Biteko afagilia ukuta kupaisha mapato Tanzanite

esther mashiker

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
616
Reaction score
552


WAZIRI wa Madini, Doto Biteko, amesema tangu kujengwa kwa ukuta wa kuzuia utoroshwaji wa madini ya tanzanite wilayani Simanjiro mkoani Manyara, serikali imeongeza mapato, kwa kukusanya kodi Sh. bilioni mbili kwa mwaka 2018/19.

Akizungumza na wachimbaji wadogo wa tanzanite, Biteko, alisema awali serikali ilikuwa ikikusanya kodi Sh. milioni 70, lakini baada ya kujengwa kwa ukuta huo, mapato yameongezeka hadi kufikia kiasi hicho. Biteko aliiagiza wizara yake kuwaongeza wathaminishaji wa madini katika eneo hilo, kutokana na idadi kubwa ya watu wanaohudumiwa kwenye migodi hiyo, wamekuwa wakicheleweshewa huduma kutokana na uchache wa watumishi.

“Katibu Mkuu wa wizara nakuagiza ongeza wathaminishaji wa madini haraka, kwa sababu wachimbaji na wanafanyabiashara, wanaonunua madini, wamekuwa wakilalamika mizigo yao inapakiwa kwa wakati, lakini wanachelewesha kuitoa kwa wakati kutokana na kutokufanyiwa tathmini kwa haraka,” alisema Biteko.

Aliwataka watumishi wa madini kuacha tabia ya kufunga ofisi hizo mara kwa mara, badala yake watumie muda mwingi kukaa ofisini kuwahudumia watu kwa sababu wanatumianguvu nyingi kufikisha madini katika eneo hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Zephania Chaula, aliwataka wachimbaji hao, kufuata sheria, kanuni na utaratibu uliowekwa wakati wakiingia ndani ya machimbo hayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…