Bloga wa Kenya ashitakiwa kwa kusambaza taarifa za uongo kuhusu COVID-19

Bloga wa Kenya ashitakiwa kwa kusambaza taarifa za uongo kuhusu COVID-19

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
Alai.png

Robert Alai
Mwanablogu wa nchini Kenya Bwana Robert Alai amefikishwa mahakamani kwa kusambaza ujumbe kupitia mtandao wa Twitter akidai serikali ya nchi hiyo imekuwa ikificha taarifa kuhusu vifo vinavyohusiana na Coronavirus huko jijini Mombasa.

Bw. Alai alikamatwa Ijumaa baada ya ujumbe huo uliozusha taharuki, huku serikali ya Kenya ikitoa onyo dhidi ya kueneza habari zisizo na ukweli na za kupotosha juu ya mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19.

Akiwa mbele ya Hakimu Muema Ndungi, Bw. Alai alishtakiwa kwa kuchapisha habari ya uongo ikiwa ni kinyume na kifungu cha 23 cha matumizi mabaya ya kompyuta na kitendo cha uhalifu wa mtandao.

=======

Controversial blogger Robert Alai has been arraigned at the Milimani Law Courts for posting a tweet claiming that the government was hiding information about coronavirus related deaths in Mombasa.

Alai was arrested on Friday after the alarming tweet that came on the backdrop of a stern warning from the government cautioning the public against spreading unverified and misleading information on COVID-19.

Appearing before Magistrate Muema Ndungi, the blogger was charged with publication of false information contrary to Section 23 of the computer misuse and cybercrimes act.

“On the 19th day of March 2020 at an unknown place within the Republic of Kenya, posted on your twitter account @RobertAlai to wit “Coronavirus: Is the Kenyan government hiding COVID-19 related deaths at the Port of Mombasa” knowing it to be false and calculated to cause panic and fears among citizens of the Republic of Kenya,” stated the charge sheet.

He denied the charge and was released on a Ksh.50,000 cash bail or bond of Ksh.150,000 and directed to provide one contact person.

The case will be mentioned on April 23, 2020.

President Uhuru Kenyatta chaired a Cabinet meeting at State House, Nairobi on Thursday where it was directed that law enforcement agencies to pursue and arrest individuals spreading false information on the disease.

Source: Citizen TV

Taifa la kwanza duniani kwa kulinda uhuru wa wanahabari.
 
Hiki kitu ni hatari sana, tujiepushe kueneza habari za uwongo, jana pia nimeona watu wanaeneza taarifa mtaa fulani karibu na kwangu hapa eti kuna mtu amefariki kutokana na huu ugonjwa.
Tutoe ushirikiano kwa serikali, kuna naibu gavana anasubiriwa apone kisha ashtakiwe kwa uzembe wake wa kutokufuata maagizo. Nimeona jana mtaani kuna baadhi ya daladala hazifuati maagizo ya kuhakikisha abiria wana nawa mikono kabla ya kuingia.
Huu uzembe utasababisha wengi tuambukizwe hiki kirusi. Waziri wa afya na rais wetu wanajitahidi sana kutoa taarifa na maelekezo ya kuhusu hiki kitu, tuwape ushirikiano.
Tujiepushe pia mizunguko ya hovyoo, wale wenye kazi zinazowaruhusu kufanyia nyumbani wabaki ndani tu, mimi kwa wiki zijazo kadhaa nafanyia kazi zangu zote nyumbani, nje nitatoka tu wakati nakwenda mazoezi ya kukimbia, na hata hiyo nitakimbia maeneo ya Karura forest ambapo hamna watu wengi.
Wanangu wote ndani, nimeunga vifurushi vya Showmax na kuwapa access halafu internet yenyewe ya Zuku ya MBs bila kikomo.
 
Hapa tunakukamata kwa kueneza uongo sio Kama bongo kwenye wanafanya the opposite.
Ccm wanaeneza data za uongo e.g. sgr, uchumi, uongo etc.. ukipinga kwa ukweli unapigwa risasi Kama lissu au kufungwa Kama zitto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiki kitu ni hatari sana, tujiepushe kueneza habari za uwongo, jana pia nimeona watu wanaeneza taarifa mtaa fulani karibu na kwangu hapa eti kuna mtu amefariki kutokana na huu ugonjwa.
Tutoe ushirikiano kwa serikali, kuna naibu gavana anasubiriwa apone kisha ashtakiwe kwa uzembe wake wa kutokufuata maagizo. Nimeona jana mtaani kuna baadhi ya daladala hazifuati maagizo ya kuhakikisha abiria wana nawa mikono kabla ya kuingia.
Huu uzembe utasababisha wengi tuambukizwe hiki kirusi. Waziri wa afya na rais wetu wanajitahidi sana kutoa taarifa na maelekezo ya kuhusu hiki kitu, tuwape ushirikiano.
Tujiepushe pia mizunguko ya hovyoo, wale wenye kazi zinazowaruhusu kufanyia nyumbani wabaki ndani tu, mimi kwa wiki zijazo kadhaa nafanyia kazi zangu zote nyumbani, nje nitatoka tu wakati nakwenda mazoezi ya kukimbia, na hata hiyo nitakimbia maeneo ya Karura forest ambapo hamna watu wengi.
Wanangu wote ndani, nimeunga vifurushi vya Showmax na kuwapa access halafu internet yenyewe ya Zuku ya MBs bila kikomo.
Nakuunga mkono,ila ingekua Tanzania ungekuja na thread kama 100 hivi,za uhuru wa kujieleza,katiba ya kenya na uchumi wa kati
 
Nakuunga mkono,ila ingekua Tanzania ungekuja na thread kama 100 hivi,za uhuru wa kujieleza,katiba ya kenya na uchumi wa kati

Kueneza uwongo sio kujieleza, Tanzania huko mnakamata mtu kisa amepiga picha inayo onyesha barabara mbovu.
 
