Binti kusafirishwa akiwa amefungwa Kamba kwenye basi Katavi – Moro, Polisi yatoa ufafanuzi

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Jeshi la Polisi mkoa Morogoro limetoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na Binti anayesafirishwa akiwa amefungwa kamba kwenye basi la Happy Nation 519 DXH inayotokea Katavi Mpanda kwenda Morogoro ambalo limeondoka Dodoma asubuhi ya leo Oktoba 2, 2024.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa Morogoro, SACP Alex Mkama imeeleza kuwa taarifa hiyo ya Mitandaoni ilieleza kwamba "Kuna msichana kafungwa kamba humo anasafirishwa na Mwanaume mmoja kwenye basi la Happy Nation 519 DXH inatokea Katavi Mpanda kwenda Morogoro limeondoka Dodoma mida hii asubuhi"

Taarifa hiyo imefuatiliwa kwenye vizuizi vya Mkoa wa Morogoro na kubaini kwamba Binti huyo aitwaye Amina Ramadhani Mohamed (28) mkazi wa Mpanda amefuatana na ndugu yake aitwaye Mohamed Ally Juma (36) Mkazi wa Nkasi Mkoa wa Rukwa kwenye basi lenye namba za usajiri T.106 DVF aina ya Youtong likitokea mkoani Katavi kwenda Mkoa wa Dar es salaam.
Baada ya mahojiano ya kina jeshi hilo limebaini kuwa watu hao ni ndugu ambapo wanakwenda mkoani Morogoro kwa ajili ya matibabu.

"Jeshi la Polisi linawashukuru wananchi waliotoa taarifa hizo na tunawaomba waendelee kutoa taarifa pale wanapoona jambo wanalolitilia mashaka ili taarifa hiyo iweze kufanyiwa kazi kwa haraka." imesema taarifa ya hiyo.
1727873883771.png
Pia, Soma:

--> Polisi Moro lasema linachunguza madai ya Askari Polisi kumshambulia Mwananchi anayemiliki banda la kuonesha mpira
--> Katavi: Binti ajaribu kuua kichanga baada ya kujifungua akiwa chooni, akihofia kuachika
 
Japo haijafafanua vizuri lakini imeeleweka
Maana kuishia kusema ni ndugu na wanaenda kwenye matibabu, ndugu wengi hupelekana kwenye matibabu sehemu za mbali bila kufungana kamba.

Nadhani wametuachia tuelewe kwa assumption kua aina ya changamoto aliyonayo bint ndo inafanya afungwe kamba.
 
Sawa sawa huenda ni changamoto ya afya ya akili kafungwa kwa usalama wake na abiria wenzake ila afande kafunika ili kutowapa taharuki abiria
 
Jeshi la Polisi mkoa Morogoro limetoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na Binti anayesafirishwa akiwa amefungwa kamba kwenye basi la Happy Nation 519 DXH inayotokea Katavi Mpanda kwenda Morogoro ambalo limeondoka Dodoma asubuhi ya leo Oktoba 2, 2024.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa Morogoro, SACP Alex Mkama imeeleza kuwa taarifa hiyo ya Mitandaoni ilieleza kwamba "Kuna msichana kafungwa kamba humo anasafirishwa na Mwanaume mmoja kwenye basi la Happy Nation 519 DXH inatokea Katavi Mpanda kwenda Morogoro limeondoka Dodoma mida hii asubuhi"

Taarifa hiyo imefuatiliwa kwenye vizuizi vya Mkoa wa Morogoro na kubaini kwamba Binti huyo aitwaye Amina Ramadhani Mohamed (28) mkazi wa Mpanda amefuatana na ndugu yake aitwaye Mohamed Ally Juma (36) Mkazi wa Nkasi Mkoa wa Rukwa kwenye basi lenye namba za usajiri T.106 DVF aina ya Youtong likitokea mkoani Katavi kwenda Mkoa wa Dar es salaam.
Baada ya mahojiano ya kina jeshi hilo limebaini kuwa watu hao ni ndugu ambapo wanakwenda mkoani Morogoro kwa ajili ya matibabu.

"Jeshi la Polisi linawashukuru wananchi waliotoa taarifa hizo na tunawaomba waendelee kutoa taarifa pale wanapoona jambo wanalolitilia mashaka ili taarifa hiyo iweze kufanyiwa kazi kwa haraka." imesema taarifa ya hiyo.
Pia, Soma:

--> Polisi Moro lasema linachunguza madai ya Askari Polisi kumshambulia Mwananchi anayemiliki banda la kuonesha mpira
--> Katavi: Binti ajaribu kuua kichanga baada ya kujifungua akiwa chooni, akihofia kuachika
Sawa mmeshukuru, SOKA et al wako wapi? Erythrocyte
 
Mkuu umeeleweka ila hapo kwenye usafiri umechanganya!Basi kutoka Dodoma kwenda Katavi kupitia Morogoro mara Dar Halipo !
 
Back
Top Bottom