Bingwa wa Kusahau!!

Kyachakiche

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2009
Posts
986
Reaction score
208
Jamaa mmoja anayesemekana ndiye mtu msahalifu pengine kuliko yeyote hapa duniani kwa sasa, ametao mpya pale alipoamua kulaza koti kitandani na yeye kujitundika kwenye henga. Ilikuwa hivi:
Alikuwa ametoka katika matembezi yake ya kawaida huku akiwa ametinga suti yake aina ya kahawia. Haikuweza kufahamika mara moja alikotokea ila alipofika nyumbani kwake, alifungua mlango na moja kwa moja kwenda hadi chumabani kwake. Akavua viatu akaweka chini ya kitanda, kisha akavua koti akaliliza kitandani, baadaye akaenda mahali alikozoea kutundika koti lake na kujitundika mwenyewe kwa kutumia mkanda wake wa suruali.
Ghafla jirani yake mmoja aliyekuwa na mihadi ya kukutana naye jioni alitokea na kuanza kugonga mlango. Jamaa kusikia kuna mtu anagonga akajirusha kwa nguvu akifikiri yuko kitandani ili akamfungulie mgonga mlango! Mara akakumbuka kwa muda kuwa kilichokuwa kitandani ni koti lake na si yeye na kwamba tayari ilishakuwa asubuhi na si jioni tena! Usiku mzima alilala kwenye henga na koti kulala kitandani!!! Bingwa wa kusahau huyo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…