Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Kampuni ya nchini Ujerumani ya teknolojia ya biolojia - BioNTech pamoja na mshirika wake wa kimarekani, Pfizer, wameomba kibali cha dharura nchini Marekani, cha matumizi ya chanjo dhidi ya virusi vya corona kwa watoto wa chini ya miaka mitano.
Makampuni hayo mawili yamesema kuwa chanjo hiyo itaweza kutumiwa kwa wajili watoto wachanga kuanzia umri wa miezi sita. Ikiwa Taasisi ya Marekani ya usalama wa chakula na dawa, FDA itaridhia kibali hicho, chanjo ya BioNTech itakuwa ya kwanza duniani kwa watoto wa umri huo.