisi tungejuaje kuwa yeye kristo alifunga?!
 
Sasa hawa wanaokula wakati wa mchana,wakati huu ni mwezi wa mfungo kwa hizi dini mbili kubwa ni dini gani?
 
Na ukimuona sista wa kikatoliki yuko mahala ujue baba paroko na yeye yuko hapohapo tena saa nyingine kapiga kanzu ya kiislamu na baraghashia safi!
Hao masista wasingeondoka kwenye makazi yao ya utawa na kwenda kushiriki futari na waislamu bila kibali na ruhusa ya baba paroko au askofu wa jimbo husika!.
 

Attachments

  • images(28) (1).jpg
    64.4 KB · Views: 1
  • images(26) (2).jpg
    41.3 KB · Views: 1
Mtumishi wa Mungu Samson Ernest kuna huyu umat wa allah anauliza kama mnaweza vumilia njaa hata dakika 3? Najua FPCT hapo Singida Mjini mna mifungo mingi. Kuna ule wa kitaifa wa siku 21 kama ambao sisi TAG tunao wa kitaifa kwa siku 21 kila mwanzo wa Mwaka. Pia kuna mifungo ya kawaida ya kutaniko la mahali pamoja.

Ndugu yangu Lucha binafsi sasa nipo CBC hapa miuji Dodoma na nina funga kila wiki siku 3 kavu kuanzia Ijumaa hadi Jumapili jioni. Hata nikiwa natumia TAG kule GEITA huwa nafunga kavu 3 days lakini pia kuna mifungo ya masaa 12 na masaa 24.

Kufunga kwa mkristu ni kitu cha kawaida pale anapoamua kumnyenyekea na kumtafuta Mungu wake na mara nyingi hatujitangazi kama tumefunga. Kuanzia nikiwa kazini nilikuwa nafunga na kama wenzangu wanakula kazini mi nawaacha na kujitenga wakimaliza kula tunaendelea na kazi otherwise umeandika hii comment kwa mzaha tu mkuu.
 
Sasa hawa wanaokula wakati wa mchana,wakati huu ni mwezi wa mfungo kwa hizi dini mbili kubwa ni dini gani?
Tukuweke sawa. Hakuna dini mbili kubwa zilizofunga kwa sasa. Waislamu ni kweli wapo kwemye mfungo ila wakristo sio wote wapo kwenye mfungo wa kwaresma. Nijuavyo kwaresma wanafunga Wakatoliki nafikiri pia na waanglicana na baadhi ya Walutheri kama sijakosea.

Mi nasali TAG, Sisi tuna mfungo wetu tofauti na huo Kwaresima. Tunamfungo wa siku 21 kila mwanzo wa mwaka pia kuna muda inaitishwa mifungo ya katikati kulingana na kanisa la mahali pamoja so sio wakristo wote wanafunga Kwaresma mkuu. Sidhani kama makanisa ya Kipentekoste hata Walutheri au wasabato wanafunga hiyo kwaresma. Kwaresma wanafunga Wakatoliki tu mkuu wangu.
 
Itikadi za imani hizi mbili ni tofauti mkuu, tofauti sana. Wenzetu wakifunga ni kwa ajili yao, jamii yao(huenda na wasio jamii yao), na baadae mioyo yao na Mungu wao

Wakristo wakifunga ni kwa ajili ya mioyo yao na Mungu wao..full stop.
 
Imeandikwa ili tupate kujifunza tu mkuu. Sidhani kama Yesu alifunga hiyo mara moja tu. Hata Mussa alifunga si chini ya mara moja tena siku 40 kavu. Mitume wakifunga ila hawakusema wamefunga mara ngapi ila kuna sehemu wanasema walifunga zaidi japo hawajataja muda walioutumia kufanga.
 
Duuh! 😁😁Hii kiboko
 
Uongo huooooooo
 
Funga ya mtu haipaswi kukera wengine.
Ile mijamaa miroho sana
Tungekuwa waroho tusingewaalika wakristo wake tufuturu pamoja nao!
Nyinyi mnapoleta hoja za kipumbavu, na sisi tunajibu upumbavu.
 

Attachments

  • images(28) (1).jpg
    64.4 KB · Views: 1
  • images(26) (2).jpg
    41.3 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-03-27 at 22.19.32 (1).jpeg
    155.3 KB · Views: 1
Kila MTU ashinde mechi zakeeeee babu.

As long as hawavunji Sheria, basi kila MTU awe huru afanye vile vinavyo mpa Amani ya moyo na akili....


Sema nini kwenye dini watu wa middle east walizo zileta walituweza saaana waafrica
Dini za middle East zimejikita kwenye chuki zaidi
 
Tungekuwa waroho tusingewaalika wakristo wake tufuturu pamoja nao!
Nyinyi mnapoleta hoja za kipumbavu, na sisi tunajibu upumbavu.
Kwani kufuturu ni nini mkuu? Huoni hiyo ni kwa ajili ya kudumisha mahusiano mema japo haifuti ukweli mu waroho na waoga wa njaa na pia sio.kama mnafunga bali mnabadilisha muda wa kula. Baada ya kula mchana, mnakula usiku kucha mkuu huku mchana mnatunukisha midomo. 🤣🤣🤣

Usimind jamaa yangu. Nakutania tu kaka. Nyie mnafunga bwana.
 
Mwenye kuleta hoja kasema wakristo! Na kwa mantiki ya andiko lake amemaanisha kwamba wakristo wote wako kwenye mfungo japo hawapendi show off (hii ni kwa mantiki ya mada aliyo mezani).
Mleta mada kaleta mada kuwapongeza wakristo na kuwabeza waislam(kimaniki ya andiko japo hajawataja moja kwa moja).
Nijuavyo mimi ukristo ni dini kubwa,sasa unavosema hakuna dini kubwa umemaanisha nini?
Je,unapingana na mleta mada kuwa hao anaowasifia sio wakristo?
 
Na ndio kwa kujifunza hukohuko kwakuwa funga za mitume hazikuwa siri, walifunga na watu wakajua kuwa wamefunga , haikuwa siri!
Aliyesema kwamba funga za watu wengine ziwe SIRI ni nani?!
 
Uwe unaelewa. Unampotezea mida jamaa kwa ligi zisizo na msingi mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…