Nchi imepatwa na ugonjwa mbaya sana. Ugonjwa wa kukataa kufikiri.
Hivi kipi hamjakielewa kwa BMT. Wao washasema, tatizo ni katiba za Simba na YANGA.
BMT wameenda mbali zaidi na kushauri Simba na YANGA zianze kwa kubadilisha katiba zao kwanza. Mbona iko wazi hii.
Watu wa Simba na YANGA mnaleta mambo kama ya Burundi. Walipojiunga ICC, walipewa na katiba. Hawakuisoma. Ghafla wanakurupuka kujitoa. Wakaambiwa someni katiba kwanza. Kurudi kuisoma aibu.
Wenye macho na akili zao waliyaona haya pale YANGA zamani sana. Wakataka kuanzisha kampuni, wenyewe wanachama wakaleta unafiki, wakaikataa kampuni.
Leo tena washasahau. Kinachotokea leo YANGA ni matokeo ya kuikataa Yanga Kampuni.
Ajabu povu lote mnalipeleka kwa BMT. Mshasahau.