BMK: Uwazi au Usiri = siku 18; jee 2 au 3 itakuwa siku ngapi? Inafurahisha.

BMK: Uwazi au Usiri = siku 18; jee 2 au 3 itakuwa siku ngapi? Inafurahisha.

Dr Akili

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2011
Posts
5,119
Reaction score
4,569
Kuamua 'wazi au siri' bunge letu maalum limechukua wiki 3
Jee kuamua seriali 2 au 3 litachukua siku ngapi? Tujaribu kutabiri.
Jee mahakama ya kadhi ni siku ngapi?
Na kadhalika - weka hapa.

Kweli hadi ina bore, wajumbe wengine wa BMK hadi wanatoa machozi wakati hata kazi haijaanza, wengine wameanza kufunga virago kurudi makwao maana ina bore na hawakufuata posho bali kazi ambayo imekwama kwenye hatua tu ya chekechea.

Jamani tukubali hili jambo halitawezekana, watuache tu tukalale na ka katiba ketu ka zamani ambako kanatosha kabisa na tumedumu nako miaka 50 kwa amani na utulivu.
 
CCM kama siyo wanafiki, tunaomba sheria ya kura ya maoni ibadilishwe ili wananchi tupige kura ya WAZI pia ili tuwafahamu wanachama wanaokwenda kinyume na matakwa ya chama chao!
 
Hili ni tendo la kikatiba hivyo kura lazima iwe ya wazi ili watanzania washuhudie kazi waliyotutuma.
 
CCM kama siyo wanafiki, tunaomba sheria ya kura ya maoni ibadilishwe ili wananchi tupige kura ya WAZI pia ili tuwafahamu wanachama wanaokwenda kinyume na matakwa ya chama chao!
Hapa hatumpigii kura mtu tunapigia kura katiba siri ya nini.
 
Sasa tuendelee au waendelee kuvutana hivi hadi siku au miezi mingapi? Kamati ya maridhiano au mashauriano hadi jana imeshindwa kuridhiana. Sasa tuendelee tu hadi lini? Kwenye 2 au tatu si itachukua mwaka kama hali ndiyo hii! Suali lilikuwa tutabiri issues hizi zitachukuwa muda gani? Ninaanza kwa kutabiri 2 na 3 itachukua miezi 5.
 
Back
Top Bottom