Black Soldier Fly Larvae(BSFL) kama Protein mbadala

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Posts
7,872
Reaction score
9,263
Black Soldier Fly au nzi chuma ni aina ya nzi ambao ni wa mwituni na hutumika sana kuzalisha larave au funza kwa ajili ya mifugo.

Commercial Production ya larave hawa inawezekana sana Tanzania kwa sababu kuna watu tiyari hasa Wazungu wanaifanya, tena wako funded kabisa na mmoja wao alipata fund mara baada ya Watanzania kuona ni kinyaaa.

Ila ili uzalishe Commercial lazima uzingatoe mambo yafuatayo,

1. Uhakika wa Organic waste au Uchafu hai wa kuwalisha hao larvae
2. Means za kuutoa huo uchafu kule uliko na kuuleta eneo la Production.

Hivyo ndo vitu muhimu sana vingine ni minor sana kama swala la wafanya kazi, na stracture.

BSFL wana kiwango kikubwa sana cha protein, Fat na Calcium kiasi kwba unapo itumia kwenye kuzalisha chakula cha mifugo basi huna haja ya kuongeza mashudu ya alzet au pamba, na pia vitu kama chokaaa kwa ajili ya calcium.

Hawa larvae wanaweza tumika na almost mifugo yoye.
-Kuku
-Samaki
-Nguruwe
-Ng'ombe

na pett animal kama mbwa na paka, Mbwa anapenda mno larave walio kaushwa na kuna mzungu Arusha tiyari anazalisha Biscut za mbwa kwa kitumia hawa Larvae.

BSFL ni Mbadala wa Soya na Dagaaa na Samaki kwenye uzalishaji wa vyakula vya mifugo hasa Kuku, Nguruwe na Samaki,

Pia anaweza tumika kama full chakula ingawa ana kosa Carbohydrate tu.

Wazungu wanachangamkia sana hii ishu huku kwetu ilihali sisi tumelala tuna subilia Waziri atutangazie kwamba tuzalishe.

Pia sio lazima Uzalishe commercial unaweza zalisha ukalishia mifugo yako mwenyewe ka Kuku, Samaki, Nguruwe na Ng'ombe na Mbwa wako na Paka

 
Kama huna Source ya Organic Waste ni vigumu sana kuzalisha hawa larvae.
 
Kama huna Source ya Organic Waste ni vigumu sana kuzalisha hawa larvae.
Nina mbolea ya nguruwe tani 2 kila siku shamba lipo kilolo Panafaa? na je temperature ya huko ni sahihi? niambie mbegu mayai napataje in c0mmercial scale?
 
Nina mbolea ya nguruwe tani 2 kila siku shamba lipo kilolo Panafaa? na je temperature ya huko ni sahihi? niambie mbegu mayai napataje in c0mmercial scale?
Yes wanaweza kula Mbolea ya nguruwe fresh na unawachanganyia na pumba kiasi huko ni cheap najua.

Majira magumu huwa ni kipindi cha mwezi wa 5 hadi 6 ambako jua linakuwa halitoki, Baridi sio ishu ila mwanga ndo ishu kubwa kwao hasa BSF kwa sababu kwenye mwanga ndo wanafanya Mating
 
Nawapataje ? Nimewasoma juz juz hapo ila naona Kenya na uganda wanawafaid sana bado hapa nyumban
 
Wekeni orodha ya wauzaji wote wa hii mifugo na wanalisha mifugo yao hawa funza.

Ni kwaajili ya kuchagua sehemu yenye nyama yenye protin ya uhakika.
 
Kuna sehemu nilishuhudia wakizalishwa mwaka jana na walikuwa wanachukuliwa machinjioni. Sina uhakika kama ile project inaendelea. ila ni source nzuri ya protini.
 
Kuna sehemu nilishuhudia wakizalishwa mwaka jana na walikuwa wanachukuliwa machinjioni..............sina uhakika kama ile project inaendelea. ila ni source nzuri ya protini.
Unazungumzia Magot wale funza wa nzi, mkuu BSFL hawa wanafugwa sio kwamba wanazaliana tu mtaani hovyo
 
Mkuu naomba nije pm tuelekezane namna ya kupata mbegu ya hawa BSF
 

Naomba number ya mzalishaji
 
Hii kitu ni nzuri sana hasa ukiwa unalishia mifugo yako, yaani gharama utaziona ni ndogo sana na asikuambia mtu gharama za kulisha mifugo ndo changamoto kwenye ufugaji
 
Kuna wazungu wanafanya Tanzania mmoja nilikutana nayr Nane nane, wanazalisha sana na yule wa Arusha nasikia ana mkataba wa kuwauzia Intetchick larvae walio kaushwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…