Biography Ya Regia Mtema

Joined
Jul 14, 2008
Posts
1,820
Reaction score
1,032
Uandishi wa Kitabu cha Marehemu Regia Mtema (Biography)

Kamati Teule iliyochaguliwa kuanzisha Taasisi ya Regia Mtema Foundation imedhamiria kufuatilia kuandikwa kwa kitabu cha Marehemu Regia Mtema kufuatia azimio lililoafikiwa katika kikao cha kwanza cha Marafiki wa Regia pale British Council na baadaye kuwekewa uzito katika kikao cha Kamati Teule.

Kamati Teule sasa inapenda kutoa fursa ya kualika mtu au kampuni yeyote ambayo inaweza kuifanya kazi hiyo ya uandishi kwa uharaka, ustadi na ubora wa hali ya juu. Itahitajika kujua mchanganuo wa gharama zote za zoezi zima.

Kazi hii inatarajiwa itahusisha kuweka kumbukumbu ya historia ya Regia, Kazi mbalimbali alizofanya, picha nk. nk.

Kama wewe ni mojawapo wa waandishi wa Biography au unamfahamu yeyote, tafadhali naomba tuwasiliane moja kwa moja kwa PM au kupitia barua pepe sam@danimex.com.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…