Binti katuchanganya mimi na kaka yangu

ankol

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2012
Posts
2,355
Reaction score
4,260
Haya majanga sasa.

Ni yuleyule binti tuliyekua tukiishi nae mtaani hapa na baadae akapata bahati ya kwenda nje ya nchi.

Msichana mstaarabu kwa muonekano, mpole, mwenye haiba na aibu tele, mwenye kujiheshimu kimavazi mbele za watu.

Kumbe nilinza nae kipindi kile alichokua akirudirudi likizo tukaahidiana tutaoana akishamaliza masomo. Ninampenda kwakweli ila baada ya kurudi nikaanza ona utofauti.Ingina hapa > https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/657002-mke-mtarajiwa-kaharibiwa.html < Sasa nilimwomba nikamtambulishe kwa kaka yangu lakini akadai anamwogopa sana akakataa, nikamwuliza kama anafahamiana nae akadai kwa sura tu anamjua.

Sikushtuka sana koz namfahamu ana aibu sana.

Baada ya siku kadhaa kupita nikiwa na mke huyu mtarajiwa, mara nikapata ujumbe toka kwa broo. Alimtumia rafiki yake aje kuniambia kua niachane na huyu mdada kwani alishatembea nae sana, nahisi kuchanganyikiwa. Tunaheshimiana sana na broo angu labda ndo mana kashindwa niambia direct.

Mawazo yamenitinga nikapata ujasiri nikampigia broo ku confirm.

Nilichojibiwa niko shocked! Nimeshare na broo! mbaya zaidi broo mwenyewe ni kicheche mbaya, mbaya zaidi bro anasisitiza si ulitumia condom dogo?'

Sijieleweielewi kwakweli nahisi kuchanganyikiwa
 
Kwani wote bro wako na huyo bint walikua wanajuana kuhusu wewe? walikua wanajua kuwa ni mashemeji? Ila pole sana mkuu...fanya checkup upate pa kuanzia.
 
Msichana mstaarabu kwa muonekano, Mpole, mwenye haiba na aibu tele, mwenye kujiheshimu kimavazi mbele za watu.....

Pole....naona alikuingiza king kwa kujifanya kondoo!!!
 
Pole kwa kuchanganyikiwa.
Kilichokuchanganya ni ku share na bro au bro kusisitiza kama ulitumia condom?
Yote yananichanganya. Lakini hili la kutumia condom ndio linaniua kabisa. Laaaah!
 
pole. kama vipi kapime ili kujiridhisha
 
hebu nami nikuulize.. 'dogo ulitumia kondom?'
 
na mi naomba kuuliza pia ulitumia condom dogo? kama kuna mda ulienda kavua aisee nenda kapime kama bado piga chini demu songa mbele usijitie mahaba niue utakufa kweli mkuu... wnawake wapole waogope lakini siyo wote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…