Binti darasa la nne adaiwa kujinyonga

Binti darasa la nne adaiwa kujinyonga

Donnie Charlie

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2009
Posts
16,908
Reaction score
19,123
JESHI la Polisi linachunguza kifo cha mwanafunzi wa darasa la nne Shule ya Msingi Kambarage wilayani Kibaha mkoani Pwani, Tatu John ambaye alikutwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya chandarua kwenye chumba cha kulala nyumbani kwao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo alithibitisha kutokea tukio hilo eneo la Mtaa wa Mkoani B.

Kamanda Lutumo aliwaeleza waandishi wa habari jana kuwa tukio hilo lilitokea Februari 19 saa 9 alasiri ambapo familia hiyo ilihojiwa na Jeshi hilo kuhusiana na tukio hilo.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mkoani B, Shabani Kasamya alisema alipokea simu kutoka kwa mjumbe wa mtaa wake akimueleza kuwa kuna mtoto amejinyonga ndani ya nyumba.

Kasamya alisema kuwa kabla hajaenda kwenye nyumba palipotokea msiba, alitoa taarifa polisi ili wafike kwenye eneo la tukio.

“Nilipofika nyumbani niliwakuta wafiwa wapo na mjumbe ndipo walipoingia ndani ulipo mwili wa marehemu na kumkuta akiwa ameingiza kichwa ndani ya kamba ya chandarua ambayo imefungwa dirishani mkono wa kulia na kushoto,” alisema Kasamya.

Alisema tukio hilo lilifanyika kwenye dirisha la chumba ambacho walikuwa wanalala watoto na walimkuta marehemu amepiga magoti na polisi walifika wakapiga picha na kuchukua vipimo kisha wakaondoka na mwili kuupeleka Hospitali ya Tumbi.

Chanzo: Habari Leo
 
Sometimes ni roho ya umauti imepandikizwa Kwa mtoto ili ionekane amejinyonga kumbe nyuma ya pazia watu wapo kwenye mipango ya kupiga hela
 
Media ishasema kajinyonga

Polisi wakajibu kweli tukio imetokea (la kajinyonga)
Serikali haijui cha kusema.

Society inalaumu "wivu wa mapenzi ya utotoni."

Incompetent media, untrained police, derelict government, illiterate society.
 
Media ishasema kajinyonga

Polisi wakajibu kweli tukio hilo limetoke (yani kajinyonga)

Society inalaumu "wivu wa mapenzi."

Serikali haijui cha kusema.


Incompetent media, untrained police, derelict government, illiterate society.
Wamesema adaiwa kujinyonga kwa hiyo bado kuna room ya uchunguzi.
 
Wamesema adaiwa kujinyonga kwa hiyo bado kuna room ya uchunguzi.
Soma kwa makini

Sentensi ya kwanza mwandishi kasema mtoto amekutwa amejinyonga. Sentensi ya pili Polisi wamethibitisha tukio hilo.

Hiyo inadaiwa iimechomekwa kwenye kIchwa cha habari cha JF ambacho hakiendani na habari yenyewe.

Kama " inadaiwa" ilibidi mwandishi aseme inadaiwa na nani.

Illiterate society. Incompetent media.
 
Back
Top Bottom