Bio Disc haijatengezwa kwa maji ya chemchem, bali imetengenezwa kwa aina 13 za madini asilia yanayopatikana ardhini na kuunganishwa kwa
kutumia utaalam maalum uitwao NANO FUSION kwa kuchomwa kwa joto la hali ya juu mpaka kuibadili molecular formular yake, kama
vanavyotengeneza vifaa viitwavyo super conductors.
Muunganiko huu wa madini mbalimbali yaligandamizwa kwenye mgandamizo mkubwa yazalisha nguvu za asili ziitwazo Scalar Energy ambazo hupatikana kwenye chemchem mbalimbali zitoazotiba, yaani chemchem zenye healing powers.
Hii biodisc inafanya kazi kwa kuzihamisha hizo scala energy kwenye kimiminika chochote kilicho karibu kwa kutumia nguvu za uvutano kama zile za kwenye sumaku inavyozalisha umeme kwa kuzunguka anti-clockwise.
Hivyo ukiiweka hiyo biodisc chini ya chupa ya coca cola, itaikata gesi na kibadili ladha within a fraction of a second hivyo wanadai ikinywa kimiminika chochote kilichopitiwa na biodisc, zile nguvu zinaakisiwa kwenye kimiminika husika, hivyo ukinywa iwe ni maji, soda, chai, unakuwa umekunywa hizo scala energy hivyo zina nguvu ya utabibu.
Mimi binafsi ninamatatizo Fulani, hivyo nikaambiwa biodisc itanisaidia, nikanunua seti nzima, bahati mbaya kwangu haukunisaidia chochote, lakini nawaona wenzangu wakinishuhudia jinsi ilivyowasaidia, hivyo kunauwezekano ili ikusaidie, ni lazima uwe na imani nayo. Nahisi mimi haikunisaidia kwa vile niliitilia mashaka kuwa hizi nguvu za kwenye biodisc ni nguvu za giza.
Ukinunua complete set, inavyo vifaa 7 navyo ni Amezcua Biodisc, Amezcua Shower Shell, Amezcua Pewter Bio Disc, Amezcua Straw Tube, Allah Chi Pendant, Om Chi Pendant, Anahata Chi Pendant.
Hizi pendant zinavaliwa kama urembo, tatizo zina miungu wa Waislamu, Allah, Wahindu Om na wawatu wa Indonesia Anahata.
Kitendo cha kukosekana pendant ya God, ai Jesus au hata yenye alama ya msalaba, kulinitia mashaka kuhusu uwezo wa nguvu hizo na niposearch kwenye net, nikakuta vifaa vyote hivyo, vinatoka kwenye single source na formular yake ni top guared secret!.
Bei ya kiwandani ni $ 500, hizo nyingine ni gharama za kusafirisha na faida ya ajenti wao. Tembelea http://www.biodisc-energy.com/
Mie nililetewa vitu hivyo nikashawishika kuvinunua. Lakini nikaamua kufanya uchunguzi kidogo na haya ndio niliyong'amua.
Kwanza nilishtukia namna wanavyovitafutia soko. Wanatumia mtindo unaoitwa PRODUCT-BASED-PYRAMIDS, ambao una namna kama ya DECI na pyramids nyingine. Kwa nini kama ni kitu kizuri tusione kwenye TV kama vile wanavyotangaza bidhaa nyingine au kwenye magazeti? Kuna dawa nyingi zinazotangazwa kwenye vyombo hivyo kama dawa za kikohozi (Goodmorning, Cofta, Vicks Kingo n.k.), dawa za maumivu, dawa za malaria n.k.
Product based pyramids zinawaahidi wasambazaji comissions kadiri wanavyopata wasambazaji wengine na kadiri wanavyouza wao wenyewe. Hatari ya hizi ni kwamba, hawa wasambazaji wa mwanzo wanaanza zaidi kwa jazba wakidhani wana bidhaa zenye
"miujiza" fulani, na hivyo wanatumia nguvu nyingi sana kuzitafutia soko, na wakati mwingine kuziweka katika "stock" yao, na kujikuta wana overstock, na kupata hasara. Pia wana exploit udugu au urafiki au wa karibu au heshima ya cheo kwa ajili ya kutimiza malengo hayo ya biashara. Mara nyingi watasambazia ndugu zao na marafiki zao, kwa ile trust waliyo nayo kwao. Hata viongozi wa dini mpaka Maaskofu (kama ilivyokuwa kwa DECI) wanaweza kutumia dhamiri za waamini wao zinazowaamini kujiinua katika level ya wauzaji na kuongeza comission. Ethics za marketing za namna hiyo zina mashaka.
Pili hata bei yake naona ni ya juu sana. $700 ni kwenye maeneo yaTSh 1m ambayo kama mtu unaitoa kwa ajili tu ya kuondoa gesi ya Coca cola na kutafuta nguvu hiyo, naona ni jazba zaidi na kufuata mkumbo wa kitu kipya kuliko
tiba inayodaiwa kuwemo ndani ya hiyo bio disc. Questionable in terms of Value for Money.
Tatu, nadhani hizo scalar energy ni ambiguous na hazieleweki zinatibu nini hasa. Kama si mgonjwa mahututi, TZS 1m kwa ajili tu ya kuwa na tiba ya kitu kisichoeleweka: kisukari, kansa, ngoma etc. ni matumizi mabaya ya pesa.
Nne, kama ni masuala ya tiba, tunataka tuone madaktari waliobobea wanaeleza maelezo ya kina na kisayansi kuhusu tiba hiyo. Badala yake ni hao marketers ndio wanazinadi kwa ushabiki zaidi kuliko utaalamu. Hivi tunataka na mambo ya tiba yawe kiholela. BEWARE matapeli wanatafuta chance hizo.
Mie nimeshaletewa na nikatafakari sana, na nikapeleleza hata namna zinavyouzwa nikapata mashaka hayo. But wenye kuiamini endeleeni, lakini mkijipa nafasi kutafiti kidogo mtaona mashaka pia.