Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mkutano huo ambao unafanyika kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete umepangwa kufanyika kwa siku tatu mfululizo leo ikiwa ni siku ya tatu.
Kabla ya Mgeni rasmi kuwasili Wadau wa NGO wanaendea na majadiliano.
Mada: Teknolojia na Ubunifu kwa ajili ya Ustawi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali: Fursa na Changamoto
Maxence Melo
Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Forums anachangia kwa kusema: Teknolojia imerahisisha utendaji wa kazi wa Watu wengi, imeingia sehemu zote, imerahisisha mifumo ya fedha katika mashirika yetu, makubwa kwa madogo.
Ndio maana wengi wamekuwa wakipata mafunzo ili kupata elimu kuhusu Ulimwengu wa Kidigitali.
Miaka ya nyumba kuna wakati mwingine Mashirika yalikuwa yakitumia vishoka kwenye uwekaji mahesabu sawa ambao kuna muda hawakuwa na utendaji sahihi na hivyo wakawa wanasababishia Mashirika kuingia katika mgogoro na Serikali wakati wa muda wa ukaguzi wa Mashirika.
Sasa hivi kuna Akili Menmba “AI” ambayo inatumiwa katika njia nyingi ikiwemo hata kuandika maandiko mbalimbali, kujieleza kwa Wahisani na mengine mengi ikiwemo kusaidia kuelewa kazi unayoifanya mbele ya hadhira unatofanya nayo kazi.
Kuhusu suala la Uwajibikaji, Asasi za Kiraia zikitumika vizuri, zinaweza kufikisha kazi zetu kwa Umma na kurahisisha mambo mengi, tunatakiwa kuhakikisha kile tunachokipigania ndio hitaji hasa la Wananchi husika.
Upande wa Asasi za Kiraia kwa kuwa tunafanya kazi kwa uwazi ni rahisi kuona hata pesa zimetumika katika matumizi sahihi, hiyo pia itasaidia Wahisani kuona kila kitu kinafanyika vizuri.
Mfano sisi JamiiForums tunatoa mafunzo, tunapita kila Kanda kwa namna bora ya kutoa mafunzo ya Kidigitali na namba bora ya kuwafikia Wahisani.
Nipo Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, kuhusu Sheria hiyo ipo na imeshaanza kufanya kazi, inagusa pia mashirika yetu kwa ukaribu.
Mimi nina wajibu mkubwa wa kuhakikisha pale mnapohitaji kupata elimu ya kukusanya taarifa za Watu kwa kuzichakata, kuzitunza na kuzitumia, ninafanya hivyo, pia kama Tume tunafanya mafunzo hayo bure, hiyo ni Elimu muhimu.
Tupo tayari kutembelea Kanda, tunatakiwa kuanza na elimu kwa wadau, Sheria ikianza kuingia na kutumika rami kwenye Mashirika yetu inaweza kuwa na athari nyingi, kwa kuwa watu wengi bado hawana utayari huo.
Hivyo, ukiona kuna mafunzo ya kuhusu Sheria au Elimu ya Taarifa Binafsi ni vizuri ukashiriki na kujifunza kuchakata taarifa na kuzitunza.
Pamoja na yote tunatakiwa kufahamu kuwa Taarifa Binafsi za Watu wenu zinatakiwa kutunzwa vizuri, kinyume na hapo unaweza kujikuta ukipata matatizo.
Niwasisitize tu ndugu zangu Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ipo na inapatika kwenye tovuti ya Bunge.
Francisca Mboya
Francisca Mboya kutoka Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO) anasema Tathimini na ufuatiliaji ni jambo muhimu sana katika mashirika yetu, Mashirika mengi hayatumii teknolojia, hata ukiuliza Mtu mmojammoja kwenye Shirika kuhusu utumiaji wa AI watakwambia hawatumii.
Ukifanya uchunguzi kiuhalisia wanatumia lakini hawataki kuonesha kuwa wanafanya hivyo.
Matumizi ya Teknolojia ni muhimu, ukitumia unapunguza gharama, mifumo hiyo pia inarahisisha uchakataji wa taarifa, mfano unaweza kukuta kuna Mashirika ambayo Mkurugenzi anafanya kila kitu, hilo sio sawa.
Hivyo, tusione aibu, tutumie AI inasaidia na inarahisisha utendaji kazi, mfano matumizi ya lugha ya Kingereza kwa kuwa lugha hiyo kwetu ni ya pili, unaweza kutumia kurahisisha matumizi na kunyoosha lugha.
Hasna Ally
Hasna Ally ambaye ni Mwakilishi wa Taasisi ya Urafiki Girls Organization anasema:
Kuna Watu wakisikia kuhusu teknolojia wanafikiria labda ni masuala ya kurusha ndege na vitu vingine vikubwa lakini sio hivyo.
Teknolojia inaanza na vitu vidogo na inaenda hadi kwenye hayo mambo makubwa.
Mara nyingi mashirika madogo yanakutana na changamoto ya kukosa Wataalam wa Teknolojia na ndio maana wengi wao wanajikuta wanafanya mambo mengi kienyeji.
Asha Abinallah
NGO tunapoteza sana taarifa kwa kuwa hakuta utunzaji mzuri wa taarifa, mfano matumizi ya e-mail, kwenye Taasisi unakuta kila mfanyakazi anatumia yake binafsi kwenye kazi za kiofisi.
