Nitaeleza kwa kirefu ninayo yajua kuhusu hii kozi na mambo yanyo ikumba.
1.Chama cha Wahandisi na mafundi wa vifaa tiba (Association of medical Engineers and Technicians Tanzania)-AMETT chini ya mwenyekiti wake Eng.Valentino Mvanga kuwa dhaifu .
Akiwa kwenye vikao vya Wizara haoneshi uwepo wa mahitaji ya wataalamu/Wahandisi wa vifaa tiba.
2.Wataalamu (Mafundi na Wahandisi)vifaa tiba waliopo , product zao kuwa dhaifu sana.Hapa Nina maanisha kuwa walioko kazini wana underperform kuliko wale waliko kwenye Kampuni (Local vendors).Mfano Mashine ikiharibika (HEAMATOLOGY ANALYZER).Technician aliyepo haiwezi kwa sababu ya knowledge ,spare parts na exposure ya hiyo mashine matokeo yake anaonekana Hana umuhimu na hakuna utofauti na ambapo hakuwepo.Awali Kampuni iliyo supply mashine ndiyo iliyokuwa inahusika pia na plan preventive maintenance na troubleshooting.Hali hii imendelea kuwa hivyo hata baada ya wataalamu wa vifaa tiba kuanza kuwepo kwenye hospitali zetu.
3.Makampuni ya vifaa tiba (Anudha Ltd,Crown medical solution,Biocare,Kasmedics,Pasific diagnostic, Pyramid pharm)Kuficha teknolojia, spare na mbinu kwenye mashine zao.Na hivyo kikitokea chochote atahitajika mwenye mashine Wala siyo fundi au mhandisi wa Hospitali .
4.Hakuna training kama ilivyo kwa Wenzetu Kenya wao kila mwezi Kuna training kwa Biomedical Engineers kwa updating mashine na changamoto za mashine hizo.Biomedical Engineers wanaonekana hawana umuhimu maana hawawi updated
5.Upatinaji wa spare parts za baadhi ya vifaa tiba kuwa shida .Mashine ikiharibika itachukua muda kutengenezeka na kuleta maneno ya kejeli kutoka kwa wahudumu wengine wa Afya (Physicians,Nurses,Lab scientists,Radiographers/Radiologists ,Anaesthetists).Kwa kipindi ambacho Biomedical technicians wameajiliwa ,kwa baadhi ya hospitali uhitaji wao umepungua kutokana na kutokuona umuhimu wao tena