WoS, kwanza nakushukuru sana kwa kuleta hii taarifa nyeti hapa jamvini. Inasadia sana kupunguza akina Thomaso. Hata hivyo ninapatwa na wasi wasi na ningependa kujua baadhi ya vitu au najiuliza hivyo vitu. Kama kweli mtoto kama Gift alifanyiwa hayo mambo angawezaje kutembea hadi nyumbani na inawezekanaje afanyiwe mara kadhaa bila kuchananwa. Vinginevyo alikuwa anachezewa tu bila kuingiliwa (there was no intromission). Na kwa watoto wengine, je waliingiliwa na hakuna aliyeumizwa (physicall) kwa kuchanika? Hilo bado linanitatiza kidogo. Na kama hawa watoto walifundishwa hiyo hadithi, kulikuwa na utaratibu mzuri wa ku-scrutinise ili kuhakikisha kuwa wanaongelea yaliyotokea na si yale waliyofundishwa?
Naguswa sana kama mzazi ila hayo maswali bado yananisumbua.
DC,
mimi pia nilikuwa mmoja wa watu waliokuwa hawaamini kilichotendwa na Babu Seya na wanawe kwa sababu zifuatazo:
1. Kama mpenzi mkubwa wa mwanamziki Nguza, sikuamini Nguza aliyekuwa anaonekana mtu mtaratibu, mkimya na serious kwenye kazi yake angeweza kufanya kitendo kama kile
2. Sikuamini kama Nguza angeweza kabisa kushirikiana na watoto wake kufanya ufirauni kama ule kwa maana kama mzazi naamini kabisa nahitaji kuweka umbali baina yangu na watoto wangu inapofikia mambo binafsi na nyeti yanayoweza kukukwaza malezi.Mzazi yeyote anataka wakati wote kuonyesha taswira chanya kwa watoto ili watoto waweze kuiga mema na siyo mabaya.
3.Kipindi kesi inatokea, ilikuwa ni wakati Nguza na mwanaye Papii wamepata umaarufu mkubwa baada ya kuimba kwa mara nyingine na kwa pamoja wimbo wa " Seya", hii ilifanya wengi kuamini ilikuwa ni mbinu kuwaangamiza kibiashara.
Pamoja na yote haya, kesi iliendeshwa kwa usiri kufuatana na matakwa ya sheria
( in camera) ili kulinda haki za watoto waliofanyiwa kitendo.
Hata wakati kesi inaendelea na hatimaye hukumu kutolewa bado niliamini kuwa washtakiwa wamesingiziwa.
Hata hivyo sikuishia hapo..nilianza binafsi kufanya utafiti wangu... kupata mawazo ya waliohusika kwenye kesi kwa namna moja ama nyingine na hatimaye kupata hukumu yenyewe.
Tukumbuke kuwa hadi Babu Seya anakamatwa, ilishapita muda mrefu..haina maana
Oct 2003 ndipo vitendo vilifanyika... ni kwamba kuwa-abuse watoto kulifanyika muda mrefu sana hadi hao watoto wakawa wamesha haribika....mtoto Gift akiwa ndiyo aliyepelekea kupeleleza na kukamatwa kwa wahusika.Hivyo hoja ya kushindwa kutembea kwa kipindi hicho naiwezi kusimama maana walishaharibiwa siku nyingi hadi kuzoea.
Kumbuka pia kuwa Gift alifikia mahali Babu Seya akampa
hadhi ya kuwa
"mama".na watoto wengine kuwa
"watoto" hii inaashiria kukomaa katika huo mchezo.Pia ujira aliokuwa anawapa hao watoto haukuzidi sh.200/=.Mahakamani Gift alimdai Nguza sh.1,400/-kama
malimbikizo! Hii itakuambia ni jinsi gani na kwa kipindi gani mchezo huo ulikuwa unafanyika kabla ya kugundulika.
Yapo mengi sana katika kesi hii.
mwisho wa yote nadhani hakuna ubishi kwamba wakina Nguza walistahili adhabu wanayoitumikia sasa.