Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
BINTI, KAMA UNAMPANGO WA KUOLEWA USICHELEWE KUOLEWA. UMRI SAHIHI MIAKA 20 - 30.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Kuolewa ni faradhi lakini kuzaa inaweza kuwa majaliwa yaani mapenzi ya MUNGU.
Ikiwa unajua kuna siku utataka Kuolewa au utaolewa Basi ninakushauri usichelewe kufanya hivyo.
Umri sahihi wa mwanamke Kuolewa ni Kipindi akiwa msichana anayevutia, ngozi laini hata ukipaka Mafuta ya kula, sura nzuri na uso wenye Nuru hata usipotabasamu.
Ukiwa mbichi ndio umri sahihi wa Kupata Mumeo afurahie mwili wako, afurahie usichana wako.
Hakuna kitu ambacho Mumeo utampa zaidi ya fahari ya usichana wako. Wanaume hujivunia Sana kuoa mwanamke mdogo, mzuri aliyekatika kilele chake cha uzuri( prime age).
Kuna Raha jamani! Kurudi nyumbani kukaona kamke kako kakiwa kabichi, kateketeke.
Usikubali Kuolewa ukiwa mtu mzima bila sababu za msingi.
Kama unajua utaolewa ni muhimu kufanya hivyo mapema. Na umri sahihi ni Kati ya Miaka 20-30 hapo. Tena ukiweza miaka 20-25 kama utakuwa na mipango Mikubwa kama ya shule basi usizidi Miaka 30.
Binti yangu, ni ngumu Sana Kupata mwanaume wa maana kadiri unavyochelewa Kuolewa.
Utaishia kuharibu ndoa za watu. Utaishia kutoka na waume za watu.
Utaishia Kuwa nyumba ndogo.
Sisi Watibeli ni mwiko kuoa wanawake waliokomaa. Wanawake waliozeeka. Ni mwiko kwetu.
Wanasema uzuri wa mwanamke wako ni ule ubichi wake.
Ndio maana Biblia yenyewe inakuambia usimsahau mke wa Ujana wako. Kwa sababu huyo ndiye ulikula fahari yake.
Mwanamke anaweza kuwa mzuri Sana. Lakini kigezo cha umri kikashusha thamani ya ule uzuri wake.
Umemaliza chuo unamiaka 25 ukapata mwanamke mwenye Miaka 40 ambaye ni mzuri lakini utakapompeleka kwa wazazi au wazee wenye akili zilizotimia watakuzuia kumwoa huyo mwanamke licha ya uzuri wake. Zaidi watakuambia sio mzuri wa kuwa Mkeo. Wanasababu kubwa na zamsingi zenye Akili.
Mkeo ni kama Binti yako wa Kwanza. Hutakiwa kumchagua akiwa amekomaa. Kwako haitakuwa fahari.
Kumbuka Moja ya mambo yanayompa Mwanaume utukufu mbali na pesa na Mali zake, pia Mwanamke Mzuri ni sehemu ya fahari na utukufu wa mwanaume.
Na katika uzuri wa mwanamke suala la umri lipo constant.
Usichezee usichana wako na wanaume wengine huko alafu ukose cha kumpa Mumeo fahari, heshima na utukufu.
Mumeo atadhalika Sana.
Mumeo watu watamsikitikia Sana.
Maskini ganda la Muwa la jana chungu kaona kivuno.
Siku ya SHEREHE yenu ya harusi Mumeo automatically hawezi kuwa na furaha. Pindi vyuma vibichi vitakapokuwa vikipita mbele vikiwa vimependeza, watoto wabichi Kabisa.
Ndugu za Mumeo hawatakuheshimu, zaidi watasema umemloga mtoto wao kwani wewe ni Mzee.
Hutojali lakini kikawaida athati zitaonekana tuu.
Binti, wewe ni mwanamke daima. Sio jukumu lako la msingi kuwa na ndoto kubwa kuliko wanaume. Ati utafute pesa Kwanza sijui utimize malengo ndipo uolewe.
Wewe kama Mpaka Miaka 24/5 kama malengo hayajatimia, sitisha kwanza uolewe. Kisha utaendelea ukipata nafasi. Hiyo ndio akili.
Maelezo haya ni Kwa wale wanawake wenye mpango, ndoto za kuja Kuolewa hapo baadaye.
Kama hauna hizo ndoto post hii haikuhusu.
Huwezi ukawa na mpango WA Kuolewa alafu ati unajichelewesha Mpaka Miaka 30+ huko ni kujitafutia matatizo makubwa. Na Hakika yatakupata tuu.
Miaka 20-30 wanaume wanakuja wengi kukufuata, Fanya usaili kwa umakini, chagua best candidate kulingana na upendavyo, na huyo candidate Moja ya vituo vitakavyomfanya awe best candidate kimojawapo ni kukupenda na kukutaka.
Sio umchague kwa matakwa yako tuu Bali angalia naye anakutaka, anakupenda, je anavigezo vingine muhimu unavyovipenda. Simple.
Kisha Olewa!
Kadiri unavyochelewa ndivyo unavyojiwekea nafasi ya Kupata wrong choice. Ndivyo unavyojiwekea mazingira ya kuchanganyikiwa.
Kama wakiwa wengi anachanganyikiwa kuchagua Basi elewa wanavyozidi kupungua kuacha kukufuata ndivyo wenye sifa unazotaka watakavyopungua.
Usijesema Babaako sikukuambia!
Acha nipumzike sasa
Nawatakia Sabato Njema
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam