Binti amenichanganya mpaka nimeshukia njiani

lossoJR

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2012
Posts
2,711
Reaction score
2,384
Wakuu nimeamini mapenzi yana nguvu kiasi kwamba waweza fanya mambo mengine kwa msukumo usiokua na tija. Juzi hapa nimekuwa nikisafiri kutoka mkoani kwenda Dar, but ndani ya bus kulikua na mrembo machachari mno kiasi kwamba nikajipa moyo kama atafanikiwa kushukia ninaposhukia basi siwezi mlazia damu.

Bahati mbaya akawa ameshuka Iringa, nami mtu mzima nikajitosa nika drop kwa vile nilimuelewa sana. Bus likaondoka, ile najiandaa kumsemesha mara ghafla akaja jamaa kajaa jaa hivi, yaonesha ni jamaa yake maana kwa zile hugs nikajua hapa sina changu, then wakatokomea kusikojulikana.

Basi mtu mzima nikaanza kuhaha pesa ya rum na usafiri wakunifikisha safari yangu ukizingatia nilikua nina interview ya kikazi.

Wanawake bwana, sijui mlinyunyuziwa sumaku ya aina gani!
 
Ni ugonjwa wetu sisi wanaume
kama sio mwanaume utamuona mtoa mada ni mtu wa hovyo hovyo lakini mtoa mada ni shuja a kapigana mpaka tone la mwisho
ningekua na hela ningekuchangia nauli
 
Hahahahahahaa polee

Nafasi yako ilikuwa ndani ya basi ucheze karata zote ili binti asishuke Iringa uende nae hadi Dar angekuwa keshamuacha jamaa yake. Hehehehee polee.

Nakumbuka nilipokuwa kigori **** mkaka alishuka kwenye daladala kituo sio chake na alinisindikiza hadi nyumbani hehehe. Kote huko sijamjibu hata kimoja alichokuwa ananiongelesha. Nilipokaribia nyumbani nikamwambia skiza nipe namba ya simu ya kazini kwako na anuani ili mimi nikutafute maana enzi hizo geti kali na sikutaka apajue nyumbani. Nikimuacha anisindikize kutoka kituo cha daladala hadi karibu na nyumbani maana kigiza cha saa kumi na mbili jioni kilikuwa kimetanda hivo nilikuwa na woga wa kutembea mwenyewe.
Hahahaha nilikuwa nashangaa wanaume unaanzaje kumfatilia mschana hata humjui tena alinilipia nauli, simjibu chochote aniongeleshacho mie natembea tuu hahahah

Kwenye daladala sasa akishakulipua nauli utaona konda anauliza sheli. ... kimya.... kwa mpemba.... kimya... jamaa anasubiria binti aseme shusha ili naye ashuke.

Siku ingune nilikutana na jamaa wa hivi na nilimuuza maana nilikuwa natoka kawe naenda posta, baada ya kunilipia nauli nikasema leo atakoma maana ukimuangalia usoni anakutazama kwa macho ya kukutongoza tuu.
Kufika mbuyuni konda kuuliza mbuyuni nikasema shusha, yeye akatangulia kusimama na kushuka mie nikajichelewesha nilisimama kisha nilipoona kushuka nikainama na kurudi kukaa. Konda kuuliza mwingine kimyaa.... akaruhusu gari iondoke heheheheh nilichungulia nje jamaa macho yanamtoka maana mda ule kupata usafiri wa posta maeneo yale ni shida.

Poleni ila nilifanya yale kwakuwa ilikuwa utoto tuu hahahaha kweli wanaume mmeumbiwa mateso.

Wakati nasoma sekondari kuna mvulana flani alishanisindikiza toka tumeshuka kwwnye daladala hadi eneo la tuition wakati huo na yeye anasoma tuition ila kwingine. Siku hiyo alinisubiri hadi mie nimetoka tuition na tunarudi tumepanda daladala moja. Akanilipia nauli, sikutaka apajue nyumbani hivyo niliposhuka mwisho wa kituo nikamwambia nipe address ya shule unayosoma na jina tuandikiane barua si unajua home kuna mbwa wakali? Akanielewa ndo nikamtoa kihivyo daah.

Yaani mleta mada nimekuelewa sanaa. Pole kwa yaliyokusibu sio pekeyako ni wanaume wengi tuu huwakuta haya.
 
Hahaahah you made my bro... Nimecheka sana.. Of coz nami kwa sasa nipo safari na nimekaa na mtoto masharaa .. Mzee mzima nashindwa hata nianzeje .. Lakini sitadhubutu kushukia njiani
Shuka tu mkuu, utalala kwngu hlf nitakukatia ticket ya kumalizia safari
 
Hahaahah you made my bro... Nimecheka sana.. Of coz nami kwa sasa nipo safari na nimekaa na mtoto masharaa .. Mzee mzima nashindwa hata nianzeje .. Lakini sitadhubutu kushukia njiani
usithubutu mkuu,maana niaibu kiukweli,nilikua mtalii bila kupenda.dooh
 
hahaha mkuu sasa umenichekesha nakufanya nisahau mauzauza yote ya juzi, ila huyo mwana wa mbuyuni atakua aliisoma namba..eeh we mutu mubaya
 
Hiyo tamaa ndugu! Si ungeongea nae humo kwenye basi kwanza!
 
hii ninkawaida mimi jumamosi ya tarehe20 mwezi uliopita nilikutana na mrembo haswaa nilipomuona tu nafsi ilipasuka nikaduwaa nikasema huyu simuachi lazima nitete naye kama nitapanda nae gari moja..

kweli nikapanda nae gari moja maana nilisubiri apande yeye alafu mie ndio nifate alipoenda kukàa akakaa siti ya mtu mmoja hapo mzee na mie nikakaa jirani yake wala sikutaka kuchelewa sana visalamu vya hapa na pale mara gari imejaa ata kuongea tena haiwezekani nikasikitika sana nafsini mwangu sikujua atashukia wapi ila nikasema kama sio riziki basi siilazimishi

tukaendelea na safari konda akauliza gereji mie nikajibu fasta shusha nikaona niko peke yangu ile kushuka si namuona yule bbe nae kateremka nikaona leo nimeokota dodo kabla ata ya msimu

hee kumbe bado tupo pamoja pale sasa tunaendelea kutembea tukielekea upande mmoja ki ukweli yule mdada binafsi aliniumiza sana moyo wangu wakati tunaweka weka maongezi vizuri mara akabadilika ghafla na kuanza kuniaga kaka asante nashukuru sana kama mara tatu ivi ila nikajiongeza kwa nini imekuwa haraka hivi alafu akabadilisha na upande wa kutembea
kumbe alikuwa anasubiriwa na jamaa yake na alikuwa katuona tangu tuanapotoka kwenye daladala na mwendo tuliotembea hauzidi ata dakika mbili kumfikia yule jamaa yake kwa kweli kama wewe dada upo humu jukwaani ni pm tu
binti flani ivi wa kishombeshombe yaaani nimeandika hii ujue mpaka leo nakukumbuka sana tuliachana maeneo ya hapo tabata garage njia panda ya kiwanda cha mpishi ..na siku hiyo ilikuwa ni usiku wa saa 22:39 ..tulikutana ubungo mataa wewe unatokea na ubungo maji mimi nimetokea na ubungo terminal
 
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] hapo mbuyuni ulitisha.
 
Hiyo tamaa ndugu! Si ungeongea nae humo kwenye basi kwanza!
mkuu sikukaa nae alikua siti ya ubavuni,sasa kumuongelesha humo soo,si unajua wavimba macho tena....bati nimepata funzo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…