Binti aua watoto wake 2 baada ya kugombana na mama yake mzazi kwa kuchelewa kuandaa chakula

Binti aua watoto wake 2 baada ya kugombana na mama yake mzazi kwa kuchelewa kuandaa chakula

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mshukiwa alirejea nyumbani akiwa amechelewa na hivyo kumlazimu mama yake kumuuliza sababu za kukosa kuandaa chajio

Mama huyo anadaiwa kukerwa baada ya mama yake mzazi kumuagiza kuwaandalia wanawe chajio ambao tayari walikuwa wamelala bila kula. Alikimbia jikoni, kuchukua kisu na kuanza kuwadunga malaika hao wawili wenye miaka saba na miwili

Winfred pia alijaribu kumuua mama yake mzazi lakini alimshinda nguvu na kumtupa nje ya nyumba

Mshukiwa aamekuwa akitishia kuwaua watoto hao kabla ya kisa hicho

Polisi katika Kaunti ya Nairobi wanachunguza kisa ambapo mama mmoja mwenye umri wa miaka 24 aliwadunga kisu na kuwaua wanawe wawili Jumamosi, Mei 2 usiku, katika mtaa wa Kayole.

Mshukiwa aliyetambuliwa kama Winfred Nduku, anadaiwa kukerwa baada ya mama yake kumuagiza kuwaandalia wanawe chajio ambao tayari walikuwa wamelala bila kula.

Kayole

Mshukiwa anapokea matibabu katika Hospitali ya Mama Lucy. Picha: UGC.

Nduku alirejea nyumbani akiwa amechelewa huku akiwa kwenye simu na hivyo kumlazimu mama yake kumuuliza sababu za kukosa kuandaa chajio kama ilivyoripoti CitizenTV.

Ni katika harakati hiyo ndipo alikimbia jikoni, kuchukua kisu na kuanza kuwadunga malaika hao wawili wenye miaka saba na miwili, kisha kujaribu kujitoa uhai na kisu hicho.

Kayole

Picha ya wakazi wakitazama kisa cha awali Kayole. Nduku alikimbia jikoni, kuchukua kisu na kuanza kuwadunga kisu watoto wake Picha:UGC.

Baada ya kutekeleza maovu hayo, Winfred pia alijaribu kumuua mama yake mzazi lakini alimshinda nguvu na kumtupa nje ya nyumba.

Watoto hao walikimbizwa hospitalini lakini tayari walikuwa wamekata roho kutokana na majeraha.

Mama yake mshukiwa aliwaambia maafisa wa polisi kuwa binti yake amekuwa akitishia kuwaua watoto hao kabla ya kisa hicho cha Jumamosi.

Kamanda wa Polisi Kaunti ya Nairobi, Philip Ndolo alisema kwa sasa mshukiwa anapokea matibabu katika Hospitali ya Mama Lucy na atakabiliwa na mashtaka ya uhalifu baada ya kupona.

Chanzo: tuko.co.ke
 
Hiyo sio roho ya kawaida...R.I.P malaika
 
Wakenya bhna, mara mwanamke amkata mumewe dushe, mara mwanamke ampiga mumewe, leo tena huyu kauwa watoto tena wawili dah!!! Lakini kiukweli wanawake wa kenya sio laini laini kama hawa wa kibongo. Akijichanganya mwanaume wa dar pale lazima achezee vitasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakenya bhna, mara mwanamke amkata mumewe dushe, mara mwanamke ampiga mumewe, leo tena huyu kauwa watoto tena wawili dah!!! Lakini kiukweli wanawake wa kenya sio laini laini kama hawa wa kibongo. Akijichanganya mwanaume wa dar pale lazima achezee vitasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha kaeni mbali na wanawake wetu. Hawa ni simba sio paka kama wenu. Lakini RIP kwa watoto
 
Tuache utani pembeni: ivi uyu jamaa watoto wawili. Mmoja miaka saba mwingine 2 At 24 years of age how?
Jamaa alioa akiwa na miaka 15 au 14?

Anyway, rest easy kids.

miss zomboko,
 
Tuache utani pembeni: ivi uyu jamaa watoto wawili. Mmoja miaka saba mwingine 2 At 24 years of age how?
Jamaa alioa akiwa na miaka 15 au 14?

Anyway, rest easy kids.
Huyo mama alizaa akiwa na miaka 17,
Mambo ya kuoana umeyaona wapi hapo?
 
Kenya hiyo!!! Hatari
watoto wapumzike kwa amani.
 
Kituko kidogo kama hiki watu mnajifanya kushangaa!! Washamba nyie
 
Majirani ukahaba nyie mmo, madawa ya kulevya mmo, hadi kuua watoto bila hatia mmo...

Mnasikitisha sana...
 
Back
Top Bottom