Bobi Wine: Mtoto wa Museveni 'anajigamba' jinsi alivyowaua watu 22

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722

​

Kiongozi wa upinzani wa Uganda Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine, anadai kuwa watu zaidi ya 100 wameuawa tangu wiki iliyopita na sio 22 kama alivyoandika mtandaoni mtoto wa Rais Yoweri Museveni na Mkuu wa Jeshi la nchi hiyo Jenerali Muhoozi Kainerugaba.

''Jana usiku mtoto wa Museveni alipokuwa akitoa vitisho vya kuniua alionekana ''kufurahishwa'' na hatua ya kuuawa kwa wafuasi wetu 22 (kwa kweli, amewaua zaidi ya 100 tangu wiki iliyopita)'', aliandika kwenye mtandao wa X, alipokuwa akijibu vitishovilivyotolewa dhidi yake na Jenerali Muhoozi.

Wine hajaonekana hadharani kwa siku kadhaa na anasema amejificha, akidai alitoroka uvamizi wapolisi nyumbani kwake.

Chanzo: BBC
 
Mziki mwingine umewaka huko webale sebo
 
Joseph kony yupo sahihi.... secret ballot haifanyi kazii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…