Black Dahlia:Kifo cha kikatili zaidi kuwahi kutokea -2

Napoleon Jr

Member
Joined
Apr 2, 2018
Posts
62
Reaction score
36
Kwanza kabisa natanguliza shukhran zangu dhati kumshukuru muumba mbingu na nchi kwa kunipa nafasi hii kuweza kujumuika na wanajukwaa wenzangu katika makala hii ya Black dahlia.Pili natanguliza samahani kwa wanajukwaa wote kwa kitendo cha kuleta uzi nusu katika sehemu ile ya kwanza samahanini sana wakuu.Kwa wasomaji wapya ningependa muipitie kwanza Black Dahlia Sehemu ya kwanza
katika makala iliyopita nilieleza jinsi mauaji ya kutisha ya Elizabeth Short yalivyotokea na jinsi FBI kwa kushirikiana jeshi la polisi la Los Angeles walivyofanikiwa kuutambua mwili huo.Leo katika makala hii tutamwangalia zaid aliyekuwa mmoja katika ya watu 150 ambao walishukiwa kuhusika katika mauaji hayo.Mtu huyo alitambulika kwa jina Dr.George Hill Hodel
George Hill Hodel, Jr. alizaliwa mnamo Oktoba 10, 1907, na kukulia huko Pasadena, California. Wazazi wake, George Hodel, Sr. na Esther Hodel, walikuwa wayahudi wenye uraia wa urusi. Baada ya kumaliza elimu yake bwana George Hodel alifanikiwa kuwa mmoja kati ya madaktari walioheshimika sana katika jamii aliyoishi.Baadae daktari huyu alikuja kuwa mtuhumiwa mkuu katika mauaji ya Elizabeth Short. Katika miaka ya hivi karibuni, amekuwa akihusishwa na kesi kama 'Chicago lipstick murder'' na 'Zodiac killer'. Hodel alikufa akiwa na umri wa miaka tisini kutokana na matatizo ya moyo.
Je ilikuaje mpaka kwa mtu mwenye taaluma nzuri kama yake kuwa mtekelezaji wa mauaji yale ya kinyama.Maswali haya yalipatiwa majibu kupitia kitabu cha 'Black Dahlia avenger' kilchoandikwa na mtoto wa Dr.George Hodel bwana Steve Hodel.Huyu alikua ni askari wa kikosi cha 'los Angeles police derpatment'.(LAPD).
Mkasa mzima ilikua hivi.....
Siku chache baada ya kifo cha baba yake,Steve alikua akipitia baadhi ya mali za baba yake.alipata albamu ya picha iliyokua imetunzwa katika sanduku. Ilikuwa ndogo ya kutosha kiganjani kwake. Albamu hiyo Ilijaa picha za kawaida - mama yake, baba na ndugu - pamoja na picha za familia zilizochukuliwa na msanii maarufu duniani Man Ray, rafiki wa familia.
Lakini nyuma kabisa katika albamu ile alikuta picha mbili za mwanamke kijana, macho yake yalijawa na mshangao kwani aliitambua kabisa sura ile kimoyo moyo alijisemea . "Mungu wangu, inaonekana kama ndie Black Dahlia."..
Lakini kabla hatujaendelea mbele zaidi ebu tuangalie utata zaidi ulioongeza mashaka kua huenda kwel Dr.George ndie aliyekua mhusika mkuu katika mauaji hayo.Miaka takriban kumi na tano kabla ya tukio lile Dr .George alikua amenunua nyumba Hollywood.Nyumba hii inadhaniwa kuwa huenda ndimo mauaji yale yalikua yametendeka.Ushahidi uliokusanywa na baadhi ya wapelelezi kwa msaada wa mbwa maalum wa kutambua harufu ya binadamu pamoja na wataalamu wa uchunguzi wa maswala ya uharifu kupitia sayansi maarufu kama(forensic science) ulidhibitisha kua mauaji yalitokea eneo lile.
Ikumbukwe kwamba George Hodel alikua ni daktari mwenye ujuzi wa hali ya juu hali iliyoongeza mashaka kwani mwili wa Elizabeth Short ulikutwa ukiwa umekatwa kitaalamu zaidi.Hii ilionesha kua mtu aliyekeleza mauaji yale alikua na ujuzi kuhusiana na mambo ya upasuaji.