Kueneza uwongo sio kujieleza, Tanzania huko mnakamata mtu kisa amepiga picha inayo onyesha barabara mbovu.
Inategemea na.barabara ya kwenda wapi
Tupo kwenye vita yakuchumi,unapiga vita barabara mbovu inayotumiwa nawatalii,maana yake ni kwamba watalii wakiiona wasije,waende kwingine
 
Inategemea na.barabara ya kwenda wapi
Tupo kwenye vita yakuchumi,unapiga vita barabara mbovu inayotumiwa nawatalii,maana yake ni kwamba watalii wakiiona wasije,waende kwingine

Huko kwenu balaa, mumekua kama Kore Kaskazini, si kuna siku mlimkamata mwanafunzi kisa amepiga picha kuonyesha nyufa kwenye ukuta wa chuo.

MWANAFUNZI ALIYEPIGA PICHA HOSTEL ZENYE NYUFA UDSM AKAMATWA

WhatsApp%2BImage%2B2017-12-03%2Bat%2B09.02.02.jpeg

Post Zake kijana huyo kwenye mtandao wake wa Facebook hizi hapa

Andiko la kwanza kabisa

“Nimetoka New Hostel (Magufuli Hostel), Hosteli ambazo rais wetu amepigania mpaka zikajengwa kwa Shilingi Bilioni 10 tu za Kitanzania.

Ni Ajabu sana, Huenda hizi zikawa ni hosteli zilizojengwa kwa kiwango cha chini kuliko hosteli zote barani Afrika…. Nitawaletea picha hapa siku ya kesho au ikiwezakana baadaye…… Mtatoa machozi.

Hatupo Salama…… Naomba msinipige risasi mpaka nitoe ushahidi.

NB:
Hosteli hizi zimejengwa kwa Bilioni 10 tu”

#Bilioni10Tu.

“#JOHN_POMBE_MAGUFULI_HOSTEL.

Ikiwa ni takriban ya Wiki nne tu toka hosteli hizi kuanza kukaliwa na Wanafunzi hatimaye Nyufa kubwa na za kushangaza zimenza kujitokeza kwenye mojawapo ya
Majengo haya alimaarufu kama JOHN POMBE MAGUFULI HOSTEL.

Hosteli hizi zilizinduliwa na Mh. Rais mwanzoni mwa mwaka huu na zimeanza kukaliwa Mwezi wa 11 mwaka huu.

Ajabu ni kuwa nyufa zimezidi kuota kwenye mojawapo ya majengo haya. Hosteli hizi zimebeba takribani ya Wanafunzi 3840.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli alidai kuwa majengo haya yalijengwa kwa bilioni 10 tu za kitanzania ingawa takwimu za Mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali yaani CAG waliweza kubaini kuwa majengo haya yalijengwa kwa Sh. Bilioni 54 … Majengo haya kujengwa kwake yametumia miezi Sita tu kukamilika kwake.. Taarifa za awali zinadai kuwa hosteli hizi huenda zikawa ni mojawapo ya Hosteli zilizojengwa kwa kiwango cha chini kuliko Hostel zozote Barani Afrika.

Pichani ni MAGUFULI HOSTEL.
Andika #Bilioni10 Kwa kilugha chako….. Twende kazi.”

Andiko la Pili

MAJIBU YANGU KWA TBA.

Masaa matatu yaliyopita nilichapisha andiko langu hapa kwenye ukarasa wa Facebook nikielezea Jengo la Hostel lililojengwa kwa hisani ya Rais wetu mpendwa John Pombe Magufuli nikielezea kuwa yamepata nyufa.

Ofisa Mtendaji mkuu wa TBA bwana Elias Mwakalinga ameliambia Mwananchi kuwa anajiandaa kwenda kuangalia kama ni kweli, akaenda mbele zaidi na kusema kuwa huenda kuwa hosteli hizo ni za majengo mengine zimehusishwa na majengo mengine.

Nimuombe Mkurugenzi wa TBA Mh. Elias Mwakalinga kuwa sijafananisha na majengo mengine na picha hizo ni za kweli na nimepiga mwenyewe.

Nendeni Hostel Block A, nitafuteni niwasadie kuwaonyesha nyufa zilipo.

Naomba niongezee kuwa tatizo sio hilo tu, tutafutane tuwaambie na matatizo mengine.

Tunawakoa ili kuwasaidia, msituone maadui na kutafuta visingizio vingine eti majengo yatakuwa sio yenyewe….
MWANAFUNZI ALIYEPIGA PICHA HOSTEL ZENYE NYUFA UDSM AKAMATWA – Habari Mpya za Leo

http://www.mwananchi.co.tz/…/1597578-4213244-7p1…/index.html
 
Back
Top Bottom