mkorinto,
Hata siyo steve jobs maana idea ya kutengeneza simu hakuletewa yeye na alipoletewa aliikataa, yeye alisema kwanini watengeneze simu wakati wana ipod inafanya poa, kitu kilichomfanya awe interested na simu ni pale alipoona mdada flani mfanyakazi wa pale apple akitumia touch pad kutumia computer kwakuwa alikuwa na tatizo la vidole kilikuwa kimeumia, akatoka hapo akampa kazi jamaa mtaalamu wa touch screen amtengenezee touch screen yenye list ya vitu,
jamaa alipoitengeneze na kuiandikia code wakati ana scroll ilipofika mwisho ika bounce, ile string effect ya ios, jamaa akahisi kuna error kwenye code lakini akaiacha, hilo la string effectt ndilo lilimgusa sana steve baada ya kupewa hiyo kitu... ni long story mpaka iphone inaingia sokoni.
Hata siku ya launchia simu haikuwa tayari maengineer wakati jobs ana present walikuwa wanajikunyata wakihis muda wowote itabuma, halafu jobs alivyokuwa mshenzi, akasema mfano ukitaka kufuta contact unaenda hapa unafuta akafuta majina mawili kwenye simu, kwa waliokuwepo mle walihisi anawaonyesha tu ila kwa wafanyakazi wa apple maana yake wale aliyowafuta walikuwa fired hapo...