lakini mnamo mwaka 1945 Dr.George alimuua aliyekua sekretari wake bi Ruth Spaulding kwa kumwekea madawa yenye sumu kali.Inadiwa kwamba bi Ruth alikua na taarifa mhimu juu ya vitendo viovu alivyokua akivitekeleza Dr.George juu ya wagonjwa katika hospitali yake kama kuwaandikia magonjwa ambayo hawakua nayo kisha kuwaibia pesa zao kwa kigezo cha kuwatibu pia inadiwa kua alikua akijihusisha na vitendo vya utoaji mimba.Dr George Hodel alitoroka kutoka nchini marekani baada ya kupata taarifa kua luteni Jemmison aliyekua akifatilia kesi yake ya mauaji ya Ruth alikua na ushahidi wa kutosha kumkamata mpaka alipofikwa na umauti mwaka 1999.
Kutokana na mfululizo wa matukio kama nilivoeleza hapo juu ni dhahiri kabisa kua huenda ni kweli Dr.George alikua ndie mhusika mkuu katika mauaji yale.Lakini pia baadhi ya ushahid uliopatikana ulimuhusisha Dr.George Hodel katika mauaji mengine mengi ya kutisha baadhi ya mauaji hayo nitajaribu kuyaelezea kwa kadiri ya vyanzo mbalimbali.
1.Mauaji ya Chicago(Chicago lipstick murder) Januari 6, 1946, Chicago, Illinois
Katika mauaji hayo mtoto aliyetambulika kwa jina la Suzanne Degnan mwenye umri wa miaka 6 alitekwa na watu wasiojulikana akiwa karibu na nyumbani kwao, mtoto huyo alichukuliwa kutoka nyumbani kwao na kuuawa katika ghorofa ya karibu ambayo wapelelezi waliipa jina maarufu kama "chumba cha mauaji."Siku chache baadae mwili wake ulikutwa katika mabomba ya maji machafu ukiwa umetenganishwa kwa namna ileile iliyofanana na jinsi mwili wa black dahlia ulivyokua umepasuliwa.
2.Mauaji ya Jigsaw (Jigsaw murder) Mei 28, 1967, Manila, Philippines
Mwanamke aliyetambuliwa kawa jina la Lucila Lalu aliyekuwa na umri wa miaka 28 alitekwa nyara akiwa katika sehemu yake ya biashara huko Metropolitan Manila mnamo tarehe 28-5-1967.Mwili wake ulipatikana siku chache baadae ukiwa nao umepasuliwa vilevile kama ilivyokua imepasuliwa miili ya Black Dahlia na mtoto Suzzan.Mwili wake uliokotwa katika maeneo ya wazi karibu na barabara inayoitwa Epitsanzo De Los Santos karibu na mtaa unaojulikana kwa jina la ZODIAC.Mauaji yaliyotokea katika mtaa huo wa zodiac ndiyo yaliyoibua mashaka miongon mwa watu kuwa mtekelezaji wa mauaji yale alikua ndiye muuaji maarufu wa wakat ule(Zodiac Killer).
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali kuna matukio mengi sana ya mauaji ambayo yanadhaniwa kuwa mtekelezaji wa mauaji yale alikua Dr.George Hodel.Pamoja na kuhusishwa na mauaji yote hayo hakukuwahi kuwa na ushahidi wa kutosha kumkamata zaidi ya ushahidi uliokusanywa katika kesi ya mauaji ya sekretari wake Bi.Ruthi ambapo hata ivyo hawakufanikiwa kumkamata kwani alitoroka kutoka nchini Marekani na kukimbilia kusikojulikana mpaka alipofikwa na umauti mwaka 1999.
Hivyo basi kesi hii ya Black Dahlia inabaki kuwa moja kati ya kesi zilizowahi kuwasumbua sana FBI na kuacha maswali mengi ambayo hayajapatiwa majibu mpaka leo.Baadhi ya maswali muhim ya kujiuliza ni nani alitekeleza mauaji yale na kwanini na kama kweli Dr George Hodel alihisika katika mauaji yale ilikuaje mpaka wakashindwa kumkamata au kulikua na watu waliomsapoti nyuma!!!!????
 
alitorokea kusikojulikana, na je? pia alifia kusikojulikana?
 
Sasa kwanini usingeendelezea kwenye uzi ule?

Unatuchanganya
 
images-10.jpg
 
Back
Top Bottom