Blinken uso kwa uso na Lavrov pembezoni mwa mkutano wa G20

Blinken uso kwa uso na Lavrov pembezoni mwa mkutano wa G20

HERY HERNHO

Senior Member
Joined
Mar 4, 2022
Posts
110
Reaction score
458
Wanadiplomasia wa Marekani na Urusi wamezungumza kwa ufupi pembezoni mwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya kigeni kutoka kundi la nchi 20 zilizopiga hatua kiviwanda G20, mkutano ulioshindwa kutoka na tamko la pamoja.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov wamezungumza kwa ufupi pembezoni mwa mkutano wa wanadiplomasia wa nchi za G20 mjini New Delhi, uliogubikwa na vita vya Ukraine na ambao umeshindwa kufikia tamko la pamoja baada ya pingamizi kutoka Moscow na Beijing.

Amesisitiza dhamira ya Washington ya kumlinda mshirika wake Ukraine ili kuondoa dhana yoyote ya Urusi kwamba Washington inaweza kuyumba katika uungaji wake mkono. Hadi kufikia leo, hapakuwa na mawasiliano ya ana kwa ana baina ya serikali ya Marekani na Urusi tangu Moscow ilipoivamia Ukraine mwaka jana, huku Washington ikisisitiza usaidizi wake kwa Kyiv na kuhimiza juhudi za kimataifa za kuitenga Urusi.

Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Urusi Maria Zakharova, aliyelieleza shirika la habari la serikali RIA Novosti, ni kwamba Blinken ndiye aliyeanzisha mazungumzo hayo lakini kwa ufupi sana, baadhi ya ripoti zikisema yalikuwa chini ya dakika 10.

Waziri Lavrov amenukuliwa akisema kwamba kundi la nchi za G20 halitotoa tamko la pamojahuku mwenyeji wa mkutano.

64865986_803.jpg


Huo ambayo ni India ikitoa tu muhtasari wa mkutano. Lavrov aliwaambia mawaziri wa mambo ya nje waliokusanyika kuwa wawakilishi wa nchi za Magharibi wamevuruga mkutano huo kwa nia ya kuikosoa Urusi kwa kushindwa kwao wenyewe, na kutoheshimu juhudi za mwenyeji India kufikia makubaliano juu ya masuala mengine. Lavrov anaongeza kwamba.

Indien G20-Treffen in Delhi | Lawrow
 
Hao warusi watengwe kabisa hawana staha.
 
Yaani Urusi ni Dude kubwa sana

Hao Jamaa kila wanapo kutana Wao ni Urusi tu.

Nasio kuwa Wanaipenda Hiyo Ukrein Kama tunavyo Danganywa.

Hii dunia Inahitaji Balance sana Bila hivyo Tutafanyiwa Kila Aina Ya Mateso
MUNGU IBARIKI URUSI
 
Tuanze kuwatenga walivamia Iraq, Libya, Afriganstan then tuamie walivamia Palestina alafu tumalizue na Urusi
Palestina nilikuwa nawaonea huruma sana, ila baada ya kujua hawa waliojiotolea kumsaisaidia Idd Amin kwenye vita dhidi ya Tanzania tena kwa sababu za kidini, sina huruma nao, Israeli awafagie kabisa.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Washenzi sana hawa, wanaposema dunia wanamaanisha eti wao Westerners tu. Africa, Asia, Far East na South America sisi hatupo katika hiyo dunia wanayoiongelea hapo
Sisi wenyewe tunakimbilia kwao nchi zetu zimetushinda Kila wiki mnazama Mediterranean sea wengi ni from Asia and Africa [emoji25][emoji25]
 
Back
Top Bottom