BINTI: Filamu ya kwanza ya Kitanzania inayooneshwa Netflix

BINTI: Filamu ya kwanza ya Kitanzania inayooneshwa Netflix

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
Filamu ya BINTI @bintimovie ni filamu ya kwanza ya Kitanzania kuoneshwa katika mtandao wa filamu mitandaoni kwa jina la NETFLIX.

Filamu hiyo inaelimisha mabinti kutotamani maisha ya wenzao ikiwa hawajui wanapitia nini.

Imeandikwa na mtunzi Angela Luhinda pamoja na @sekoshamte na tayari imejinyakulia tuzo katika Zanzibar International Film Festival 2021.

Ni filamu inayohusu Maisha ya Binti Wa Kiafrika, Kitanzania ikiwa na ujumbe wa kuelimisha mabinti kutotamani maisha ya wenzao ikiwa hawajui ni nini wanapitia.

Imeoneshwa katika majukwaa makubwa ya filamu Kenya, Marekani, Ujerumani miongoni mwa nchi zingine.
 
lol [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Yaleyale ya akina shumileta anatoa moyo wa mtu anaula kumbe andazi.

[emoji1787]
Mdada anabakwa hapigi hata kelele ndo kwanza anakaa ile staili ya baby panda dirishani fanya kama unaidondokea..[emoji1787]
 
[emoji3][emoji3]
 
Hiv mwigizaji/mtunzi atapataje hela kwa filamu yake kuoneshwa Netflix?
 
Hiv mwigizaji/mtunzi atapataje hela kwa filamu yake kuoneshwa Netflix?
What I think inakuwa hivi it's either wanalipwa na Netflix ama kwa faida itakayoingia au mkataba wa moja kwa moja yani wana ku cash out msijuane kazi inakuwa yao kila ulichokifanya ndo kimekuwa chao we yako hela.
 
Nilipoiona Netflix nikasema niangalie kdg nione kama nzuri. Ilinichukua nkaimalizia mpk mwisho. Ni nzuri
 
Back
Top Bottom