Binti akisema amekufananisha na kaka yake!


Huyu sikumuuliza kanifananisha nini maana sikumuuliza maybe angenambia hajui pia.

Yeye kakumbuka kuwa keshawahi kuniona kwa sababu Mara ya kwanza aliponiona alinifananisha ATI

Unaweza mtu ukamjua miezi na usijue umemfananisha kiti gani hasa kama hamna mazowea.

Besides inaweza kuwa imemclick time hiyo kuwa kakufananisha
 
Kama ujaoa sasa kama kichwa hicho mzee kimeshaingia chenyewe ! ukikutana nacho kiambie dada yangu yale maneno yako bado nayakumbuka akisema kwanini mwambie hujui kwanini? Siku ipo ataongea ukweli alikuwa anamaanisha nini!
 

mimi nlimpotezea japo alikuwa mzuri ila mi niliona hatuendani. Ngeweza kufanya lolote ila skupenda kumchezea mana sijawa tayari kwa ndoa,na najua yeye alikuwa akisaka ndoa. Kaka mtu anakuja anakaa kwako leo mpaka usiku,kesho mpaka usiku n.k sasa unategemea nini,ukidhubutu si ndo anafuata mizigo yake nyumbani kwao? Kaka kama uko interested we weka mitego yako akianguka umo ujue wako. Kaka ama huna software ya kutegea?! Hawa ndugu ni weak sana huwezi amini! Unataka software?sema kaka usione noma,kwa sekta hii ata mkuu wa nchi mwenyewe huwa anaitegea sikio labda mapadre tu ndo hawausiki apa!
 

Gaijin; nashukuru kwa mtazamo wako Dada yangu. Ila penye red nadhani ndiyo sababu yenyewe ya huyo mtu wako kukufananisha.
Mwenzio niliambiwa tu tena nje kabisa ya mazungumzo yetu ya awali (akakaa kimya ghafla halafu akaonesha sura ya msisitizo nimsikilize), nanukuu:
Binti: TANMO nakufananisha kweli na kaka yangu!
Mimi: Kwa nini umesema hivyo?
Binti: Sijui kwa nini, ila naona kama mnafanana (akacheka).
Mimi: (nikiwa na butwaa) Hehe, haya Bana, basi twenzetu tukaendelee na kazi..

Kama ujaoa sasa kama kichwa hicho mzee kimeshaingia chenyewe ! ukikutana nacho kiambie dada yangu yale maneno yako bado nayakumbuka akisema kwanini mwambie hujui kwanini? Siku ipo ataongea ukweli alikuwa anamaanisha nini!

Kaka ushauri nimeusikia, naahidi kuufanyia kazi...
 

Mamaaaa!!! mbavu zangu..
Mkuu nihitaji software itakayonisaidia ku-crack system ya huyu binti ili nijue hasa alikusudia nini kunipa kauli kama ile.......
 
Wewe kwani mtu akikufananisha ndio anakutaka kimapenzi?tena kakufananisha na kaka yake ina maana muheshimiane kama mtu na dada yake,na je kama angekuwa mwanaume mwenzako kakufananisha na dada yake ungesema anakuta kimapenzi?
 
Wewe kwani mtu akikufananisha ndio anakutaka kimapenzi?tena kakufananisha na kaka yake ina maana muheshimiane kama mtu na dada yake,na je kama angekuwa mwanaume mwenzako kakufananisha na dada yake ungesema anakuta kimapenzi?

Wataalamu wanasema kuwa binaadamu tunakuwa attracted kimapenzi na watu wanaofanana na familia zetu 🙂
 
Wewe kwani mtu akikufananisha ndio anakutaka kimapenzi?tena kakufananisha na kaka yake ina maana muheshimiane kama mtu na dada yake

Inawezekana ndiyo maana nataka kupata mtazamo wa Great thinkers mkuu, manake penye wengi unaweza kupata mawazo tofauti na ya msingi..

na je kama angekuwa mwanaume mwenzako kakufananisha na dada yake ungesema anakuta kimapenzi?

Dah! Si mchezo. Ila sintoshangaa kama akinipa na sababu (labda dada anatabia kama zangu - "let's say ni mkimya" au "Mkorofi" hii ni kwa mfano tu). Ila akiniambia tu na kuishia kusema hajui kwa nini tunafanana basi nitamshangaa. Na cha kufanya au kufikiria nitakipata kulingana na jinsi atakavyo iwasilisha kauli yake.

Pamoja kaka...
 
