Mwana_si_Hasa
New Member
- Jul 25, 2022
- 3
- 5
“Kama utaendelea kuishi, acha urithi, weka alama duniani ambayo haitafutika”
-Maya Angelou.
Ellen Johnson Sirleaf, Maya Angelou, Mellody Hobson pamoja na Mo Abudu ni kati ya majina maarufu sana ambayo kama ukijaribu kuuliza watu kumi unaowafahamu basi nane au tisa kati yao watakupa habari za kutosha juu ya watu hawa. Kama walio karibu yako wameshindwa kukujibu waulize na haya.
Samia Suluhu Hassan,Kamala Harris pamoja na Oprah Winfrey.
Naam!
Naamini hata wewe unayafahamu vizuri majina haya inawezekana hata kichwani mwako umeziona picha za sura zao kulingana na ulivyowahi kuwaona.
Ni wazi kwamba majina haya yanaakisi jinsia ya kike.Bila kupepesa maneno wanawake hawa ni maarufu sana duniani, isitoshe jarida maarufu la Forbes disemba mwaka 2021 lilitoa orodha ya wanawake 100 wenye ushawishi mkubwa zaidi duniani, nambari 94, 2 na 23 zilikamatwa na wanamama tajwa katika aya ya pili kama majina yao yalivyopangwa.
Lakini makala hii haina lengo la kuwazunguzia watu hawa isitoshe hata kama ingekuwa na lengo hilo basi makala hii isingetosheleza kueleza kazi wanazofanya wanamama hawa japo tunaweza kuwatumia wanawake hawa kama kioo cha kuakisi mazuri yao kwa jamii lakini haswaa kwa mabinti wa kisasa.
Nukuu mojawapo ya jarida la Forbes ilisema kwamba wanawake hawa walipewa heshima kwa kuandika historia katika sekta zao za kazi, ni kweli katika majina hayo kila mmoja ametangaza jina lake kwa kazi yake na ni kazi yake tu ndio iliyomfanya ajulikane,aheshimike au apendwe.
Ndugu msomaji nisikuchoshe, lakini niruhusu tutete kidogo, nadhani mimi na wewe hatukuwepo zama za wanamama hawa kipindi wanakua au kwa maneno mengine wakati wa malezi na makuzi yao.
Ila tutakubaliana kwamba nyakati za malezi na makuzi ya mabinti wa siku hizi mimi na wewe tupo, ndio, tupo kweli.
Kabla sijaendelea na soga hii embu nikukumbushe jambo, nakurudisha mwanzo kabisa wa makala hii nikiyanukuu maneno ya mwanamama Maya Angelou,
“Kama utaendelea kuishi, acha urithi, weka alama ambayo haitafutika duniani”
Naam!
Weka alama.
Japo sikuwa ndani ya mawazo ya mwanamama Maya Angelou lakini naamini alama aliyoimaanisha haikuwa alama yoyote tu, sidhani kama alimaanisha uache alama kwa hali yoyote ile, hapana.
Naamini alimaanisha alama chanya katika ulimwengu.
Alama chanya katika ulimwengu huu wa sasa ambao moja kati ya lengo kubwa ni kumuinua mwanamke, kumtia moyo na kumkumbusha kwamba anaweza.
Mabinti wa kisasa wanajua kuacha alama. Alama tunaziona na tunaishi nazo katika jamii zetu.
Alama tunaziona kwenye kumbi za starehe, alama tunaziona mitandaoni, alama za kuutafuta umaarufu kwa namna yoyote ile.
Ndio!
Umaarufu.
Embu tujiulize kwa pamoja hizi alama tunazoziona mitandaoni na mitaani kwetu tunaweza kuzitumia kama mfano wa kuigwa kwa mabinti zetu?
Kabla hujanijibu niruhusu nikukumbushe kitu.
Mtaalamu moja wa mambo ya burudani aliwahi kusema kwamba katika dunia ya sasa muogope Mungu pamoja na teknolojia.Imani yangu iliniletea ukakasi kidogo kuukubali msemo huu nilitamani kumpinga na kumrekebisha niseme hapana muogope Mungu tu.
Ila si suala la kuficha, teknolojia ni ya kuogopwa pia.
Teknolojia inaishi, itaishi hata wakati ambao mlengwa akitoweka.
