Blatter aipongeza Yanga

Blatter aipongeza Yanga

Mapengo 17

R I P
Joined
Mar 28, 2014
Posts
1,229
Reaction score
610
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu DunianI - FIFA, Joseph Blatter ametuma salamau za pongezi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, Jamal Malinzi kufuatia klabu ya Young Africans kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2014/2015.

Katika salamu hizo za Blatter, amemuomba Rais wa TFF kufikisha salamu zake za pongezi kwa klabu ya Young Africans, wanachama, wapenzi wa mpira wa miguu kwa kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi mwakani katika michuano ya kimataifa barani Afrika.

Blatter amesema anatambua mafanikio hayo ya kutwaa Ubingwa, yametokana na na jitihada za uongozi, wachezaji, bechi la ufundi, madaktari, wanachama , washabiki na kila mmoja aliyeshiriki katika kufanikisha kutwaa Ubingwa huo.

Mpira wa miguu unapata mafanikio makubwa kwa kuvuka mipaka hadi kuwa kichochezi halisi cha maendeleo, unawasaidia wachezaji wa ngazi zote kuinua vipaji vyao na mbinu katika kuelekezwa na kubadilika wakati huo huo wakiwa wakiwa na nyoyo za ushirikiano.

Aidha Blatter amesema mpira wa miguu kwa sasa ni shule kwa maisha, vijana wa leo wanaweza kufaidika kupitia kucheza mpira wa miguu kwa ngazi ya kijamii na mtu mwneyewe binafsi, ndio maana amewapa salamu za pongezi Young Africans na kuendeleza kazi yao na kuongoza njia ya mafanikio.

Kujituma kwa klabu ya Young Africans kumewasaidia kushinda Ubingwa huu ikiwa ni ni mara ya 25, huu ni ushindi mkubwa katika mpira wa miguu.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
 
Naam, leo ukiwa Yanga rahaaaa, Simba wanashangilia yanga leo, hawana jinsi!!
 
Ha ha ha ha.. Nilidhani kwa kufungwa goli moja tu watunisia lol.. Sefu Abdallah ni bingwa wa fitina..
 
Pongezi kwa Mapinduzi Cup hamna au FIFA hawalitambui?
 
Blatter anaijua Yanga jaman mbona mbwembwe wanajangwan
 
Homa ya uchaguzi wa FIFA inamsumbua Blatter,aache blah blah zake tumemchoka
 
Hizo ni kampeni tu za kujiweka karibu na wapigakura wake wakubwa kwa maana ya nchi za Afrika katika uchaguzi anaokabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Luis Figo; kama ni ubingwa Yanga wamekuwa mabingwa wa Tz mara nyingi yeye akiwa Rais wa FIFA na hakuwahi kutuma pongezi, iweje leo!!! Blatter ni kiongozi aina ya Nkuruzinza, Mugabe, Kagame, Hayatou.
 
mtuma post mwenyewe anaitwa mapengo ana mapengo kwenye ubongo wake. yaan hili nalo la kuzungumzia? blatter na ligi ya bongo seriously anifatilia? aaaahh jaman tuwe wakati mwingne tunatumia ubongo hata kidogo.tusiulaze sana
 
Sishabikii yanga hata iweje.

raha yake ni kwamba unune ufurahi sie furaha yetu iko pale paleeeeeee

tukiwafunga Azam ndugu zenu rahaaaaaaaa kwetuuu
tukifungwa na Azam pia rahaaaaa..... maana wale mnaotaka kupanda ndege kwa huruma ya Yanga hamtapanda...

Leo ni siku ambayo inabidi tu ushangilie yanga... usiufanye moyo wako kuwa mgumu, sikia leo mkuu


karibu Yanga
 
mtuma post mwenyewe anaitwa mapengo ana mapengo kwenye ubongo wake. yaan hili nalo la kuzungumzia? blatter na ligi ya bongo seriously anifatilia? aaaahh jaman tuwe wakati mwingne tunatumia ubongo hata kidogo.tusiulaze sana

Wewe ni kuku tu!
 
Back
Top Bottom