Biriani ya Samaki

farkhina

Platinum Member
Joined
Mar 14, 2012
Posts
14,568
Reaction score
16,917
1.Samaki wa kipande 1/2 kg

2.Mchele 1/2 kg

3.Vitunguu maji 2

4.Carrot 1 kubwa ikwaruze

5.Mdalasini 1 teaspoon

6.Bizari ya pilau 1/2 tablespoon

7.Nyanya ya kopo

Kitunguu saumu na tangawizi 1 teaspoon kila Kimoja

Chumvi kiasi



Namna ya kutaarisha

1.Kaanga kitunguu maji hadi kiwe rangi ya kahawia

2.Weka kitunguu saumu na tangawizi

3.Weka tuna koroga vizuri

3.Mimina nyanya ya kopo pamoja na bizari ya pilau na mdalasini bila ya kusahau chumvi...

4.Ukimaliza weka pembeni

5.Katika sufuria nyengine chemsha maji weka na chumvi kidogo

6.Tia mchele na uwive half way (uwe na kiini)..

7.Chukua tray minima wali kidogo...

7.Mimina carrot

8.Mimina wali tena kdg

9.Mimina mchanganyiko wa Samaki

10.Mimina wali uliobakia

11.Funika weka kwenye oven 350 degree

12Angalia ikiwa imewiva pakua weka mezani
 
Unanifanya nijisikie hamu ya kula hiyo biriani wakati nimesha kula usiku huu Wali kwa mchuzi wa kuku na mboga ya mchicha asante mama mkwe farkhina ngojea niwakaribishe marafiki zangu watatu Mkuu utafiti njoo ule biriani Mkuu BAK unakaribishwa mama mkwe wangu kula biriani kaka Globu njoo unisaidie kula biriani nimealikwa kula biriani na imenishinda hahahah
 

Shukraan nawe kwa kuwaalika marafiki zako wasijali karibuni sana lol
 
Shukrani Mkuu MziziMkavu sijawahi kula biriyani ya samaki wala pilau ya samaki, machoni inavutia bila shaka mdomoni pia itakuwa tamu sana.

 
Last edited by a moderator:
Ahsante kwa kuniita sisy..ila hii kuiandaa nahisi kama itanishinda...ntamforwadia wifi yako ajifunze
 
Shukran jaan. Naitamanije hii kitu. Ila mm napenda ya nyama zaidi ila hapa Angel Nylon atanyanyuka na sahani lol..
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…