Biriani ya nyama

Biriani ya nyama

farkhina

Platinum Member
Joined
Mar 14, 2012
Posts
14,568
Reaction score
16,917
Mahitaji

Nyama nusu

Chumvi kiasi

Mafuta 1 Kikombe

Vitunguu maji 3 vikubwa

Nyanya 3 kubwa

Nyanya kopo

Thomu 1 table spoon

Tangawazi 1 table spoon

Pilipili mbichi iliyosagwa 1 tea spoon

Kotmiri (giligilani) iliyokatwa 2 Vijiko vya chakula

Viazi 6

Uzile wa unga 1table spoon

Mtindi ¼ Kikombe cha chai

NAMNA YA KUTAYARISHA KUPIKA

1. Kwenye karai au (sufuria) mimina mafuta Yakishapata moto mimina vitunguu vikaange mpaka viwe rangi ya hudhurungi. Vitowe viweke pembeni.

2. Kaanga viazi na viweke pembeni.

3. Chukua sufuria tia nyama, thomu, tangawizi, pilipili, nyanya, nyanya ya kopo, mtindi. Chemsha mpaka iive.

4. Tia vile vitungu ulioyovikaanga, tia viazi, uzile, kotmiri na yale mafuta uliokaangia vitunguu kama ¼ kikombe, acha moto mdogo mdogo kama ¼ saa, epua weka pembeni.

VIPIMO VYA WALI

Mchele kg 1

Mdalasini mzima wa vijiti

Zafarani ½ kijiko cha chai

Rangi ya biriani ¼ Kijiko cha chai

Mafuta yaliyokaangiwa vitunguu ½ Kikombe

Chumvi kiasi

Zabibu kavu.

Roweka zafarani na rangi kwenye kikombe na ¼ kikombe cha maji. Roweka kabla ya robo saa.

NAMNA YA KUTAYARISHA

1. Osha mchele uroweke kwenye maji muda wa dakika 20.

2. Chemsha maji kwenye sufuria kama magi 10.

3. Tia mdalasini.

4. Yakishachemka unatia mchele,chemsha usiive sana, unamwaga maji.

5. Unamimina tena ule mchele ½ yake kwenye sufuria, unatia rangi na zafrani kidogo na zabibu halafu unamimina mchele uliyobakia unatia rangi iliyobakia.

6. Mafuta yake unayachemsha mpaka yachemke unamimina juu ya mchele, unarudisha motoni unaweka moto mdogo ukisha kuiva, tayari kupakuliwa.

7. Unapakuwa wali unaweka chini kwenye sahani na juu yake sosi ya nyama.
 
Attachments

  • 1384629028931.jpg
    1384629028931.jpg
    82.9 KB · Views: 1,517
asante mpishi mahiri. Mie biriani napenda sosi tu, nakula na ubwabwa wa kimatumbi bila rangi. Ila sasa kucheua kutwa nzima!
 
umenifunza kuweka mafuta ya vitunguu kwenye mchele. Naamini itanogesha zaidi. Kila siku nakuibia moja lol
 
Farkhina
Hebu kama unajuwa kupika ile nyama ya kwenye harusi za waarabu inakuwa na vitunguu thomu na tangawizi nyingi naomba utuandikie
Inaonesha mpishi mzuri au unatangaza dau ili vijana wachakarike?
 
Dau gani wewe babu? Hiyo nyama eleza vizuri..
 
Farkhina
Kwenye harusi za waarabu kunaletwa nyama kama imekaushwa lakini inakuwa na masalo masalo nzuri sana na huwa ninaipenda lakini sijuwi wapi nitaipata kwani kwasasa sipo mikoa ya pwani kwahiyo siipati na huku nilipo hakuna waarabu kama wa pwani
Dau la mahari kwani wanajuwa mke mpishi dau kubwa

Nimeshaijua hiyo nyama....ila babu weye una lako jambo lol
Umewahi kula maini pia yaliyopikwa hivo hivo?
 
Mahitaji

Nyama nusu

Chumvi kiasi

Mafuta 1 Kikombe

Vitunguu maji 3 vikubwa

Nyanya 3 kubwa

Nyanya kopo

Thomu 1 table spoon

Tangawazi 1 table spoon

Pilipili mbichi iliyosagwa 1 tea spoon

Kotmiri (giligilani) iliyokatwa 2 Vijiko vya chakula

Viazi 6

Uzile wa unga 1table spoon

Mtindi ¼ Kikombe cha chai

NAMNA YA KUTAYARISHA KUPIKA

1. Kwenye karai au (sufuria) mimina mafuta Yakishapata moto mimina vitunguu vikaange mpaka viwe rangi ya hudhurungi. Vitowe viweke pembeni.

2. Kaanga viazi na viweke pembeni.

3. Chukua sufuria tia nyama, thomu, tangawizi, pilipili, nyanya, nyanya ya kopo, mtindi. Chemsha mpaka iive.

4. Tia vile vitungu ulioyovikaanga, tia viazi, uzile, kotmiri na yale mafuta uliokaangia vitunguu kama ¼ kikombe, acha moto mdogo mdogo kama ¼ saa, epua weka pembeni.

VIPIMO VYA WALI

Mchele kg 1

Mdalasini mzima wa vijiti

Zafarani ½ kijiko cha chai

Rangi ya biriani ¼ Kijiko cha chai

Mafuta yaliyokaangiwa vitunguu ½ Kikombe

Chumvi kiasi

Zabibu kavu.

Roweka zafarani na rangi kwenye kikombe na ¼ kikombe cha maji. Roweka kabla ya robo saa.

NAMNA YA KUTAYARISHA

1. Osha mchele uroweke kwenye maji muda wa dakika 20.

2. Chemsha maji kwenye sufuria kama magi 10.

3. Tia mdalasini.

4. Yakishachemka unatia mchele,chemsha usiive sana, unamwaga maji.

5. Unamimina tena ule mchele ½ yake kwenye sufuria, unatia rangi na zafrani kidogo na zabibu halafu unamimina mchele uliyobakia unatia rangi iliyobakia.

6. Mafuta yake unayachemsha mpaka yachemke unamimina juu ya mchele, unarudisha motoni unaweka moto mdogo ukisha kuiva, tayari kupakuliwa.

7. Unapakuwa wali unaweka chini kwenye sahani na juu yake sosi ya nyama.
Mwanawee utatupasua mtumbo !! naona umebobea mapishi ya kinyumbani....
 
Back
Top Bottom