Kama ambavyo teknolojia itakavyoishi nadhani ingependeza sana kama alama ambayo mlengwa ameiacha ikaishi pia. Alama chanya ambayo itanyanyua vifua vya ndugu na jamaa zako kujinadi kwamba mwanamama fulani ni mtu wangu wa karibu.
Alama wanazozipigania mabinti wa kisasa sidhani kama mwanamama Hillary Clinton alizipigania pia kipindi akiwa binti au mama Getrude Mwongela alizitazamia kipindi akiwa kijijini kwao, sidhani nasisitiza sidhani kama Ummy Mwalimu aliutafuta umaarufu kwa njia kama ya mabinti wa kisasa kufika hapo alipofika.
Ndio nimesema umaarufu.
Mabinti wengi wanautaka umaarufu ili tu wajulikane mitaani, wajulikane mitandaoni, wafuasi wajae kwenye mitandao ya kijamii, mishale irushwe kwa wingi mingine waikwepe mingine iwachome waangukie magonjwa yasiyotibika kisha wafe.
Hivi alama hii inatosha kweli?
Haitoshi, lakini kabla hajutatupa lawama kwa mabinti niruhusu nichukue dakika zako kadhaa nikuoneshe tatizo lilianzia wapi.
Mtaalamu mmoja aliyafahamika kwa jina la Bwana William Golding aliwahi kunukuliwa akisema,
“Nadhani wanawake ni wapumbavu kujifanya wako sawa na wanaume, wako juu sana sana na siku zote wamekuwa hapo. Chochote utakachompa mwanamke atakifanya kiwe kikubwa zaidi.
Ukimpa mwanamke mbegu za kiume, atakuletea mtoto, Ukijenga nyumba ukamkabidhi mwanamke atakutengenezea mazingira ya nyumbani.
Ukimkabidhi mazaga ya jikoni mwanamke atakupatia chakula.
Ukimpa tabasamu mwanamke atakupa moyo wake.
Mwanamke atazidisha na kukuza chochote utakachomkabidhi.
Hivyo basi, ukimkabidhi upuuzi kaa tayari kupokea shehena la mavi”
Ndio, amesema shehena la kinyesi kwa lugha nyepesi.
Bwana William Golding alikuwa sahihi sana miaka hii ya karibuni tumemjaza binti upuuzi wa kutosha, upuuzi mtaani,upuuzi mitandaoni upuuzi upuuzi mtupu, sasa anatuzawadia mashehena ya kinyesi ya kututosheleza sisi sote.
Tugawane mashehena ya kinyesi kwa usawa , tugawane video za utupu mitandaoni, tugawane hizi alama za umaarafu zinazotafutwa kwa namna yoyote ile, tugawane nasema tugawane hivi sababu tumemjaza binti upuuzi kwa muda mrefu sana.
Lakini huenda tusiwapate tena kina Dkt. Joyce Ndalichako hapo baadae au watu kama mwanamama Asha Rose Migiro miaka ijayo kama tusipobadili uelekeo wetu kama jamii na taifa kwa ujumla.
Niseme wazi kwamba nafurahishwa na majina mapya kama Jokate Urban Mwegelo au Faraja Nyalandu ambao kabla hawajafika kuitwa wanamama wametengeneza majina yao.
Ni majina tofauti na mapya tofauti na yale ya awali lakini jitihada zao zinaongea.
Umaarufu wao kwa sasa si kwa idadi ya picha za kisasa zilizopo kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii tu au idadi ya wafuasi wengi walionao wanaowasifia kila kukicha kwa uzuri wao au wa picha wanazotupia, hapana.
Bali ni kwa alama chanya wanazoziacha katika jamii kila mmoja kulingana na nafasi yake, sipo hapa kuzimimina sifa na kazi zao la hasha! Bali kuzitumia kama kioo cha kuakisi mazuri yao kwa jamii na hasa kwa mabinti wa kisasa.
Natoa rai kwa jamii, kumsaidia binti aweze kujijenga, binti aweze kutengeneza njia ya kuwa bora zaidi, binti aweze kuacha alama itakayoishi duniani hata pale ambapo hatakuwepo, binti aweze kuitumia teknolojia kumtengenezea kesho yake yenye kumpa fursa zaidi na si kumdidimiza.
Naiwajibisha jamii kwa sababu tunachokipanda kwa binti ndicho tutakachokivuna. Kama tuna nia ya kumtengeneza Makamu wa Rais mwanamke ajae au hata Rais ajae basi tuanze kumuandaa binti bora kuanzia sasa.

Upvote
6