BLOCK 89 Wasafi FM

princemikazo

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2019
Posts
2,195
Reaction score
2,056
Wasalaam wadau poleni na mfungo kwa wale ndugu zangu waislam chungu cha ngapi Leo??anyway acha niende moja kwa moja kwenye nia,Kuna kipindi kipya Pale usafini FM redio kinaanza Saa mbili usiku sijui hadi saa ngapi!?Kikiongozwa na Jonijoo Babaako akiwa na Calypso,Aaliyah na Mtu imara,bila kuwasahau ma'Djs wao DJ Vasley na DJ Jaco,,kipindi kipo fresh ila sidhani kama Mtu imara anastahili kuwa pale coz haendani na wenzake(No chemistry) pia ni mkimya sana sometimes audience wanatuma comment wakiuliza mbona yeye haongei?alaf jambo lingine Nafikiri kingewekwa mchana kipambane na XXL,Planet Bongo,Show Time New chapter,ingekua poa sana,,,Hizo ni kasoro nilizoziona kuhusu iki kipindi cha Block89 Wasafi FM,,Lakini niwapongeze wameleta utofauti wa kuruka Live YouTube mwanzo mwisho....Yangu hayo ariff.




@ChaliiYaKijengeJuu.
 
Kuhusu mchana sikubaliani nawewe,hiki kipindi trust me kina bamba usku,mana maniga ndio tunakua free

Kuhusu huyo jamaa ni kwel kapoa sana..ila akiamuaga kuzingua anakuaga poa tu..

Weakness mi naona ni kuleta wasanii kila siku,,naona watawamalza mapema mwisho waanze kuwarudia..wangetenga hata siku tatu tu kwa wiki ndio siku za kuwa na wasanii..sema nini jamaa wana studio kali sana
 
Mda waliochagua upo sahii kabisa 100%,ila ndio mwanza kimeanza,bado wanajifunza,bado ni wapya mwisho wa siku kama wakiendelea kujifunza na kujituma zaidi katika kuandaa contents zao watakuwa vizuri.
 
hauoni kuwa muda kimewekwa ndio mzuri maana hakuna mshindani, halafu, kitafaa sana kwa wale ndugu zetu wa bunju, muda huo huwa wana foleni za usiku kurudi kwao mwisho wa dunia, basi kumbe, kipindi hiko cha club 89 kinawafaa sana kukisikiliza kwenye foleni
 
Hivi mtu aliefunga yampasa kupewa pole ama hongera? Au mimi ndio sijui haya mambo?
 
producer wa hicho kipindi achukue huu ushauri. >>>>> kwanza hawapeani nafasi kwenye kuuliza maswali mgeni akitaka kujibu anakatishwa na swali jingine, very unprofessional! alafu hayo maswali yao hayana ushawishi wa mtu kusikiliza zaidi pia hayamfanyi mgeni kufikiria marambili mbili kwenye kujibu. Maswali yao hayana utafiti ndani yake sometimes wanaweza wakamuuliza mgeni kitu alafu mgeni akawasahihisha kua sio hivyo bali ni hivi.. pia kwenye hayo maswali yao kuna mengine yanamfanya source apatwe na jazba ila basi tu anavumilia, maswali hawayaweki kwa mpangilio from malaini to magumu to malaini. Kipindi kinaendeshwa na mihemko makelele mengi content 0. waache kuigana. Hawaendi na muda inapaswa ikifika saa tano kamili show is over ili watanzania tulale sasa utakuta wanapitiliza kwa vitu visivyoeleweka very unprofessional. Wanapaswa kutenga dakika hata 2 tu za kusoma messages za raia tu sio wanataja social media zao alafu wanamaliza kimya kimya hata kusikia maswali yenye content kutoka kwa raia. Kabla hawajamuita mgeni wafanye research kwanza tena kweli kweli sio kufreestyle tu On air its very unprofessional.

MWISHO uchezeshaji wa jingles ni mbovu sanaaaa, jingles hawazipi nafasi hata sekunde kadhaa kwa sekunde kadhaa. mtu unaburudika na mziki mara utaskia ndani ya sekunde moja jingles 5! very unprofessional wajifunze kwa east africa radio na clouds jamaa kwenye muziki jingels ni moja au mbili tu na zinapikwa kwa wakati maalumu sio hovyo hovyo hadi kumboa msikilizaji.
 
Ni muda mzuri Sana,kuna demu mmoja Hivi mweusi anakiele else Sana.
 
Daah bonge moja la ushauri chaliangu,nna imani wapo humu ndichi so ni vizuri waufanyie kazi ,Nakumbuka interview ya Lady Jay Dee walimtoa machozi hadi mala mbili bado wanarudia maswali yale yale ya kumliza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…