Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine ameruhusiwa kutoka hospitali baada ya jana kudaiwa kupigwa risasi katika mzozano na maofisa wa usalama Mji Mkuu wa Kampala.
Bobi Wine aliyekuwa amelazwa Hospitali ya Nsambya ameruhusiwa kutoka leo Jumatano Septemba 4, 2024 baada kufanyiwa upasuaji mdogo katika mguu wake wa kushoto.
Kwa mujibu wa madaktari waliomfanyia upasuaji mdogo wa mguu wa kushoto uliopata majeraha wakati wa mabishano na polisi wamesema wamemtoa vipande vya vilipuzi vya machozi.
Wamesema kuwa Bobi Wine itakuwa alipata jeraha hilo baada ya kirungu cha machozi kumfyatukia kwenye mguu wake wa kushoto na kumsababishia jeraha hilo ambalo jana chama chake walidhani kuwa ni la risasi.
Jana, Msemaji wa Polisi Uganda, Kituuma Rusoke alikanusha tuhuma za Bobi Wine kupigwa risasi na kusema kuwa alijikwaa wakati anaingia kwenye gari yake na kusababisha jeraha kwenye mguu.
Soma Pia: Bobi Wine apigwa risasi ya mguu katika vuta n'kuvute na polisi
"Maofisa wa polisi kwenye eneo la tukio wanadai kuwa (Bobi Wine) alijikwaa wakati akiingia kwenye gari lake na kusababisha jeraha, huku Bobi Wine na timu yake wakidai kuwa alipigwa risasi," amesema Rusoke.