Wataalamu wanasema kuwa binaadamu tunakuwa attracted kimapenzi na watu wanaofanana na familia zetu 🙂

Gaijin; kweli?
Nipe somo dada yangu nisijekuwa simtendei haki binti wa watu...
 
Gaijin; kweli?
Nipe somo dada yangu nisijekuwa simtendei haki binti wa watu...

Hiyo ni kweli kwa mujibu wa watafiti. Na wanasema inatokea unconsciously.
Watu wana tendency ya kutafuta partners wanaofanana na familia zao au watu waliokuwapo around walipokuwa wadogo

*note: sisemi kuwa huyo kawa attracted na wewe au kila binaadamu akimfananisha binaadamu mwenziwe na familia yake ni kuwa ana sexual feelings.
 
Tukiwa bado kwenye kufananishwa..vipi kama mtu kakufananisha na mtu aliye cheat na mwenzake halafu atake kukupa kibano?

Mimi nishawahi kufananishwa na watu mara nyingi sana. Vitoto vishawahi kunifananisha na baba zao, kuna demu alishawahi kunifananisha na ex wake (nami nikapata upenyo wa kurusha ndoano hapo hapo lol).

Kufananishwa kuna faida na hasara zake bwana.
 
Mimi sipendi kufananishwa hasa na mtu ambaye yupo kwenye position ya kuonana nae mara kwa mara.

Nahisi kama ndo 'nalazimika' kuwa rafiki yake kwa kuwa nimefanana na dada yake japo sikuwa na mpango huo. :s

( hata akiwa mfananishaji ni mwanamke mwenzangu)
 
ina maana wewe ni sawa na kaka yake!huwezi kumu approach.ndiyo maana wanaume wengi hawataki salamu ya shikamoo toka kwa mabinti,maana binti ukimuomba atakuambia ninakufananisha au kukuheshimu kama baba au kaka
 
Amekuona hakuna mwelekeo wowote wa yeye na wewe kuwa wapenzi!!
 
Kwa maoni yangu binafsi, sina tatizo na ufananisho huo, si kufananishwa tu? mi nilidhani ungeishia hapo kuliko kupeleka mawazo mbali zaidi, kwa mfano, angekuja akaku-kiss shavuni, just a simple kissing, je ungesema anakupenda? au akikukumbatia? mpwa, dalili ya mvua ni mawingu, usilazimishe mvua kuja kabla ya mawingu, yaweza kukuletea aibu! simba mwenda pole.....
 

kwa sisi wataalamu wa fasihi tunasema hicho ni kibuti kitakatifu na cha kidiplomasia , wewe ulishaona wapi dada akaolewa na kaka yake? umepewa cheo cha u kaka ili utulie bana. mdada kaona unampigia misere kidizaini. umeongea kwamba haujaonesha dalili ya kumtaka lakini hayo majokes yako pengine yamempa tafsiri nyengine. karibuni nitaanzisha sredi kule jukwaa la lugha kuelezea matumizi ya neno "kaka", nimeona upo umuhimu huo.

-THE END-
 

Nashukuru kwa ufafanuzi dada yangu (hasa kwenye red), basi ngoja nifanye kautafiti halafu nitakuja kukupa feedback..
 

Hapana...ni mapema mno kwa yeye kukonkludi hivyo. Yeye ni avute tu subira kwani kama totoz kweli anampenda jamaa basi ataonesha hints zaidi.

Kuna watu mahusiano yao wakikusimulia jinsi walivyoanza utabaki mdomo wazi. Hii ya kaka-dada ni ishu mdogo kabisa.
 
ina maana wewe ni sawa na kaka yake!huwezi kumu approach.ndiyo maana wanaume wengi hawataki salamu ya shikamoo toka kwa mabinti,maana binti ukimuomba atakuambia ninakufananisha au kukuheshimu kama baba au kaka

Nashukuru kwa ufafanuzi mkuu. Nitaufanyia kazi.....

Amekuona hakuna mwelekeo wowote wa yeye na wewe kuwa wapenzi!!


Naam, nimekupata Bandugu.. Ushauri wako utazingatiwa.....


Bwana Mtaalamu wa Fasihi, naomba ufanye hima kuanzisha hiyo sredi angalau itasaidia kuondoa mkanganyiko...
Ila kama ulivyosema, kutaniana kwetu labda mwenzangu alikuchukulia kama mitego ya kumnasa na ameamua kujihami kabisa....
Nitalishughulikia hili suala ili nipate ufumbuzi though.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…