Bobi Wine kufikishwa katika Mahakama ya Kijeshi ya Gulu, leo Agosti 23

Bobi Wine kufikishwa katika Mahakama ya Kijeshi ya Gulu, leo Agosti 23

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,046
Reaction score
3,971
Mbunge ambaye aliwahi kuwa mwanamuziki nchini Uganda Robert Kyagulanyi jina maarufu Bobi Wine leo anatarajiwa kufikishwa katika mahakama ya kijeshi mjini Gulu kaskazini mwa Uganda.

Taarifa hiyo imewashtua mawakili wake ambao awali waliambiwa kuwa kesi itasikilizwa katika kambi ya kijeshi ya Makindye anakoshikiliwa mjini Kampala.

Wakati huo huo Mtandao wa haki za binadamu za waandishi wa habari nchini Uganda umetoa saa 48 kwa jeshi kuwatambulisha askari wake waliowajumu waandishi wa habari.

Bobi Wine amewaajiri mawakili kutoka Marekani kumwakilisha kwenye kesi.

Kwa upande mwingine, Wanamuziki wakubwa wakiwemo Chris Martin , Angelique Kidjo na Damon Albarn, wametoa waraka wa kuachiwa kwa Mbunge huyo.

Mbunge huyo ameshatimiza wiki moja tangu kukamatwa kwake na akiwa na mbunge mwezake na zaidi ya watu 30.

Wakili wa Bobi Wine anasema kuwa mteja wake ameteswa sana na jeshi, lakini jeshi kwa upande wao wanakataa kumtesa.

Anatarijiwa kufikishwa mahakamani juu ya madai ya kumiliki silaha kinyume na sheria.

Waraka huo umeanzishwa na Rikki stain aliyekua msimamizi wa zamani wa mawamuziki fella Kuti ambaye alikua mkosoaji mkubwa wa Serikali ya Nigeria

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lidikteta uchwara la hovyo kabisà na ile misuti yake mikubwa mikubwa
 
nn kimekumba e afrika wenzetu wa w afrika wamejiondoa kwnye utawala wa kimabavu sisi east afrika ndyo tunaka kuelekea huko huko kwnye mabavu.sijui huyu mwalimu wetu n nani
 
Back
Top Bottom