Bint yangu anaugonjwa wa ajabu

Ana sexual hysteria ambayo huwapata sana mabinti hasa wa umri huo na haijafahamika hasa sababu halisi ya tatizo hilo ni nini japo watalamu wengi wa afya hulihusisha na mabadiliko ya ukuaji wa binti wa kike. Unaweza ukampeleka kwa counselor lakini pia unaweza ukamkeep busy sana kwa kumpa kazi nyingi za kutumia nguvu zitakazomuweka busy na kumchosha, japo kwenye mashule mengi ya wasichana wanapoliona tatizo hilo huwapeleka watoto kucheza disco na wanafunzi wa shule jirani ya wavulana japo siyo njia nzuri sana. Usijali ni tatizo la muda tu, mpatie tu manual works na counseling itamsaidia.
 
Usikate tamaa endelea kutafuta daktari mwenye uelewa na huo ugonjwa.Mimi nadhani huo utakuwa ni UGONJWA UNAOHUSIANA NA UFAHAMU PAMOJA NA UBONGO ukichangiwa na mazingira.Endelea kutafuta daktari anaejua matatizo ya mtoto wako,nina imani atapona kama akipatiwa matibabu sahihi wa huo ugonjwa unaomsumbua.
 
Toa sadaka hakuna kitu kizuri kama kutowa sadaka.

Yani wewe nunua mbuzi utuchinjie tuje kupiga mlo hapo kwenu, afu tukuombee dua.

Usiogope huta filisika pesa ndo zitazidi :biggrin:
 

Pole sana Mimi nakushauri kwamba mpeleke kanisani akaombewe, kuna makanisa yaliyotapakaa karibu kila kona ya jiji nenda na uonane na mchungaji kiongozi ni bure hautatoa kitu chochote.. Baada ya mambo yote kushibdikana hapa duniani wakumkimbilia ni MUNGU TU
 
Aisee pole sana..Ingawa ana umri wa miaka 16 ..binafsi inge-rule-out assumption za sexual hysteria..Nashauri ..Mpe muda apumzike..vizuri kama mngesafiri haraka sana.. anywhere... badili mazingira..

Kwa sababu wewe ni binadamu kama mimi.. Basi amini Mungu yupo na fuata imani yako kumwomba Mungu akusaidie yapite. Usihofu ni vitu kawaida.. Niliona vitu kama hivyo vilimtokea mtoto wa dada yangu..ila yeye ni binti wa miaka 10..Alipona..
 
Aisee kuna watu wanapata majaribu ya kidunia humu sijapata ona
Ngoja wikiend niende bagamoyo kumwangalia mwanangu maana mnenitisha

Hivi we ndugu yako ni jaki bawa nini?
 
Kuna mawili hapo kama wasemavyo wengi yawezekana ni pepo au kuna tatizo lingine katika mfumo wa damu hili tatizo huwa linawapata watu wengi sana siku hizi hasa wakike na kama halitachukuliwa kwa umakini basi mtu anaweza kupata ukichaa.Mara nyingi huwa damu haifiki kichwani(blood circulation in the brain),huu sio ugonjwa tafadhali ndio mana hata hospitali huwezi kugundulika.kwa maelezo zaidi:0657117377
 
Jaribu kuenda pale department ya psychiatric muhimbili utasaidiwa sana na tatizo litaisha! Um sure of it na uwahi hilo mapema kabla hilo tatizo halijaanza kuathiri ubongo wake .take it serius
Na huo sio uchawi ndugu
 
hiyo hali kitaalam inaitwa hysteria nakushauri umuone daktari wa magonjwa ya akili.
 
Pole bro
jaribu kumpeleka kwa watu wa saikolojia na utafiti wanajua jins ya kuwatambua watu kama hawa kama ni kujifanya au ni tatizo
ikishindikana mpeleke kwenye maombi na endelea kubak na msimamo wako wa kutoamin iman za kishirikina
 
pole mkuu...ilishawahi kutokea shule niliyosoma..ilikua wasichana watupu...wakaanza wasichana watatu then bweni zima then karibia shule nzima...tukaandaliwa party ambapo waalikwa walikua ni wanafunzi kutoka shule za wavulana tu...baada ya hiyo party wagnjwa wote wakapona...
ila tiba sio kusex na hao wavulana..ile tu kumingle na jinsia nyingine inasaidia kisaikolojia..
 


Ana mfadhaiko au pia inawezekana ni pepo.

Siku hizi Tanzania uchawi ndiyo dini, kijicho, visasi, na wivu vinatawala. Mpeleke afanyiwe maombi na mtafute

psychiatrist amfanyie evaluation. Au kama mwana JF mmoja alivyosema, change of scenery will help. kama una mahaela

mpeleke akatalii.
 
Blood circulation in the blood ndo ugonjwa gani huo ndugu..unaelewa maana y ulichokiandika unajua unamaanisha nn dah utakuwa tiba asilia ww maana nyie kujifanya mnaelezea magonjwa kwa kutumia kiingereza wakati lugha nyingi za kitabibu zinazo taja magonjwa ni za kigiriki na kilatini. hospital gani isiweza kuona cirulation ya blood katka brain na unamaanisha nn haswa au ndo unataka kuelezea kuhusu syncopes au convulsion na hujui nn hapo pole sana.
Kwa mujibu ya short history ya huyu msichana it posible ni hysteria au conversion disorders na hakuna cha maombi wala nn zaidi ya konana na psychologist fika muhimbili kuna wataalamu kuenda huko sio kwamba mungu hayupo wala nn
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…