Bloggers waendeleza kejeli kwa Rais Kikwete


Who is this little guy?
 

"Uhuru usio na mipaka ni wendawamizmu" (JKN)
 
Mkuu wala usipate tabu kuna watu simply hawana adabu...hawajuwi kuongea kistaarabu, hata Brown anakosolewa na watu wake lakini watu wanachunga heshima siyo!!
 
Du mnaonaje kama tutakuwa tunatumia lugha yetu ya Taifa tu kutoa hoja zetu humu ndani?. Manake vi-inglishi vingine humu ndani ni aibu tupu.
 

Rais akianza kujidhalilisha mwenyewe watu wakae kimya kikondoo? Kama ukweli ni kwamba rais anajidhalilisha na observer yeyote atakayesema kweli ataonekana anamdhalilisha wasema ukweli waogope kusema ukweli?

Rais akitinga mkutanoni mtupu wa nyama tumsifie kwamba suti yake imempendeza?

Rais akijikojolea hadharani tumwambie hayo maliwato yanayochuruzika yananukia vizuri?
 
Mpendwa Pasco,
asante kwa ufafanuzi murua.
Na hiyo 2010 JK atashinda kwa kishindo na ataendelea kutawala hadi 2015.
Stay blessed.
UNGEMALIZIA KWA KUANDIKA ATAENDELEA KUTAWALA KWA MABAVU NA KWA WIZI WA KURA ZADI 2015. shame on Him.!!! Sijawahi sikia Rais au Mfalme yoyote Duniani aliye shindwa kuongoza nchi yake kama Rais wetu.! Ukweli utabaki pale pale..!
 
Simple math: Kikwete alipata kura milioni 9, idadi ya Watanzania wakati huo ilikuwa milioni 35. Hivyo alichaguliwa na 26% ya Watanzania wote na sio 80%.

Habari ndiyo hiyo.

.
 
hilo nalo neno!
 
Anaye kejeli wenzie ni kikwete kwa sababu anaambiwa lakini yeye kimya tu huku nchi ikiyumba
 

Ukistaajabu ya Mussa!...Na yeye anavyoidhalilisha nchi yetu inakuwa kama haina sheria kwa kuacha Mafisadi watambe hadharani bila hata ya woga nani atamhukumu!? Si umewaona mafisadi akina Rostam, Vijisenti na wengineo wakitamba hadharani pamoja na kuwa Kikwete ana madaraka makubwa kama Rais wa nchi hadi hii leo hajachukua hatua yoyote dhidi ya mafisadi hawa na wengineo. Je, nani atamuhukumu Kikwete!?
 

Waswahili hawakukosea waliposema "ukicheka na nyani utavuna mabua"....huyu rais apewe heshima kwa kitu gani? Kwa kuhalalisha ufisadi au? Akifanya jema tutamsifia, akiboronga tutamnanga! Tukiendelea kucheka naye bila kuchukua hatua, basi nchi itakuwa matatani
 
JF ingekuwa inawakilisha hata 1% ya mawazo ya Wadanganyika ningefurahi sana. Bahati mbaya nilipokwenda Tanzania baada ya miaka kadhaa ya kusoma na kuburudika na michango ya JF nikiwa ughaibuni nilikuta hadidhi ni tofauti kabisa. Yaani nilikaribia kuzirai; nilichoka kabisa! Jamaa bado watanzania wengi wanamuona kama nabii! Na ukweli ni kwamba (japo unauma) 2010 jamaa atashinda kwa zaidi ya asilimia 75%! Ukweli ndio huo!

Ushauri wa bure: JF tujaribu kuandika kwa ku-reflect a lil bit on what is taking place on the ground! From there tunaweza kubadilisha fikra za watu wengi. Lakini kwa sasa tuko sayari ya pluto huku tunataka kubadili upepo ndani ya mercury!
 

Kama unachozugumza ni sawa basi 'Habari ndiyo hiyo' hakuwa na haja ya kuleta habari yake hii,maana ni wachache tu wanaotumia hii mitandao kwa mtazamo wako. Lakini huwa kuna kuambukiza habari. Akijua mmoja nyuma yake kuna wasiopungua watano wanaojua. Na kuna wengine wana mitandao mipana zaidi.

Kimsingi habari hii ya 'Habari ndiyo hiyo' haimsadii huyo anayedhamiria kumsaidia-JK. Alichofanya ni sawa na kuwatangazia watanzani kuwa Mfalme ana pembe yaani hata waliokuwa hawajui hiyo mitandao na namna mzee wa kaya alivyo kiuhalisia basi waanze kuitafuta na kujua.Sasa badala ya kuficha aibu ya mzee unaitangaza zaidi. Kwa hivyo wengi watajua kumbe mzee wa kaya anakilema- anapembe, si mzuri kama alivyokuwa akitangazwa au kujitangaza.
 

Wakuu ,
hawa watu wanaozungumzia 80% naona hawakumbuki kiapo alichoapishwa kuwa Raisi. Sasa hata kama alishinda kwa 80% lakini kama hatekelezi yale aliyoahidi kutekeleza kwa kiapo ....?????????? the 80% turns upside down!!!
 
When someone claims to be insulted when you tell the truth, you should know that you have delivered your message. Waswahili wanasema Ukweli unauma.
So badala ya kulalama HABARI NDIYOHIYO, utafute muda ukae na rais wako na umweleze ukweli kuwa siyo kejeli wala matusi bali ni maoni na mtazamo wa wananchi, na kama kiongozi hawezi kupuuza maoni ya wapiga kura wake. Yeye ni mtumishi wa umma, ni mtumishi wa wananchi wote, siyo bosi wetu au mfalme wetu. The last shall be the first and the first shall be the last. He has been put in office to SERVE us!
 
JF ni watu Mungu aliowabariki na kuwa na uwezo wa kupata mkate wa kila siku, na wengi wao wapo nje ya nchi maana hapa TZ internet access ni shida isipokuwa mpaka ofisini. Kwahiyo hawana direct impact.

Ila magazeti yanatembelea humu kwahiyo wanatusaidia kidogo kuwafikishia wa TZ ujumbe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…