Birthday Parties To Our Lovely Kids: Ni muhimu au hazina maana?

Kwangu mimi naona birthday haina umuhimu wowote ule.
Na sioni mantiki ya kufanya birthday nikiwa kama mzazi sioni umuhimu wake maana sherehe ya kufurahi na mtoto wangu nae anajisikia ni x-mass, new year, pasaka na Idd

Kama alivyosema BelindaJacob, ni furaha kwa mzazi. Watoto wengi wanakufa chini ya umri wa miaka mitano. Hivyo kwa mwanao kuendelea kuishi, pekee ni furaha kubwa. Labda, kwa kuongeza wale wenye imani si vibaya,pamoja na sherehe, kufanya kitu cha kumshukuru mungu (kwa mfano wakatoliki unaweza ukaomba misa ya shukrani) ili kumjenga mtoto kiimani pia.

Fidel80, wewe una mtoto?
 
bravo
GOOD STUFF!


Fidel80, wewe una mtoto?
good question!
 
Birthday party mie naona muhimu kama mzazi mfuko unakuruhusu kumfanyia mtoto wako kumbu kumbu. Vile vile hata kwa watu wazima ni muhimu pia.
 
Ooh hell yeah...I go all out for my cute little munchkin
 
kama pesa inaruhusu kwa wakati huo sawa, sio iwe ya lazima kila mwaka....
 
mimi nadhani hakuna ubaya wa kufanya sherehe ndogo kwa ajili ya kukumbuka siku ya kuzaliwa, nasisitiza iwe sherehe ndogo, ni muhimu kwa ajili ya kumjenga mtoto kuthamini maisha yake na kutamani kufikia kuiona birthday nyingine, lakini inategemea kamqa uwezo unaruhusu, maana siku hizi kuna mambo ya ajabu mtu anakutaka umchangie mpaka birthday party,hili silikubali hata kidogo
 
Fidel80, wewe una mtoto?

Yeah mi mzazi.
Lakini birthday siipendi kabisa hata tarehe niliozaliwa mimi nilisha sahau kama kuna kuandika kwenye doc. iwa nampigia mama ananikumbusha.
 
Ah mbona mie nina miaka 87 sasa na the only party i celebrated was my 21st..tena nikajifanyia mwenyewe chuoni....the other day namuuliza mama kama hiyo siku ( it was birthday) rings a bell na hata!!! hana habari... sidhani nimepungukiwa na chochote kwa kuwa sikufanyiwa bday kila mwaka na wazazi.
 
Yeah mi mzazi.
Lakini birthday siipendi kabisa hata tarehe niliozaliwa mimi nilisha sahau kama kuna kuandika kwenye doc. iwa nampigia mama ananikumbusha.

Mkuu,
Makuzi ya watoto hutegemea sana tabia za wazazi wao.
 
Hivi wakubwa,
Kuna umuhimu wa kuwafanyia kajisherehe japo kadogo ka kuikumbuka siku yao ya kuzaliwa watoto wetu bila kuangalia kwamba hawalitambui hilo?

...mkuu umuhimu upo kwani; kila jema utalowatendea wanao sasa ni 'investment' yako kwao wakati utapokuwa kwenye 'fainali za uzeeni!'
 
Mimi ni bora nisherehekee birthday na new year kuliko hizo nyingine. Naona hazihusiani na chochote kwangu mimi kama mwafrika ambaye bado naabudu imani/dini za mababu zangu wa kiafrika za miaka 300 iliyopita!
Kaka hao wazee walisheherekea hizo birthday party za kuzaliwa!? lol!

Tuendelee tu na kuiga, Birthday party, Father day, mother day, sister day, brother day, guys day... zote na washeherekee tu... as long pesa ni yako... poa tu kwani ufisadi upo mpaka kwenye matumizi yako ati.

 
Last edited:
[ame="http://www.youtube.com/watch?v=OPmYbP0F4Zw"]YouTube - Broadcast Yourself.[/ame]
 
Baba akiwa msaurifu basi na watoto nao watakuwa wasaurifu pia?

Duh! Dogo apo 'umebaka sana' lugha, umetokea kule kwenye mapigano nini?


Hapo ni "msahaulifu' na 'wasahaulifu'.

Na kisayansi sio lazima watoto wawe wasahaulifu ila wanaweza kuwa na vijinasaba vya usahaulifu kwenye damu yao, kwa hiyo ukakuta wajukuu ndo wasahaulifu 'kama babu yao'
 
Mimi naona birthday party kwa watoto wetu ni muhimu hasa kutokana na karne hii tuliyokuwepo ya utanda wazi na siyo kama starehe wengine wasemavyo kwani inaimarisha upendo kati ya wazazi na watoto na kumfanya mtoto ajisikie na yeye yupo katika ulimwengu wa sasa.Na unapo fanya b'day siyo lazima sherehe kubwa ya kualika watu wengi ni ile hali ya mtoto kujumuika na watoto wenzake kwa kile kidogo ulichonacho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…