Bocco asaini miaka miwili simba

amygdala

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2016
Posts
1,082
Reaction score
997

STRAIKA aliyeifunga Simba mara nyingi kwenye rekodi za mashindano yote, John Bocco ‘Adebayor’


STRAIKA aliyeifunga Simba mara nyingi kwenye rekodi za mashindano yote, John Bocco ‘Adebayor’ amesaini miaka miwili Msimbazi.

Hakuna mchezaji yeyote wa ndani na nje anayeifikia rekodi ya Bocco kuinyanyasa Simba akiwa na Azam ambayo ilitaka kumpa mkataba wa kishikaji.

Nahodha huyo aliyeipandisha daraja Azam, amesaini mkataba wa miaka miwili kuhitimisha mazungumzo yaliyoanza wiki iliyopita ambapo juzi Jumanne yalikamilika huku Bocco akiridhia dau la Sh48 milioni na mshahara wa Sh4 milioni ambao atapewa na Simba.

Simba imemaliza ishu hiyo wakati ambapo Bocco alishafanya mazungumzo ya awali na Yanga ambao bado akili zao zinaonekana kujikita zaidi kwenye furaha ya ubingwa na mkwara wa Mwenyekiti wao, Yusuf Manji ambaye amebwaga manyanga. Lakini Mwanaspoti linajua kwamba Manji hataondoka Yanga licha ya wadau na vikundi mbalimbali kujipanga kwenda kumwomba abadili uamuzi.

Chanzo hicho kinasema kuwa Simba wameanza kufanya usajili wao kimya kimya ambapo sasa watahamia kwa kipa wa Azam, Aishi Manula na beki wa Mbao FC, Mrundi Yusuph Ndikumana ambaoa wote mikataba yao imemalizika. Aishi anatakiwa pia na Singida United.

“Bocco tayari amesaini mkataba huo akiwa mchezaji huru, ni mchezaji mzuri ambaye atawapa changamoto akina Laudit Mavugo, pia Aishi naye mazungumzo yanaendelea na muda wowote yanaweza kukamilika, tunamuhitaji Aishi ili ampe changamoto Daniel Agyei,” kilisema chanzo hicho.

“Tulikuwa tunamuhitaji zaidi Mbaraka Yusuph lakini anaonekana kutokuwa tayari kurudi Simba, ni kama ilivyo kwa Shomary Kapombe naye hana utayari huo japo tunahitaji huduma zao.

“Usajili tutakaoufanya utazingatia mahitaji yetu kwa msimu ujao.”

Mbaraka yeye ana ofa tatu mkononi ambazo ni Yanga ambao wapo tayari kumpa Sh50 milioni kwa miaka miwili, Azam FC wenyewe wamedaiwa kutoa ofa ya Sh 15 milioni kwa mkataba wa mwaka mmoja na Singida United ambao ofa yao haijawekwa wazi.

Kiongozi huyo alisema kuwa wachezaji ambao wanadengua kusaini mikataba mipya huenda wasiwabembeleze tena ni pamoja na Ibrahim Ajibu anayetajwa kuwaniwa na Yanga, Jonas Mkude na Abdu Banda.

Habari za ndani pia zinasema wakongwe Mwinyi Kazimoto na Method Mwanjali ambao mikataba yao inamalizika nao hawatapewa mikataba mipya wakati kipa Manyika Peter Jr atapelekwa Lipuli kwa mkopo.


BOCCO ASAINI MIAKA MIWILI SIMBA
 
Dah, hii ndo teknik ya kumzuia asitufunge, jamaa katunyanyasa sana huyu na katigharim msimu huu, tungedroo na azam point moja muhimu sana!
 
Hao kina ajib, mkude na banda labda wawnde singida utd, wakienda yanga wajue wanapishana na gari la ubingwa na malipo mazuri, yanga iliyolemazwa kumtegemea Manji itakuwa ngumu sana, hata demigod anajua!
 
Dadekiii badala wasaini mastraika wa maana wanatusainisha mabubu
 
Hao kina ajib, mkude na banda labda wawnde singida utd, wakienda yanga wajue wanapishana na gari la ubingwa na malipo mazuri, yanga iliyolemazwa kumtegemea Manji itakuwa ngumu sana, hata demigod anajua!
Nyimbo zenu mnazianza tena(Eti Yanga awi Bingwa). Unataka kusema Billion 5 za sport pesa zitashindwaje kumfanya Yanga awe Bingwa tena ikiwa msimu wa 2016/17 ilitumia Billion 2.

Kuwa muwazi ya Kwamba mnaogopa uwepo wa Ajibu Yanga kuwa atafanya Makubwa!

Alichokifuata Kessy pale Yanga SC ndio hiko hiko kitamleta Ajibu pale Jangwani.

Mfano mzuri waulize akina Barthez, Tambee, Yondani waliofuata Mafanikio Jangwani.

Namalizia kwa hii Quote:

"Hata Simba isajili namna gani, haitokuja kuchukua kombe la Ligi Ku".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…