Siku ikitokea Mfanyakazi husika ameondoka, anaweza kuondoka mna taarifa nyingi za ofisi, e-mail aliyokuwa akitumia ni ya kwake binafsi, huwezi kumwambia akupe e-mail.
Hivyo, ni vizuri kutumia e-mail ya ofisi ni vitendea kazi vingine ya kiofisi ili siku mtu akiondoka unaweza kubadilisha nywila au jina la mtumiaji kisha akapewa mtumiaji mwingine au inakuwa rahisi kupata taarifa.
Mfumo wa Usajili wa Mashirika kwa njia ya Elekroniki, ni moja ya ishara ya Serikali kutambua umuhimu Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGO’s).
Wizara ya Fedha ipo katika mpango wa kuandaa muongozo kwa ajili ya Asasi Zizizo za Kiserikali ambapo mchakato huo ukikamilika utakuwa unajumuishwa kwenye Bajeti ya Serikali.
Serikali haitapuuza wala kudogosha hata kidogo mchango wa Mashirika kwenye maendeleo ya Nchi yetu katika nyanja zote, ikiwemo za Kiuchumi na Kijamii kwa kuwa ni Mdau mkubwa.
Kazi ya Serikali ni kumhudumia Mtanzania, kinachofanywa na Mashirika pia ni kuisaidia Serikali kutekeleza majukumu kwa urahisi na kumsaidia Mtanzania
Tumeambiwa fedha zilizopatika kwenye NGO ni Tsh. Trilioni 2.6, zimezunguka Nchi nzima, inawezekana kuzitaja ni rahisi, jiulize kuna watu wangapi wamenufaika kwa kupitia fedha hizo, kazi hiyo haiwezi kufanywa na Serikali peke yake.
Kuna ajira zaidi ya 21,000 ambazo zimepatikana kupitia Mashirika hayo. isingekuwa NGO ingekuwa ni jukumu la Serikali.
Jiulize Watu wangapi wamepata huduma, wamepata msaada wa aina mbalimbali ikiwemo manyanyaso ya kijinsia. Mashirika yataendelea kuwa Mdau na rafiki wa Serikali.
Serikali haiwezi na haina mpango wa kusigana na NGO bali ina mpango wake kusaidia mtimize majukumu yenu.
Tekelezeni majukumu yenu kwa kuzingatia maadili na tamaduni za Mtanzania, msikubali mtu au Watu wakawashawishi kuingia katika maadili ambayo siyo ya kwetu.
Rais Samia Suluhu Hassan alianzisha Kampeni ya Nishati Safi ya Kupikia, hapa Duniani, Watu Bilioni 5.8 wanatumia nishati safi ya kupikia, Watu Bilioni 2.4 wanatumia nishati isiyokuwa safi na kati yao Watu Milioni 933 wanatoka Afrika, na tumeambiwa kuwa tafiti zinaonesha Watu Milioni 3.7 kila Mwaka wanafariki kutokana na magonjwa yanayotokana na nishati isiyokuwa safi.
Kwa Tanzania zaidi ya Watu 30,000 wanafariki kila mwaka kutokana na magonjwa yanayotokana na nishati isiyokuwa safi ambayo wayu wanatumia.
Tafiti zinaonesha kati ya watu wanaokufa 60% ya Watu wote hao ni Wanawake na Watoto ambao kwa kiasi kikubwa wanahusika na matumizi ya nishati isiyokuwa safi.
Tuendelee kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa Watanzania ili inapofika Mwaka 2034 basi Asilimia 80% ya Watanzania wote wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.
Kwanza ni kuhakikisha nishati hiyo inapatikana kwa bei nafuu.
Pia, taratibu za NGO kuchukuliwa kama makampuni ya kawaida, nataka kuwaomba wale tuliopo Serikalini kusimamia hilo.
Kama Mtu akiomba jambo majibu ni mawili, ndio au Hapana, ukiona Mtu anaongeza jibu la Tatu ujue huyo ana ajenda yake, najiuliza kama NGO zimesajili kwa mujibu wa Sheria, kama zimeoba status Fulani tunahitaji kitu gani huyo anayetakiwa kutoa jibu, asitoe jibu.
Kama jibu ni Hapana mwambie Hapana, ukimwambia utampunguzia muda wa kuzunguka, kuliko kumwambia njoo kesho, ukifanya hivyo unatengeneza njia ya Rushwa.
Nasema hivyo kwa kuwa kila mwaka wanapoita mgeni rasmi, NGO zinakuwa na maelezo yakeyale, maana yake wamekuja Dodoma kupiga picha, lazima wapate majibu ya maswali na hoja zao, hilo siyo jambo la hisani ni haki yao.
Zaidi ya Watu 21,101 wameajiriwa katika NGO, najua kuna NGO ambazo ukisikia malengo yao hata masikio yanakuwasha lakini hizo zisiwe njai ya kuhukumu zile nyingine ambazo zina nia nzuri.
Zipo NGO zimechaguliwa kutoa elimu ya mpiga kura na kufanya uangalizi wa zoezi la daftari la mpiga kura, tutambue umuhimu wa zoezi hilo tutimize hilo kwa kuwa ni muhimu kwa Demokrasia.
Niwaambie wale wanaotumia nafasi hiyo watekeleze majukumu kwa weledi wa hali ya juu wakitambua umuhimu wa mchakato huo, kama una mahaba ya chama weka mahaba binafsi pembeni ili utoe elimu.
Pia soma ~ Day 2: Mkutano wa Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Dodoma, Septemba 5, 2024