POTOSHI Binti wa Obama ameonekana kwenye mitaa ya Marekani akiwa mjamzito

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2





​
 
Tunachokijua
Natasha marian Obama anajulikana kama Shasha Obama ni binti wa pili na wa mwisho wa Rais wa 44 wa Marekani, Barack Obama, na mkewe Michelle Obama. Alipata umaarufu mkubwa duniani baada ya kuishi katika Ikulu ya Marekani (White House) kuanzia mwaka 2009 hadi 2017 wakati wa uongozi wa baba yake.

Madai

Kumekuwepo na picha zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikidaiwa kumuonesha Sasha Obama, binti wa aliyekuwa Rais wa Marekani, Barack Obama, akiwa na ujauzito.
Picha hizo zinadaiwa kumuonesha Sasha akiwa katika maeneo ya Los Angeles, Marekani, wakati akiwa majukumu yake
Na pia kumekuwepo na madai yanaonyesha shasha obama akiwa wanapiga busu na penzi wake huko marekani

Uhalisia

Ufuatiliji zaidi umeonesha kuwa picha hiyo imehaririwa kwa kutumia teknolojia ya akili unde.

Licha ya hivyo picha inayosambazwa na picha ya awali imebainika kuwa picha halisi ya Sasha Obama ilichapishwa na tovuti ya whowhatwear.com ikimuonesha akitembea kwenye jiji la Lo angels marekani, ambapo awali picha halisi ilitolewa na tovuti ya Backgrid 22 july 2025

Sambamba na hilo picha inayonyesha shasha Obama akipiga busu na mpenzi wake imetemgenezwa n akili unde kutoka kwenye picha halisi ambayo imepigwa na tovuti ya daily mail mwaka 2023

Picha halisi inamuonyesha Sasha Obama, mwenye umri wa miaka 22, alionekana akiwa pamoja na dada yake mkubwa, Malia Obama, mwenye umri wa miaka 25, pamoja na marafiki kadhaa jijini New York.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…