Binamu (fa) ulifikiria nini kumshirikisha Bongo Bahati Mbaya - Big up sana

chipa GM

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2012
Posts
1,815
Reaction score
2,973
Hivi kati ya Yound Dar es Salaam na Fid Q nani Bongo bahati mbaya?

Mwana fa safi sana kwa ngoma yako..ila bongo bahati mbaya kaua..huyu jamaa sema tu kwakuwa Tanzania tuna ombwe la redio presenters na entertainment industry ndiyo maana hapati kiki ile kubwa ya mziki. Bongo bahati mbaya (Fid Q)ni msanii mkubwa sana sijaona hata wa kumfikia nusu ya uwezo wake kwa hip hop Afrika Mashariki. Fid Q anajua kuandika, anaswaga kwenye mashairi, anabadilika..safi sana. huu ndiyo mziki mzuri.. unaifanyia vizuri hip hop, tatizo wanaiyoishika industry ya mziki wanapenda waimbaji.

Kilimchonifanya kukua siyo raha ya ndoa..
bonge la hip hop kwa mwaka huu. mi ndiyo najua mpaka naboa. Fid Q kuzaliwa Bongo ambapo kiapji chako hakithamini ni bahati mbaya sana kwako bro. We ungekuwa hata marekeni ungekuwa km wakina Jiga, Nas, Kanye..Fid Q nakwambia hata Wiz khalifa hakuwezi wewe. Umekuwa na bahati mbaya sana kuzaliwa TZ. Unakipaji sana.

Tatzo Nchi yetu akili ndogo, media nyingi zinapiga sana nyimbo za kawaida. Upo hapo? eti mkeka haujachanika leo..we mzee wa bucha balaa sana. Fid Q tafuta management ubrand mziki wako..wewe mziki wako mkubwa sana, unahitaji kuubust kidogo tu. Tanzania tumepewa Bahati ya kuwa na Fid Q, Tafadhali tumsapoti..Asije kuondoka km Ngwair tunabaki tunahunika tu. Ni mwendo wa kunukia vizuri tu km duka la pafyumu..mtoto wa Tanga, kijana wa kwanjeka.. vaa gloves shauri yako.

Fid, na joh tengenezeni basi hata kaupinzani na ka fake bifu maana mziki wetu unahitaji showbiz kidogo..Fa & Mo technical tengenezeni kabifu basi..maana hamna. We siunaona mshikaji wake na mwana fa (kariakoo boy) anapopata mteremko kwa kushindanishwa na namba 1 artist in Tz( the Platinum): Mwana FA tafadhali vaa tai aisee. FA, A.Y mna connection kubwa duniani plz wekeni ngoma basi..FA tunataka ngoma artist nje ya NCHI.

RIP G.Mabovu, Langa & Kaubama

Zawadi yako hii Fid Q..JISIKILIZE..Hii nyimbo bora ya hip hop Tanzania maisha yangu yote ..sijawahi kuichoka na sitokuja kuichoka.

Marehemu Gees Mabovu ft ngosha,mjukuu wa mchopanga na ilalaaaa

Mabovu kwa nyimbo ulipaswa Tajiri.Rip




Mungu mpe maisha marefu mimi na Fid Q.

Lamar classmate kwa biti hata ukistaafu mziki SIKUDAI tena. ulitisha.
 
Hii thread umeandikia bar nini mkuu mbona uandishi wako kama ushavesha tayari
 
Mkuu umeandika kwa hisia sana na unaonekana unaielewa sana Hip Hop. Big up
 
Binge la ngoma
 
Mkuu sijui umewaza nn leo.
Hivyo vichwa ni noma
 
Sidhani kama itakuja tokea tuuthamini mchango wa mtu akiwa bado yuko hai mtanzania.


Tumezoea kumsifu mtu akiwa marehemu,


Namkumbuka mzee ngurumo tukiwa morogoro aliwahi ongea haya.

Kuna watu wengi sanaa Tanzania ambao wanapaswa mchango wao uthaminiw.
Muone Fid Q
Mwana FA
AY
Alikiba
Diamond
Tundu Lisu
ZZK
Magufuli


Ngoja wafe sasa
 
Bonge la ngoma..bonge la dude hatari sana
 
Mkuu ongeza na Makonda kwenye list yako
 
Fid Q anafanya muziki uliotofauti na wana hip hop wote wa kibongo....Fid Q ndio msanii pekee wa Mainstream Hip Hop anaekubalika na wale wanaofanya Underground Hip Hop siku zote kunakuwaga na beef la asili kati yao.

Hawa jamaa hata kule Marekani wakina Rakeem hawawakubali kina Jay Z wanaona kama wanabebwa ila hapa bongo wakina Nikki Mbishi wote wanamkubali Fid Q hii ni heshima kubwa sana kwake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…